Pole sana Singasinga seth wanasiasa wamekusaliti, kwenye shida hakuna undugu..

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
2,362
4,851
Mwana falsafa au maarufu kama mwana FA Kwenye wimbo wake wa 'unanijua unanisikia' kuna shairi alighani "ukiwa fukara kamwe huwezi kuwa kiburi, masikini jeuri ni msemo tu usiweke kwenye akili..." Mara baada ya kashfa kubwa ya ESCROW iliyopelekea bunge kuja na maazimio mengi kwa serikali, ikiwemo kumkamata aliyeitwa 'fisadi' singa singa Seth na kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi. Katika hali ya kushangaza SETH hakukamatwa na badala yake akawafungulia kesi na kuomba fidia ya mamilion kwa baadhi ya wanasiasa waliomtuhumu, lahaula!!! Jeuri ya pesa!

Seth alionesha kibri ya fedha, Seth alijiamini wala hakukimbia nchi, wala hakukamatwa na serikali badala yake alienda kuwapa msaada serikali kwa kulipa msaada Jeshi la polisi. Huyo ndo alikua Seth almaarufu singa singa. Japokua nilikua mwanafunzi wa bachelor mwaka wa pili tu wakati huo, ila akili zangu fupi zilitosha kunihakikishia kua nyuma ya Seth alikuepo mtu mzito aliyempa kibri huyu singa singa. Isingewezekena wabunge 300 waishauri serikali na serikali ilipuuze bunge, isingewezekana.

Ashakumu si matusi, na hakuna marefu yasio na ncha singa singa yakamkuta. Leo hii anaandika barua kuomba radhi, wale waliompa jeuri wanamtazama tu, si kwamba hawapo, wapo ila wanalinda majina yao. Jela anakaa peke yake mahakamani anaenda kujibu peke yake aliokula nao wanaitwa viongozi wastaafu... Au waheshimiwa wastaafu.

Moyoni mwa Seth atakukua na hasira na wanasiasa hawa, wamemtumia sasa wanamuacha kama ilivyo mipira ya kiume baada ya kutumika. Watu wagumu wanapita ila nyakati ngumu hazitapita, pole singa singa.
 
Kaomba radhi buana, kagundua kukusaidia ndooni hakuvumiliki.

Kafanya hesabu mtu huru ndio mwenye nuru. Gereza Ni Kama tanuru.
 
unaweza kuomba msamaha under pressure,hiyo inakubalika hata mahakamani baadae msamaha unaweza kuwa void,
 
Back
Top Bottom