Poleni kina mama hayo ndo matokeo ya kuchagua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poleni kina mama hayo ndo matokeo ya kuchagua CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msema hovyo, Jul 3, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  VillageWomen1.jpg
  Hawa akina mama wanatumia zaidi ya masaa matatu hadi manne kuchanja kuni huko maporini, na wanajiweka katika hatari ya kuumwa na nyoka. Lakini zaidi ya yote, wanakata miti iliyo kwenye chanzo cha maji jambo ambalo linachangia sana kuharibu mazingira na kusababisha ukosefu wa maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme. Wakati hawa akina mama wakikata kuni, wababa upande wa pili wanachoma mkaa, kuzidisha athari ya uharibifu wa mazingira.
  Lakini tukumbuke kwamba gesi inazalishwa pale Mtwara, nchini tanzania, si ya kununua kutoka nje. Kama tungesambaza gesi nchi nzima na kwa bei rahisi, hakuna mtu angekata kuni wala kuchoma mkaa. Kwa kufanya hivyo tungetunza mazingira, tungeokoa muda unaotumika na hawa kina mama kuchanja kuni, tungewaokoa na hatari ya kujikata au kuumwa na nyoka, na zaidi sana tungepunguza gharama ya maisha kwa watanzania walio wengi ambao wanategemea sana mkaa na mafuta kwa ajili ya kupikia. Lakini kwa kuwa watanzania na hasa hawa akina mama maskini, ndiyo waliochagua CCM, basi hawana budi kula jeuri yao. Poleni sana kina mama, next time msiipe kura CCM.
   
 2. A

  AZIMIO Senior Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Labda kama watakumbuka, ni wepesi kusahau
   
 3. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umaskini huwa unawafanya wadanganyike haraka na khanga, tshirt, chumvi na buku kumikumi za CCM. Kwa hiyo umaskini wa watanzania ni mtaji wa CCM. full stop
   
 4. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni ajili ya matatizo walio nayo!
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakuunga mkono katika suala zima la matumizi ya gesi. Kwa kweli haileti maana kabisa kuzalisha gesi mtwara halafu wananchi si dar wala vijijini wanaendelea kupikia mkaa na kuni. Yaani hovyo kabisa huyu waziri wa nishati na madini.
   
Loading...