Pole rafiki yangu Ruth kwa msiba mlioupata

Mary Chuwa

Senior Member
Feb 24, 2011
177
40
Najua ni kipindi kigumu lakini kwa Uwezo wa Mungu mtayaweza yote.
Haikuniingia kirahisi akilini na moyoni,pindi nilipopata taarifa za msiba wa Kaka Mbogo.
Niliumia nilipokuja nyumbani na kumuona Merylin,Ebenezer na Ian kuwa baba yao Godwin a.k.a Mbogo hayupo tena.
Nimejifunza mengi sana toka kwake ni kaka ambaye alikuwa na moyo wa uthubutu na utoaji.
Mungu amlinde mjane Margreth na kumpa moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
Muwe pamoja naye kwa upendo,mkimsaidia ili kuhakikisha alivyoanzisha Mbogo pamoja na Mallya vinaendelea kustawi
Nawapa pole sana kwa msiba mlioupata.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Libarikiwe.
 
Huna simu yake?
 
Mary Chuwa;Kuna ubaya nikitumia forum hii kumpa pole Rev Masanilo?Ni mbaya! ni sawa na kum-beep akupigie useme pole!
The way ulivyoleta mada hii ni msiba na pengine maongezi yenu wawili. We dare to go deep! Kuna akina mbogo tunawafahamu and one moment in time we do move as a block. So in such shocking news u need to be very clear. R. I. P mbogo.
 
kwakweli this kind of message hazifai (sisemi kwa nia mbaya)... ni bora hata ungeleta hapa kama tarifa ya msiba kuliko ulivyoiweka, ni kama unataka kumwambia mfiwa na wengine wote kwamba uliweza kwenda msibani hivyo wasiulize kama ulikuwepo au la
 
na sisi wengine tunajiuliza hao ni akina nani?
na kama ni member hapa wanatumia user name zipi?
mnatuchanganya
 
Yawezekana Ruth ni member humu...lkn ingekuwa poa kama angetumia jina lake la JF...

RIP Godwin aka Mbogo... nadhani ni ule msiba ambao Mh.Mbunge Lema anadaiwa "KUCHAFUA HALI YA HEWA!!!"...
 
Kuna ubaya nikitumia forum hii kumpa pole Rev Masanilo?
ni member huku jf? kila mtu akiweka post kama hii server si itaanguka? au unataka ulimwengu mzima ujue Ruth alifiwa? sina nia mbaya kuhusu msiba wa Mbogo (RIP) lakini wakati tunabandika thread tufikirie kwanza sio kukurupuka
 
Ujumbe wa mtu mmoja ila unawekwa hadharani usomwe na mamilioni na yawezekana mlengwa asiwe memba wa hili jamvi.
kama una mpenda sana na ujumbe huu lazima upitie JF basi atleast ungem PM.
 
Nawashukuru sana kwa ushauri mlionipa,maana JF. ni mahali pia kwa kujifunza,sikuwa na nia ya kumkwaza mtu yeyote.
Samahani kwa wote waliokwazika na ujumbe niliouweka hapa na response zenu zimekuwa somo kwangu wa kwanza ukiwa Rev Masanilo.
Aksanteni Mbarikiwe sana na Amani Iwe mioyoni Mwenu pia.
 
kwakweli this kind of message hazifai (sisemi kwa nia mbaya)... ni bora hata ungeleta hapa kama tarifa ya msiba kuliko ulivyoiweka, ni kama unataka kumwambia mfiwa na wengine wote kwamba uliweza kwenda msibani hivyo wasiulize kama ulikuwepo au la

u made my day....
 
sifa za kijinga...anajifanya mpole n huruma kwa wafiwa........nenda msibani na sio kuandiaka humu
 
sifa za kijinga...anajifanya mpole n huruma kwa wafiwa........nenda msibani na sio kuandiaka humu

Hahahahahahaha TOSA boy! Kwa kweli mijitu ya namna hii hata rambi rambi hakuna wanaosha vinywa JF
 
Back
Top Bottom