Pole sana Ally Bananga, sisi ndio makamanda wa CHADEMA, unavuna ulichopanda na iwe fundisho

Bananga alifanya kazi nzuri sana na Lissu, historia itamuandika vyema kwa hilo.

Ila sasa naye kategwa na mfumo kwa sababu mfumo umerusha fupa kwa mkewe. Laiti naye angekuwa hajarushiwa fupa bila shaka angeelewa logic ya chama kukomaa na wale madada 19.

Wale madada wameshiriki kubypass vikao halali vya chama na kwenda kujiapisha, Hilo ndo kosa lao kubwa!. Hakuna chama makini kinachoweza kuvumilia wanachama wanaopoka mamlaka ya kamati kuu ya chama husuika kwa maslahi binafsi!
Mbowe amewahi kuyaacha majina ya viti maalumu yaliyopitishwa na kamati kuu ya chama na kuweka yake kwa maslahi yake binafsi and nothing happened.

Mpaka hapo CDM siyo chama makini according to you.
 
Kama Dr Slaa ambaye alikuwa Rais wa mioyo yao alitukanwa unafikiri kuna atakayepona?

Wote hapo ikiwemo Mbowe&Lissu watakuja kuyaoga tu.

Ni suala la muda tu.
 
Mke wa Bananga n mmoja kati ya wale wamama 19 wa viti maalum, incase akisema anapinga matokeo ya uchaguzi mkuu inamaanisha hakubalian pia na hatua ya akina Mdee pamoja na mkewe.
 
Polepole aliwaita wapinzani kuwa ni corona,basi wakang'aka kweli kwanini waitwe hivyo ila leo wapinzani haohao wanawaita wenzao kuwa ni covid 19.

Tatizo la wapinzani wa bongo hawaamini katika yale wanayoyapigia kelele,walikuwa wanapiga kelele sana kuhusu corona ila ilivyofika kipindi cha uchaguzi wakanyamaza na kufanya uchaguzi na hatuwasikii tena kuzungumzia corona. Wapinzani wa bongo utakuta wanapigia kelele kuhusu uhuru wa kutoa maoni ila hawaamini katika hilo,kwao uhuru wa kutoa maoni tafsiri yake inaishia kwa kuwakosoa serikali tu ila ukiwakosoa wao hapo hakuna tena kuheshimu maoni ya mtu.
 
Polepole aliwaita wapinzani kuwa ni corona,basi wakang'aka kweli kwanini waitwe hivyo ila leo wapinzani haohao wanawaita wenzao kuwa ni covid 19. Tatizo la wapinzani wa bongo hawaamini katika yale wanayoyapigia kelele,walikuwa wanapiga kelele sana kuhusu corona ila ilivyofika kipindi cha uchaguzi wakanyamaza na kufanya uchaguzi na hatuwasikii tena kuzungumzia corona.
Wapinzani wa bongo utakuta wanapigia kelele kuhusu uhuru wa kutoa maoni ila hawaamini katika hilo,kwao uhuru wa kutoa maoni tafsiri yake inaishia kwa kuwakosoa serikali tu ila ukiwakosoa wao hapo hakuna tena kuheshimu maoni ya mtu.
Unaongea utoto gani dogo? Ukimwi kuna wakati ulishikiwa bango sana, je sasa hivi kuna kelele tena? Je kukosekana kelele ni kuwa ukimwi umeisha au umepata dawa?
 
Ukimwi unafananisha na corona?unazeeka vibaya nini? Kubali tu kwamba wapinzani wanapigia kelele vitu ambavyo hata wao hawaviamini,yani wamepiga kelele za corona weee ila walivyoona uchaguzi umefika wakaacha tena hizo wakawa wanafanya kinyume na walichokuwa wanakipigia kelele halafu wewe mzee unakuja kutulinganishia na ukimwi!
 
Ukimwi unaua kama ilivyo corona. Hao wanaopiga kelele kuhusu ukimwi kwani wote wanatumia condom? Usichanganye uhalisia na utekelezaji dogo.
 
Ukimwi unauwa kama corona? Nina ndugu zangu wana ukimwi ila huwezi kuwajua na wana miaka kibao toka wapate huo ukimwi halafu wewe mzee unakuja kufananisha na corona kweli?
 
Habari wanaJF,

Leo kuna jambo ambalo nimeona nilizungumzie. Wengi wetu nadhani tunamjua Ally Bananga, alikuwa diwani wa sombetini huko Arusha na pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu alikuwa ni mmoja wa timu ya kampeni ya Lissu.

Bananga alikuwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakitoa maoni yao vizuri tu kwa kukosoa na kurekebisha pale ambapo kuna kitu hakipo sawa, hakukaa kimya.

Kutokama na umuhimu wake kwenye upinzani, Lissu aliona ni mtu sahihi wa kwenda nae kwenye kampeni za uchaguzi mkuu.

Ukiacha hayo, Bananga alikuwa ni mmoja watu mtandaoni wanaoshambulia sana wenzake wa huko upinzani ambao wameona wafanye maamuzi ambayo kwao wanaona ni sahihi ikiwemo kuhama chama na kama kawaida washabiki wa chadema walikuwa wanamshangilia sana.

Mfano ni kuna kipindi aliwatukana na kuwasema vibaya sana wale akina kubenea na komu walioamua kuondoka chadema, kama ilivyo kawaida mashabiki wa chadema walimshangilia sana.

Leo imekuwa tofauti, bananga hakubaliani na msimamo wa chama chake wa kutotambua uchaguzi, na pale alipojaribu tu kukosoa hilo ameambulia matusi mengi sana na ya kila aina.

Anashangaa na anachukizwa na hayo matusi kutoka kwa walewale mashabiki wa chadema.

Bananga ameenda mbali na kuamua kutoongea tena chochote na kukaa kimya.

Sasa ndugu yangu bananga, wewe kila mara ulikuwa unasema unapigania UHURU WA KUTOA MAONI, cha kushangaza ulisahau kupigania hilo kwenye chama chako.

Ulisema sana kuwa serikali inaminya uhuru wa maoni, ila leo hii chama chako na washabiki wako wamekunyima uhuru wa maoni. Najua una mengi ulitamani kuyasema.

Nakupa pole sana, na iwe fundisho.

Chini ni screenshot za post zake za mwisho

Kusema na kutenda ni tofauti
 
Hizi ndio siasa za Tanzania na upinzani kwa ujumla. Poleni kwa wote mnaochukulia serious siasa za Tanzania na wanasiasa kwa ujumla.
 
Ukimwi unauwa kama corona? Nina ndugu zangu wana ukimwi ila huwezi kuwajua na wana miaka kibao toka wapate huo ukimwi halafu wewe mzee unakuja kufananisha na corona kweli?

Watu kibao wanakufa kwa ukimwi, lakini hawathubutu kusema maana ni kama ugonjwa wa aibu. Halafu hoja yako hapa ni nini? Maana yote ni magonjwa ya kuambukiza.
 
Ili ufuzu ukamanda ni lazima uwe unamudu kutukana na kuzusha

Back
Top Bottom