Pochi la Rais Samia kujenga zahanati kila kijiji

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
46
125
POCHI LA MAMA KUJENGA ZAHANATI KILA KIJIJI:

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anakusudia kujenga zahanati kila kijiji Nchi nzima ili kuongeza huduma za Afya jirani na wananchi Zaidi.

Akizungumza Kwenye kikao cha Ndani kilichowakutanisha wakuuu wa Idara na Baraza la madiwani Wa Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Waziri Ummy amewataka madiwani wawahakikishie wananchi wao Kupitia mikutano ya Hadhara kwamba serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Samia inayo dhamira ya dhati ya kuondoa changamoto za huduma za Jamii ikiwemo Afya, Elimu na Barabara

"Nataka niwahakikishie ndugu zangu madiwani, Rais Samia amekusudia kujenga zahanati Kwenye kila kijiji Nchini na kama alivyosema yeye ni mtu wa matendo Zaidi kuliko maneno hivyo Nendeni mkawaambie wananchi Kwenye mikutano ya Hadhara dhamira hii njema ya Rais wetu" alisema Ummy Mwalimu

Waziri Ummy anaendelea na ziara za kukagua Utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo Chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Kwenye Halmashauri mbalimbali Nchini.​

IMG_20210926_150244_595.jpg
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,128
2,000
Siasa nchi za Kusini wa Jangwa la Sahara raha sana
Kwahiyo hata kijiji kikawa na zahanati 3 itaongezwa nyingine iwe ya nne au zitajengwa vijiji visivyo na zahanati??
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,667
2,000
Yaani hela zetu tunazo ibiwa kupitia tozo kandamizi ndiyo zimegeuka kuwa POCHI LA MAMA!! Unapata mpaka ujasiri wa kuanzisha kabisa na uzi!!

Young boy/ girl, please!! be serious!!!
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,207
2,000
Natamani Chif Hangaya akemee unafiki huu. Mwendazake alipenda kutukuzwa na kuabudiwa.
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,696
2,000
pochi yake!! pesa yake au kodi zetu?
Sawa, isiwe kesi; mi naona mambo mengine ni madogo tu. Hebu sasa tuseme ni pesa alizoacha mwenzake ndo zinajenga hizo zahanati.

Maana theme hapo ni upatikanaji wa huduma ya afya tu basi, hayo mengine ni utashi tu wa watu. Basi tuseme hivyo na tuache kugombana bila sababu! Au mnasemaje wadau?
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
35,653
2,000
Sawa, isiwe kesi; mi naona mambo mengine ni madogo tu. Hebu sasa tuseme ni pesa alizoacha mwenzake ndo zinajenga hizo zahanati. Maana theme hapo ni upatikanaji wa huduma ya afya tu basi, hayo mengine ni utashi tu wa watu. Basi tuseme hivyo na tuache kugombana bila sababu! Au mnasemaje wadau?
kuabudu mtu ni mambo madogo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom