PLZ, Uncle wangu anahitaji msaada wa kitaalamu.

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,136
Wakuu salaam!
Kuna uncle wangu anateseka sana kwa ugonjwa ambao kimsingi haujafahamika kwa familia. Hata hivyo, baada ya mimi mwenyewe kufuatilia kwa karibu nikagundua kuna ugonjwa unaoitwa HALLUCINATION ambao unalandana sana na matatizo yanayomkuta uncle wangu!!! Kimsingi, mara nyingi uncle wangu wakati mmekaa mnapigwa story, utakuta anakuambia kuna mtu kamsikia akisema jambo fulani, ambalo mara nyingi huwa linasemwa dhidi yake! Si hivyo tu, wakati mwingine atavunja maongezi na kusema kuna mtu wakati kiukweli kunakuwa hamna mtu yeyote wala sauti yoyote! Hii ni kwamba huwa anasikia na kuona vitu ambavyo havi-exist! Baada ya kufuatilia sana, ndipo nikagundua huo ugonjwa uitwao HALLUCINATION!!!! So, wataalamu wenye uelewa kuhusu huu ugonjwa naomba wanifafanulie vizuri kuhusu ugonjwa huu! Aidha, ningependa kuifahamu endapo kuna tiba na tiba yake(including) gharama zake zinaweza kuwa vipi!!!

PLZ, help manake uncle wangu anataabika sana kiasi cha wakati mwingine kuharibu personality yake kv anaweza kukaa na mtu na kumshutumu kwamba kamsema vibaya wakati sio!!!
 
NasDaz pole kwa tatizo hilo la mjomba wako,

Ninavyofahamu mimi hallucinations si ugonjwa ila ni dalili ya magonjwa mengine. Magonjwa haya yanaathri utendaji kazi wa kufikiri na utambuzi na kumfanya mtu afikiri au atambue vitu ambavyo kiuhalisia havipo.

Hallucinations ziko za aina nyingi, zipo za kusikia vitu ambavyo havipo (auditory hallucinations), kuona vitu ambavyo havipo (visual hallucinations), kunusa harufu isiyokuwepo (olfactory), lakini saa nyingine hata kuhisi kama unaguswa (tactile hallucinations). Huyu mjomba wako anaonekana ana auditory na visual hallucinations.

Kama nilivyosema, hallucination ni dalili ya magonjwa mbalimbali, baadhi ya magonjwa hayo ni haya yafuatayo:
1. ugonjwa wa akili uitwao schizophrenia
2.ugonjwa wa akili uitwao depression (kushuka moyo)
3.wagonjwa wa kifafa (epilepsy) ambao kifafa chao kinaanzia kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa temporal lobe (hawa wanakuwa na olfactory hallucinations).
4. wazee sana huwa chembe hai zao za ubongo zinapungua size (atrophy) hivyo wanapata dementia ambayo pia inaweza kusababisha hallucinations.
5. utumiaji wa dawa za kulevya kama bangi, cocaine zinaweza kusababisha hallucinations.
6. Homa kali hasa kwa watoto pia husababisha hallucinations (utasikia watu wanasema mtoto anaweweseka), nk.

Mgonjwa wako ana tatizo ambalo anahitaji kuonana na madaktari bingwa wa magonjwa ya akili (psychiatrists - Kama Prof Kilonzo wa Muhimbili) wataweza kujua ni ugonjwa gani unamsababishia hizo hallucinations na najua watamsaidia.
 
Pole sana NasDaz kwa mjomba.....'Hallucination' (kuweweseka) sio ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Hallucinations zinaweza kuwa visual (kuona vitu visivyokuwepo) au auditory (kusikia vitu visivyokuwepo), kwa lugha rahisi vitu vya kufikirika lakini havijatokea kweli. Na zinaweza kusababishwa na vitu vingi tu commonly 'substance abuse' kama bangi, madawa ya kulevya, etc. Lakini pia inaweza ikawa kutokana na msongo wa mawazo (stress) na/au depression, au baada ya tukio fulani kubwa la kimaisha kama ajali/msiba etc (post-traumatic disorders), na matatizo mengine ya akili.

Magonjwa kama uvimbe kwenye ubongo, kuvilia damu kwenye ubongo baada ya ajali au kiharusi (stroke) navyo huweza kujionyesha kwa hallucination.

Tukirudi kwa mjomba yako:
Sidhani kama anachopata yeye ni 'hallucination', bali ni kitu kingine kinachifanana na hallucination...kinaitwa 'Delusion'! Delusion nazo nin dalili mara nyingi za magonjwa ya akili (hasa ugonjwa unaitwa Schizophrenia) ambapo mgonjwa anaamini na anaona/kusikia (kama ilivyo kwa hallucinations) kuwa kuna watu wanamuambia vitu fulani, au wanamtuma vitu fulani...na inapotokea anaamini/kuona/kusikia kuwa kuna watu wanamsema, au wana nia mbaya naye, wanataka kumdhuru, anakuwa haamini watu kwa sababu ya kuwahisi hawana nia naye njema..hiyo hali inaitwa 'Paranoid Schizophrenia' (sina hakika lakini kwa dalili chache ulizosema inaelekea huko).

Kama uncle yuko Dar, mpelekeni Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili kwa uchunguzi zaidi...challenge ni kuwa, waginjwa wa Paranoid Schizophrenia unapotaka kuwasaidia hasa kuwa kuwapeleka hospitali, we ndio anakuona mbaya!
 
THANKS mkuu kwa maelezo yako ambayo ni very helpful for one step foward!! am afraid No.1 OR No.2 inaweza kuwa sababu!!
 
Pole sana Mpwa, sina cha kuongeza ila yaliyosemwa hapo juu ni muhimu, pole sana na MUNGU akutie nguvu for caring
 
Pole sana NasDaz kwa mjomba.....'Hallucination' (kuweweseka) sio ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Hallucinations zinaweza kuwa visual (kuona vitu visivyokuwepo) au auditory (kusikia vitu visivyokuwepo), kwa lugha rahisi vitu vya kufikirika lakini havijatokea kweli. Na zinaweza kusababishwa na vitu vingi tu commonly 'substance abuse' kama bangi, madawa ya kulevya, etc. Lakini pia inaweza ikawa kutokana na msongo wa mawazo (stress) na/au depression, au baada ya tukio fulani kubwa la kimaisha kama ajali/msiba etc (post-traumatic disorders), na matatizo mengine ya akili.

Magonjwa kama uvimbe kwenye ubongo, kuvilia damu kwenye ubongo baada ya ajali au kiharusi (stroke) navyo huweza kujionyesha kwa hallucination.

Tukirudi kwa mjomba yako:
Sidhani kama anachopata yeye ni 'hallucination', bali ni kitu kingine kinachifanana na hallucination...kinaitwa 'Delusion'! Delusion nazo nin dalili mara nyingi za magonjwa ya akili (hasa ugonjwa unaitwa Schizophrenia) ambapo mgonjwa anaamini na anaona/kusikia (kama ilivyo kwa hallucinations) kuwa kuna watu wanamuambia vitu fulani, au wanamtuma vitu fulani...na inapotokea anaamini/kuona/kusikia kuwa kuna watu wanamsema, au wana nia mbaya naye, wanataka kumdhuru, anakuwa haamini watu kwa sababu ya kuwahisi hawana nia naye njema..hiyo hali inaitwa 'Paranoid Schizophrenia' (sina hakika lakini kwa dalili chache ulizosema inaelekea huko).

Kama uncle yuko Dar, mpelekeni Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili kwa uchunguzi zaidi...challenge ni kuwa, waginjwa wa Paranoid Schizophrenia unapotaka kuwasaidia hasa kuwa kuwapeleka hospitali, we ndio anakuona mbaya!

ua right mkuu, mi mwenyewe ni kv kichwa maji ndo maana huwa nam-face na kumwambia wht i think abt his problem!! Anakuwa mkali kiasi kwamba hata watu wazima ambao labda wangeweza kuwa na ushawishi wa kumwambia nini afanye huwa wanamuogopa!!!! am seriously very affected by his problem, coz' nam-feel sana huyu uncle wangu ingawaje hata mimi nimewahi kuwa victim wa tatizo lake!!! i'll work with ur advice
 
NasDaz pole sana ndugu yangu. Kwa bahati mbaya huo ugonjwa siufahamu, ila naamini wapo ambao watakupa/wameshakupa maelekezo mazuri. Pole sana mkuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom