Poleni jeshi la polisi

ngurutu

Member
Mar 31, 2017
54
50
Naztoa kwa dhati pole zangu kwa askari walo poteza maisha ,ni kweli askari ni nyama ya risasi lakni si kufanyiwa unyama huu naimani na watanzania wezetu ambao wamejawa na visasi ,na chuki ambazo mpaka sasa hatujui sababu ni nini, kwasababu nmepita hko najua jinsi gani askari anatengenezwa na kuandaliwa hadi kuitwa askari ni ghalama kubwa sana na nguvu kubwa sana hutumika kumuandaa askari mmoja ,so anapo potea askari mmoja tena kwa chuki za watanzania wenzetu kiukweli ni msiba mkubwa sana , lakn hpa kuna mambo kama 2 au 3 ya kujifunza jpo tunaambiwa tujifunze kwenye makosa ya wengne lakn sababu ishatokea hbu tuyatazame hya mambo kidogo hasa kwa mtazamo wangu

1.Kwa mtazamo wa haraka hawa ni watanzania wasaliti ambao wana mafunzo au washawh kuptia mafunzo ya aina flani ukitaka kulijua hli njia inayo tumika hasa kuwaua askari ni AMBUSH njia hii kwa askari yoyote watakubaliana na mimi kuwa ni ngumu kutoka mkiwa hai hata mkiwa 100 mkiwa kwenye target hatoki mtu ni njia mbaya sana ,na hapo hta kma askari mmeiva vipi ni qudra za mungu ndo ztakazo baki kuokoa maisha

2.Pili njia wanayo tumia kuua raia ni njia ya kawaida jpo wanahakikisha hyo mtu wanamjua vizuri ili wasimdhuru mtu ambae hausiki

Hapa cha kujifunza ni kwamba hta mnapo kuwa kuwa kweny uwanja wa medani(battle ground) mtu ambae hausiki hamruhsiwi kumgusa kwa mantiki hii sababu wana mafunzo na wanalijua hili wanajthd wale watu walo walenga ndo hao wanawatia kwenye target.

3.Nguvu inayo tumika ,kuonesha kma hawa wana mafunzo ambayo wamepata ,kuna tofauti kubwa nguvu wanayo tumia kati ya askari na raia,nguvu inayo tumika kuwa vamia askari wetu ni kubwa sana ukilinganisha na raia sababu wanajua ni aina gani ya kundi wana pambana nalo.

4.Wepesi katika kufanya matukio,

5.wanajua vizuri nguvu ya adui wanayo pambana nae

6.To take cover, hili pia nisomo ambalo mtu wa kawaida ambae hajapitia mafunzo ni ngumu kulitklza lkn sababu wana mafunzo wanalimudu

USHAURI
1.watanzania na hasa wana pwani hii vita tukiiachia majeshi yetu ni ngumu kushinda au itachukua muda sababu wanao fanya ni miongoni mwa jamii yetu na tujue hakuna vita inayo piganwa na mtu mmoja ushrkiano ndo kila kitu katika mapambano,

2.Lakn majeshi yetu pia yajue "no easy task on the battle ground" hakuna jukumu rahsi katika uwanja wa medani,pia hakuna adui mtoto ,adui ni adui na ashghlikiwe ipasavyo sababu najua uwezo upo tukiweka dharau mambo yatakuwa magumu

3.ushauri kwa serikali:pamekuwepo na wimbi kubwa la vijana wa walo pitia mafunzo ya awali ya kijeshi hasa kwa kijitolea ambao hawa kubahtika kupata nafasi kujiunga na majeshi yetu ambao wapo mtaani bila shughuli maalum na miaka ya nyuma unaweza kukuta OP nzima imerudi au nusu yake na tunajua vjana wengi wakujtolea ni form4 au darasa 7 kma wakikutana na watu ambao si wazalendo na hawana uchungu na nchi hii ni rahisi sana kushawishika na kujiingza kwenye makundi mabaya na kuharibu maisha yao na malengo yao..

Kwamfano, mwaka jana kulikuwa na kuandkisha majina ya vjana ambao wamptia jkt kwa baadhi ya mikoa taarifa zlikuwa informal lkn zoezi lilikuwa formal na Dar es salaam lilifanyika karibu wilaya zote binafsi nlienda sababu kuna mtu nlimsndkza lakn kwa Temeke mpaka sa tatu asbh palikuwa na vjna takrbani 300 na zoezi lili kuwa la siku 3 harafu taarifa zlikuwa not formal,lakn pia nljrbu kudadisi na kugundua kuwa wengi kuanzia op mkapa na kuendlea wengi wapo mitaani bila shughli maalumu, kiusalama si jambo zuri sana

4.kuna haja ya kuwepo na taarifa za vijana walo pitia mafunzo ya kijeshi hasa baada ya kuisha mikataba yao ili kujua kijana flani yupo sehmu flani na anajishghlisha na nn,ukarbu hu utazuia vjana kujiingza kwenye makundi yasiyo faa sababu wanajua wanafuatiliwa

OMBI
Kuna haja ya kupunguza vijana walo pokea mafunzo hasa ya kijeshi mtaani na ambao hawana shughuli maalum ili wasije kutmbukia katika madimbwi yasiyo na tija kwa taifa eidha kwa 1.kuwapa mitaji au kuwatfia ajira rasmi

Mwisho kabisa napongza hatua znazo chkuliwa na wizara ya ulinzi katika mapambano hayo ,lakn watanzania tunapaswa kuwapa suport askari wetu maana kupigana na kikundi flani ni ngumu bora upgane na nchi kuliko kikundi lakn umoja ni nguvu
 
ngurutu ni wazi fika upo katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na inatakiwa uelewe kuwa jambo halijakaa sawa ngoja niishie hapo
 
Mwalimu Nyerere alitufundisha kuishi kwa Amani na utulivu upendo Kiswahili ikawa lughayetu kwa pamoja hatukupenda vita wala ukabila, Lakini kaja shetani mmoja ametuvuruga visasi kila kona, tumepoteza undugu. Kilamtu anataka amfurahisheahuyu shetani bila kujua kua visasi vinaweza kulipwa kwa baadae. Shauri ya shetani huyu sasa.
 
kwa mtazamo wangu kupambana na ugaidi inakuwa ni kitu kigumu sana,kwa kuwa yeye anakua anajua anakufa hapo hapo wakati wewe hujui utakutwa wapi,London yanatokea na kwingine kwingi,makubaliano ni best option
 
Umenena vyema kabisa... Hili jambo sio la kuchukuliwa kimzahamzaha... Hiki kikundi kina nguvu isiyohitaji mzaha...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom