Wanabodi,
Nimeisikiliza Press Conference ya Mwenezi wa Chadema, Brenda Rupia. Amemuita Mwenezi wa CCM, Kenan Kikaragosi badala ya Kenan Kihongosi, nikaona kauli hiyo inatakiwa kufanyiwa PNA.
Kwanza msikilize Brenda
View: https://youtu.be/lscfiTCe69o
Kwa sisi waandishi wa habari wa broadcast journalism, tukimsikiliza mzungumzaji ambaye amekosea kwa bahati mbaya kulitamka jina la mtu, kwa bahati mbaya utajua, na yule ambaye anakosea jina la mtu kwa makusudi ili kumtamka vibaya utamjua.
Mfano yule aliyemtamka mtu Samuya, au ile ya Mhe. Mungu, hapo ni bahati mbaya ya kweli ya kuleleza ulimi, na hawa wanaomuita Samuya kwa makusudi, tunawajua.
Brenda amemuita Kenan Kikaragosi, makusudically na kujifanya amekosea!.
Kitendo cha Mwenezi wa Chadema kumuita mwenezi wa CCM Kenan Kikaragosi, sio cha kunyamaziwa!, hii sio lugha ya kiungwana. Juzi kati kiongozi mmoja mkubwa tuu, ameitwa Yuda Bungeni na Bunge lote kimya bila mbunge yeyote kupinga hiyo hilo jina la Yuda, liko kwenye hansard za Bunge!.
Brenda amefanya makusudi kwasababu kwanza alilianza kwa kulitamka hilo jina vizuri tuu "Kenan Kiong", akakatisha na kusema "Kikaragosi", ili kujifanya ni amekosea kwa bahati mbaya akasema "Sorry", Kiong kisha akajifanya hamjui anaitwa nani, "Sijui, anaituwaje?. Hivi ni kweli Brenda ni wa kutojua mwenezi wa CCM anaitwa nani?. Mtu anaweza asielewe majina ya waenezi wa vyama vingine vyote, lakini sio CCM!.
Kuna mwandishi akamtajia kisha yeye kusema "huyo huyo!"
"Nilikuwa nimejanda kujibu na kumzungumzia lakini badae nikaona kwamba hafai kumpa muda wala, muda wetu wachama ni very precious kumzungumzia Kiongosi". Mbona hapo mwisho amelitaja hilo jina lake vizuri tuu!. Nawashauri viongozi wa vyama vyote kuheshimiana.
Ila pia naitaka serikali yetu, Msajili wa Vyama vya Siasa, na jeshi letu la polisi, kiongozi wa chama chochote akitoa matamshi hatarishi, achukuliwe hatua, na sio viongozi wa upinzani tuu!, mfano neno "tutakinukisha" sio uhaini ni sedition tuu!, kuna mwenezi wa chama fulani alitoa maneno hatarishi kwelikweli kwa usamala wa taifa, lakini hakuulizwa chochote!, kuna kiongozi alisema watu wanavyopoteza watu, hakuulizwa chochote!.
Vyama vyote ni sawa mbele ya sheria na viongozi wote ni sawa mbele ya sheria.
Tutende haki sawa kwa wote!.
Paskali.
Hakuna dhambi hapo, Bali ni sehemu ya game ya kisiasa na zaidi ya hapo ni "bora anaekutukana in public kuliko anaekupoteza in secrecy "