Poleni Clouds, Ni wakati sasa msaada wa kisaikolojia utolewe kwa wafanyakazi

mayowela

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,124
2,000
Poleni sana Clouds Media kwa msiba mwingine alfajiri hii ya leo wa Mtangazaji ambae sio siri ana wafuasi wengi sana ambao ni wasikiizaji wa kipindi cha Jahazi Ephraim Kibonde aka Kibs,

Kibs ameonekana kama Mshehereshaji kwenye msiba wa kiongozi wake Ruge pale Karimjee mpaka Bukoba, lakini inavodaiwa huko huko Bukoba alianza kujisikia vibaya mpaka siku anaondoka kuja Mwanza anashushwa airport alikuwa akijisikia vibaya zaidi inadaiwa ni presha na hatma yake alfajiri ya leo ametutoka.

Tangu alipopatwa na msiba wa mke wake mwishoni mwa mwaka jana na kurejea kazini mimi binafsi niliona hayuko sawa na kumtaja marehemu mke wake hakukumuisha ilikuwa kama nikujifariji nakukumbuka mema na uvumilivu wa mke wake kwenye ndoa yao, ila kwenye moyo hatujui aliumia vipi kuondokewa na mkewe

Picha aliyoweka juzi kwenye mtandao wa Instagram baada kumpumzisha Ruge ilinifikirisha sana na sikupata jibu, yaweza kuwa kuendesha shughuri ya kumpumzisha Ruge ili muingia sana rohoni mpaka kumkumbuka marehemu mkewe nakupelekea hari yake kiafya kubadilika, ni siri kubwa,

Poleni Clouds, ni siku chache timu ya uzalishaji ilipokuwa inarudi Dar es salaam kutoka Bukoba, walipata ajari maeneo ya nje ya mji wa Dodoma, wakati bado machungu hayajawaisha, poleni sana

Pole Gardner na George team mate ameondoka, mtaimisi san radha yake kwenye kipindi cha Jahazi, George naamini Kibs alikuwa kama kaka yako na ulijifunza mengi kwa kuwa karibu nae, Pole sana kaka, Gardner maumivu uliyonayo siwezi kuyaelezea na ukaribu uliokuwa nao na Marehemu Kibs ni wa muda mrefu, your partner is gone bro, pole sana.

Clouds mlikuwa mmeanza kujipanga kuanza vipindi rasmi na mdogo mdogo mlikuwa mmeanza kurejea ila mmepatwa na mtihani mwingine mgumu sana kuuelezea, sasa ni wakati wa timu nzima kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kurejea kwenye hari na kufnya kazi yote ni mapito, kiongozi mkubwa hana hata wiki tatu mtihani mwingine kwa mtangazaji mkubwa sana sana, simanzi lake halielezeki,

Poleni Clouds Media

Uhai ni Zawadi Kifo ni Lazima,

Pumzika kwa amani Kibs, (Kuzimu hakuna Biaaa,)
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
CMG wanapitia kipindi kigumu.

Kwanza kama taasisi kuondokewa na Mkurugenzi 'kichwa' kama Ruge Mutahaba sio pigo dogo. Sote tumeshuhudia kishindo chake.

Jumlisha na kupata msiba mwingine wa Ephraim Kibonde, miongoni mwa watangazaji mahiri na mwenye ushawishi mkubwa, ikiwa ni siku chache baada ya mazishi ya Ruge. Tena sababu ikiwa ni msiba wa awali. Acha kabisa!

Kwangu naona misiba hii inawavuruga wafanyakazi ambao wengi ni vijana pale mjengoni na bado wanatakiwa kufocus ili kazi ziende.

Ukifuatilia hisia zao mitandaoni; videos, picha na hata jumbe wanazoandika unaona kabisa huzuni waliyonayo na hakika inaweza kuwaathiri sana kisaikolojia. Pengine na uoga ukawaingia.

Wapo watakaovunjika moyo na kupata mtikisiko wa kiimani pia. Wapo wanaoweza hata kukufuru au kupoteza morali kabisa. Si ajabu wengine wakaugua na kupoteza maisha kwa kihoro (God forbid).

Nashauri uongozi uangalie namna ya kitaalamu ya 'kuwatibia' hawa vijana. Wawe na therapy ya ukweli. Hii ni kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya taasisi.

Au ndio yatapita tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
2,210
2,000
Hata wakivunjika moyo na kupata mfadhaiko kisha wakapoteza maisha kwa kihoro yote itakuwa ni kazi ya Mungu si ndo mnavyosemaga yanini sasa mtake kuipinga mipango ya Mungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
Hauna ndugu zako waliofiwa na wana huzuni?ungeanza nao hao kwanza,usi judge hisia za mtu kwa kuona post za mitandaoni hao wengi ni wasanii wasikuumize kichwa!Alikufa Steve Jobs na Apple haikutetereka itakua hao jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kama una hasira mkuu?

Ni ushauri tu.

Hao wafanyakazi wa Apple una uhakika hawakuwa na therapy sessions?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,682
2,000
CMG wanapitia kipindi kigumu.

Kwanza kama taasisi kuondokewa na Mkurugenzi 'kichwa' kama Ruge Mutahaba sio pigo dogo. Sote tumeshuhudia kishindo chake.

Jumlisha na kupata msiba mwingine wa Ephraim Kibonde, miongoni mwa watangazaji mahiri na mwenye ushawishi mkubwa, ikiwa ni siku chache baada ya mazishi ya Ruge. Tena sababu ikiwa ni msiba wa awali. Acha kabisa!

Kwangu naona misiba hii inawavuruga wafanyakazi ambao wengi ni vijana pale mjengoni na bado wanatakiwa kufocus ili kazi ziende.

Ukifuatilia hisia zao mitandaoni; videos, picha na hata jumbe wanazoandika unaona kabisa huzuni waliyonayo na hakika inaweza kuwaathiri sana kisaikolojia. Pengine na uoga ukawaingia.

Wapo watakaovunjika moyo na kupata mtikisiko wa kiimani pia. Wapo wanaoweza hata kukufuru au kupoteza morali kabisa. Si ajabu wengine wakaugua na kupoteza maisha kwa kihoro (God forbid).

Nashauri uongozi uangalie namna ya kitaalamu ya 'kuwatibia' hawa vijana. Wawe na therapy ya ukweli. Hii ni kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya taasisi.

Au ndio yatapita tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwongozi gani? Kiongozi wa uongozi wa juu kafa, unadhani nani wa kumjenga mwenzie kisaikojia? Kwa ufupi watu wote wa clouds hawako sawa, labda watu wa nje ya clouds kama MCT au wataalam wa saikoloji kutoka wizara ya habari.
 
julnd

Senior Member
Jan 4, 2019
116
225
Wazo zuri itasaidia kwa kiasi Fulani - wapewe na ushauri nasaha pia.
CMG wanapitia kipindi kigumu.

Kwanza kama taasisi kuondokewa na Mkurugenzi 'kichwa' kama Ruge Mutahaba sio pigo dogo. Sote tumeshuhudia kishindo chake.

Jumlisha na kupata msiba mwingine wa Ephraim Kibonde, miongoni mwa watangazaji mahiri na mwenye ushawishi mkubwa, ikiwa ni siku chache baada ya mazishi ya Ruge. Tena sababu ikiwa ni msiba wa awali. Acha kabisa!

Kwangu naona misiba hii inawavuruga wafanyakazi ambao wengi ni vijana pale mjengoni na bado wanatakiwa kufocus ili kazi ziende.

Ukifuatilia hisia zao mitandaoni; videos, picha na hata jumbe wanazoandika unaona kabisa huzuni waliyonayo na hakika inaweza kuwaathiri sana kisaikolojia. Pengine na uoga ukawaingia.

Wapo watakaovunjika moyo na kupata mtikisiko wa kiimani pia. Wapo wanaoweza hata kukufuru au kupoteza morali kabisa. Si ajabu wengine wakaugua na kupoteza maisha kwa kihoro (God forbid).

Nashauri uongozi uangalie namna ya kitaalamu ya 'kuwatibia' hawa vijana. Wawe na therapy ya ukweli. Hii ni kwa maslahi yao binafsi na maslahi ya taasisi.

Au ndio yatapita tu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
851
1,000

Naunga hoja mkuu. Hili inabidi lifanywe na CMG. Japo naona kuna wanaokupinga hapa lkn nadhan hawajawahi kupitia Mental and psychological problems kama depression, intense fear of failure, etc...

Hii inaathiri sana mwili wa mtu katika sehemu zote, yaan Kiroho, Kiakili, kimwili na kijamii.

Therapy ya maana inahitajika kwa watu hawa ili wapate kukubaliana na kilichotokea...

Kwa mnaopinga ombeni siku moja iwatokee depression ndipo utaona jinsi inavyotesa sana akili na mwili.
 
kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
851
1,000
Hauna ndugu zako waliofiwa na wana huzuni?ungeanza nao hao kwanza,usi judge hisia za mtu kwa kuona post za mitandaoni hao wengi ni wasanii wasikuumize kichwa!Alikufa Steve Jobs na Apple haikutetereka itakua hao jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu training ya wafanyakazi wa Apple sio kama ya wafanya kazi wa Clouds. Sio rahisi kufanyia kazi makampuni makubwa kama hawajafaham vzr personality yako na jinsi unavyoweza ku cope na stresses.

Pia huko nje wafanyakazi na pia wanavyuo hupewa kozi ya personal development ambayo inasaidia sana kuwajengea moyo wa kupokea kile kinachotokea. Sasa unapolinganisha CMG na Apple sifhan kama uko sahihi
 
ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
2,210
2,000
Ushajiuliza kwanini nchi zilizoendelea zina high life expectancy?

Miongoni mwa sababu ni kutochukulia poa suala la afya..

Sent using Jamii Forums mobile app
Toa kwanza msaada wa kisaikolojia kwa ndugu zako na familia yako hasa hsa ndugu zako kabisa wa familia na uko wako acha umbea na kujipendekeza kwa aina hii yaani wewe unataka kutwambia kwamba unawathamini na kuwapenda zaidi wafanyakazi wa clouds kuliko ndugu zako wa damu na uko. acheni unafiki na kujipendekeza watanzania p

A.........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom