Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,569
Nachukua nafasi hii kumpa pole MPIGANAJI MACHACHARI WA MASLAHI YA TAIFA HILI....Mh. ZITTO, POLE SANA! Pamoja na hayo,uchunguzi wa kitabibu umeonyesha anasumbuliwa na malaria (vidudu 120)! Ni mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wakisisitiza suala la utumiaji wa vyandarua tena vyenye dawa na kwa nia thabiti ya kukomesha malaria nchini,mkuu wa nchi aliwahi kupokea TAKRIMA ya vyandarua alipotembelewa na swahiba wake, George BUSH! Hoja yangu, watu wengi wanasumbuliwa na malaria hadi sasa japo vyandarua vimejaa kila kona na kuna uhamasishaji wa kutosha,tuamini havina uwezo wa kutukinga na malaria au watu tumepuuza kuvitumia!!!?
Mbu wanashambulia sehemu yoyote si wakati wa kulala tuu. Hata ukiwa kwenye mkusanyiko wa vikao vya misiba, harusi vinavyofanyika maeneo ya wazi kama bustanini uwezekano wa kuumwa na mbu ni mkubwa sana. Tuombe tu ipatikane chanjo lakini chandarua inazuia wakati umelala tuu