Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi.

La muhimu ni namna walivyo "behave" walipoachiliwa. Hatukuwasikia wakituambia unayotuambia mtani. Unafikia hata kumuudhi aliyekusamehe! Kwamba hakuna aliyekuhurumia bali umetoka kwa nguvu ya umma? Really? Ipi? Ni nguvu ipi ya umma unafanya kazi kwenye kutoa watu jela lakini inashindwa kuzuia watu wasiende jela? Mtaniii?

Mtani ushakuwa mtu mzima na uzee ushabisha hodi. Haipendezi kila siku uwe wa vituo vya polisi, jela na mahakamani ! Mtani kuna marafiki wa kweli na kuna wapambe! Hebu tusikilize marafiki wa kweli.

Achana na siasa fanya biashara. Na kama siasa ndio biashara yako basi acha siasa za kibabe. Hazilipi kwa kuwa sifa ya ubabe ni sifa ya serikali zoote duniani. Hakuna chombo au mtu anaweza kuwa mbabe kuliko serikali.

Dai chochote kwa kistaarabu utaeleweka. Serikali kuiambia hupoi, mpaka kieleweke, una kiberiti, utafanya nchi iwe Libya, n. k. haifai. Serikali ina uwezo wa kufanya hicho kibiriti kikuchome mwenyewe! Serikali ina uwezo wa kufanya wéwé peke yako uishi kama uko Libya!

Mtani hakuna sifa ya mtu kutembelewa na watu wengi gerezani, Sawa na mgonjwa ajisifie kutembelewa na watu wengi kitandani akiwa wodini It's an illusion! Haimfanyi awe mgonjwa bora kuliko wagonjwa wengine!

Mtani miaka inasonga hairudi nyuma. Na ukweli ni kuwa bado hauna hiyo "nguvu ya umma". Wenye nguvu ya umma hawakamatwi usiku, wakasafirishwa usiku, wakakaa ndani miezi 8 Huku wenzake wanachomudu ni kuvaa t-shirt zenye hukumu!

Sikupenda walichofanya UAMSHO lakini nimependa busara zao baada ya kuachiwa. Ukiziiga utakuwa salama. Ukifuata wapambe basi utatembelewa tena jela. Na hao wapambe watalala na kula makwao wewe ukilia njaa. Jela hakujawahi kuwa kuzuri hivyo sio mahali pakupenda kwenda.

Wenzako wanaokupa moyo Mtani kina Godbless Lema na Tundu Lissu wapo ughaibuni wanakula maisha na kuendesha shughuli zao huku wakilipwa madola kila mwezi. Usiwe mjinga, jua limezama shtuka!

Umelia kwa uchungu sana Mtani kila uliposimulia miezi yako 8 jela, itoshe kusema imekufunza. Ogopa mwanaume kulia kwa kiwango kile tena mbele ya umati akiwa na mke wake kando yake.

Anyway, akili ni nywele!
Screenshot_20220309-085059_1646805113095.jpg
 
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi...
Huyu ni mwanasiasa, kwahiyo kila jambo lazima alipeleke kisiasa. Anatumia kifungo chake kama njia ya kuwarubuni watu ili aongeze wanachama zaidi, na muda sio mrefu ataanza kuomba michango ya chama ili aende zake Dubai akapumzishe akili na familia yake, huku akiwaacha wachangaji wakilia kuhusu ugumu wa maisha nk. Jamaa anajua kucheza na akili za watu, ndio maana amefanikiwa kukusanya akili za mamilioni ya wafuasi wake na kutembea nazo mfukoni kwake.
 
Huyu ni mwanasiasa, kwahiyo kila jambo lazima alipeleke kisiasa. Anatumia kifungo chake kama njia ya kuwarubuni watu ili aongeze wanachama zaidi na muda sio mrefu ataanza kuomba michango ya chama ili aende zake Dubai akapumzishe akili na familia yake, huku akiwaacha wachangajiwa wakilia kuhusu ugumu maisha nk. Jamaa anajua kucheza na akili za watu ndio maana amefanikiwa kukusanya akili za mamilioni ya wafuasi wake na kutembea nazo mfukoni kwake.
Kumbe una kiri kuwa kuna ugumu wa maisha ulisababishwa na mfumo mbovu wa CCM?
 
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi...
Ushauri mzuri sana ila Mbowe asivyokuwa na hekima nakuhakikishia atarudi jela. Hata yeye angekuwa na serikali wala asingekubali drama na tena yeye angekuwa muuaji na mfunga watu midomo maana kama tu uenyekiti hataki kuachia na kila mwenye dalili za kuonesha anamuua, je angepewa mamlaka?

Nadhani kizazi cha mbowe inapindi kiondoke kwenye siasa kije kizazi kingine chenye kuendesha siasa za kimkakati na kuheshimu utu wa mtanzania
 
Kumbe una kiri kuwa kuna ugumu wa maisha ulisababishwa na mfumo mbovu wa CCM?
Soma vizuri nilichoandika. Inawezekana vipi uchukue hela umpe mtu akale bata na familia yake, afu wewe urudi kwako ukilia njaa. Kwanini hizo hela ulizomchangia mtu usizitumie kwa biashara au mambo mengine ya kimaisha!
 
Ushauri mzuri sana ila Mbowe asivyokuwa na hekima nakuhakikishia atarudi jela. Hata yeye angekuwa na serikali wala asingekubali drama na tena yeye angekuwa muuaji na mfunga watu midomo maana kama tu uenyekiti hataki kuachia na kila mwenye dalili za kuonesha anamuua, je angepewa mamlaka??? Nadhani kizazi cha mbowe inapindi kiondoke kwenye siasa kije kizazi kingine chenye kuendesha siasa za kimkakati na kuheshimu utu wa mtanzania
Dah Chacha Wangwe kadhulumiwa uhai wake kama masihara. Kitendo cha kujaribu kum beep bwana mkubwa kimeyagharimu maisha yake na familia yake. RIP Chacha Wangwe Mungu ataendelea kuwanyima amani wote waliohusika na dhulma ya maisha yako.
 
Ushauri mzuri sana.
Hungera SautiYaMnyonge, siasa anazoendesha mbowe za kuhamasisha vurugu za Katiba Mpya sio za kistaarabu hata kidogo.

Zinaenda pamoja na kashfa, kebehi na kejeri kwa viongozi wa kitaifa.
Mchakato wa Katiba Mpya Waliuanzisha CCM na wakishauriwa vizuri wataumalizia bila kejeri za akina MdudeChadema.

Mbowe anatakiwa ampate mshauri mzuri wa mambo ya kisiasa.
 
Hilo ni sikio la kufa huwa halisikii dawa kamwe. Pia umeongea jambo la msingi kukaa jela sio sifa wala sio ujanja sababu kunyimwa uhuru sio jambo la kujivunia sababu hapo mahakamani akina kibatala wanatokwa jasho kukutetea muda ukiisha we unarudi lupango kwa kalandinga na kwenda kula dona maharage wenzio wanapanda VX wanaenda kula vyuku.

Wanatoka out na familia zao,usiku wana gegeda kwenye vitanda vizuri wakati we saa kumi jioni ushaingizwa kulala selo halafu mtu anajiona mjanja na pia umesomewa mashitaka na kukutwa na kosa la kujibu bado ataona mzaha ngoja akutane na ving'ang'anizi mtaani utapasikia siku unatoka utakuta Dar inafanana na Newyork City.
 
Ushauri mzuri sana ila Mbowe asivyokuwa na hekima nakuhakikishia atarudi jela. Hata yeye angekuwa na serikali wala asingekubali drama na tena yeye angekuwa muuaji na mfunga watu midomo maana kama tu uenyekiti hataki kuachia na kila mwenye dalili za kuonesha anamuua, je angepewa mamlaka??? Nadhani kizazi cha mbowe inapindi kiondoke kwenye siasa kije kizazi kingine chenye kuendesha siasa za kimkakati na kuheshimu utu wa mtanzania
Nyie wapuuzi Mbowe kurudi gerezani halitakuwa jambo la kushangaza, tena zaidi mtakapomtudisha kwa kumbambikia kesi.

Mbowe hawezi kuwa mjinga akavumilia uvunjifu wa sheria mnaofanya kila siku ili mumuite ana hekima. Kuliko kuwa na hekima ya aina hiyo bora aonekane hana hekima kwa wajinga kama wewe na mwenzako mleta mada ili apiganie haki za wanyonge.
 
Dah Chacha Wangwe kadhulumiwa uhai wake kama masihara. Kitendo cha kujaribu kum beep bwana mkubwa kimeyagharimu maisha yake na familia yake. RIP Chacha Wangwe Mungu ataendelea kuwanyima amani wote waliohusika na dhulma ya maisha yako.
Hizi propaganda zenu za miaka 20 iliyopita kwanini hamtaki kuzi update?

Kama una ushahidi wa Mbowe kuhusika peleka polisi then muende nao mahakamani.
 
Nyie wapuuzi Mbowe kurudi gerezani halitakuwa jambo la kushangaza, tena zaidi mtakapomtudisha kwa kumbambikia kesi.

Mbowe hawezi kuwa mjinga akavulia uvunjifu wa sheria mnaofanya kila siku ili mumuite ana hekima. Kuliko kuwa na hekima ya aina hiyo bora aonekane hana hekima kwa wajinga kama wewe na mwenzako mleta mada.
Eti Mbowe kurudi jela si tatizo, mbona wewe huendi huko jela kila siku uko humu jf?
 
Nyie wapuuzi Mbowe kurudi gerezani halitakuwa jambo la kushangaza, tena zaidi mtakapomtudisha kwa kumbambikia kesi...
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari
 
Back
Top Bottom