Pole Lissu, unavuna ulichopanda?

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Habari wanajf, kama kawaida kuwetea kinachojiri,

Mimi ni Mwanachadema na kamanda mwerevu, kumbuka wapo baadhi ambao wao ndio walipelekea makamanda wote tuitwe nyumbu. Lakini ukweli ni kwamba tupo ambao sio nyumbu.

Mara kadhaa wanachadema ambao wana busara na weledi walishauri lissu afungwe spidi gavana, aache kutoa matamko ya chama bila ridhaa ya chama.

Jana Lissu akiwa kwenye interview alisema Chadema hawataingia bungeni wala kushirikiana na serikali kuanzia serikali kuu hadi za mitaa. Hayajapita masaa 24, leo tunashuhudia Wabunge wa viti maalum akiwepo Mwenyekiti Bawacha anaapa.

Hapa tafsiri yake ni kuwa Lissu hana taarifa zozote za chama na pengine hana mawasiliano na wenzake kwa kuwa kama angelijua linatokea leo basi jana asingeweza kutoa lile tamko. Tamko alibidi alitoe baada ya hawa wabunge kuapa.

Ni kuwa lissu hana watu wa intelijensia?

Pole sana Lissu, umeona ni jinsi gani hueshimiki ndani ya chama, kwa maana kama wangekuwa wanakuheshimu, basi misimamo yako wangeifuata sio tu kama lissu basi kama makamu mwenyekiti.

Lissu bado narudia kuangalia ile press yako ya jana nabaki kusema utavuna ulichopanda na ndio maana hata ukashindwa kuwaingiza watu barabarani.
 
Vyama vya upinzani vinazidi kupitwa na wakati Soon they will be irrelevant! Wengine tulishaona miaka mingi iliyopita na nilisema wakati movement ilipoanza. Ndo narudia Wenye Nchi Wananchi ukinielewa vyama vyote vitakuwa havina relevance!
 
20201124_163110.jpg

Huyu ni Lissu? au tuseme na Katibu Mkuu hana taarifa? haaa haaa
 
Mbona yeye alikuwa wakwanza kuchapa lapa
Watoto wa mujini wanasema ngoma droo
Alieuza dhahabu feki kapewa noti bandia
Ukweli hapa hasara kwa aliye haribu uchaguzi
Kibano cha beberu kipo palepale
 
Hii nimeipenda
Mbona yeye alikuwa wakwanza kuchapa lapa
Watoto wa mujini wanasema ngoma droo
Alieuza dhahabu feki kapewa noti bandia
Ukweli hapa hasara kwa aliye haribu uchaguzi
Kibano cha beberu kipo palepale
 
Hapa tatizo sio lisu tatizo ni chadema waliokubali kumpitisha lisu kugombea urais wakidhani kura zinapigwa na wabelgiji na wajerumani sasa hapa kina halima tayari wamemwaga ugari tunasubiri kina lisu wao wamwage mboga kama wataweza
 
Jamani nadhani walifanya maamuzi mapya na machungu lakini kwa kufanyeje kwani hakuna aliye halali pale bungeni wacha waingie hawa walio halali watuwakilishe kwani hao wengine hatuna uhakika ni nani alishinda na nani hakushinda tulio na hakika nao ni hawa wa Chadema kwani wameingia kwa kuwa kwa bahati nzuri ama mbaya waliruhusiwa kupata kura walizopata! Amen! Wenye aibu ni wezi siyo Chadema!
 
Vyama vya upinzani vinazidi kupitwa na wakati Soon they will be irrelevant! Wengine tulishaona miaka mingi iliyopita na nilisema wakati movement ilipoanza
Ndo narudia Wenye Nchi Wananchi ukinielewa vyama vyote vitakuwa havina relevance!
Wabadilishe aina ya siasa wapinzani kutoka za mapambano kwenda siasa za tija. Wataeleweka.
 
Back
Top Bottom