Kwanza nikupongeze kwa hotuba yako nzuri ya leo inayohusu siku ya wafanyakazi. Umesema ulpoingia madarakani PSPF ilikuwa inadai Serikali zaidi ya 700bn. Lakini kwa uthibitisho wako kabla hujaingia madarakani fedha hizi walizidai bila mafanikio kutoka Serikali ya awamu ya nne. Wastaafu wengi wa Mfuko wa PSPF wamehangaika sana wakifuatilia mafao yao bila mafanikio. Leo hii umetamka kuwa tayari deni hili umelipunguza kwa 500bn na muda siyo mrefu utakuwa umelimaliza. HONGERA SANA Mhe. Rais. Tunakombea ulimalize den hili ili sisi Wastaafu tupate mafao yetu. Sijui viongozi wa awamu ya nne wanajisikiaje kwa haya mazuri anayofanya Mhe .Magufuli. Aibu sana kwa Serikali ya awamu ya nne.