Pleese naombeni ushauri kati ya hizi gari ipi ambayo inaweza kunifaa kwendea kazini na kurudi

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
Pleese naombeni ushauri kati ya hizi gari ipi ambayo inaweza kunifaa kwendea kazini na kurudi , utumiaji wake wa mafuta uwe mdogo

1.brevis
2.toyota Alex
3.Altezz
4.Verosa

Nafikiria kununua na si mwenyeji sana katika hilo..ili ninapofanya maamuzi nisijutie kipato changu cha kawaida
 
Unsishi maeneo ya wapi? Namaanisha gari ya chini au ya juu itahitajika? Kuna utelezi siku za mvua kuhitaji gari ya 4wheel drive?

Umbali wa kazini na kwako ukoje ili kujua gharama za mafuta kama zirakua rafiki.

Sijuo kwa vigezo vyako lakini hapo hiyo Alex itakupa uzoefu wa magari ili baadae ufanye maamuzi ya kuchagua kulingana na uzoefu wako.
 
Mi naishi mwanza Kazini kwangu ni umbali wa km Toka ninapokaa 16 ,kwenda ....barabara ni ya vumbi ila iko poa !! , Nikwaajili ya kwendea kazini na kuridi bac...siku za mvua kama kubwa nitakuwa naenda tu na piki piki aina ya boxer ninayo
 
Chukua Toyota Allex hutojutia pesa yako.... Kuiagiza maximum 13M mpaka inaingia brabarani. Inategemea na year of manufacture na mileage
 
Mi naishi mwanza Kazini kwangu ni umbali wa km Toka ninapokaa 16 ,kwenda ....barabara ni ya vumbi ila iko poa !! , Nikwaajili ya kwendea kazini na kuridi bac...siku za mvua kama kubwa nitakuwa naenda tu na piki piki aina ya boxer ninayo
Hapa sijakuelewa kidogo,yaani kwenye mvua unasepa na tukutuku kwenye jua unasepa na gari?
 
Ndio kipindi cha kiangazi ndio napenda sana kuendesha gari ila masika kwa kule ninakofanyia kazi sio rafiki kwa gari inanilazimu nitumie piki piki ninayo .....!!
 
Don tach brevis.
Utaleta uzi humu wa kuuza laki 5.
Kuna boss wangu anayo ni kali Brevis ...ananiambia nimpe milion 5;aniachie ila mafuta sasa !! Ndio itaniua kabisa !! Ndio maana nimeomba ushauri mnishauri nijue nachukua gari ....mwezi nataka nikamilishe
 
Chukua Allex kwa kigezo cha fuel fuel economy kwa running costs na spare kwa maintanace costs

Sent from my SM-A205F using Tapatalk
 
Pleese naombeni ushauri kati ya hizi gari ipi ambayo inaweza kunifaa kwendea kazini na kurudi , utumiaji wake wa mafuta uwe mdogo

1.brevis
2.toyota Alex
3.Altezz
4.Verosa

Nafikiria kununua na si mwenyeji sana katika hilo..ili ninapofanya maamuzi nisijutie kipato changu cha kawaida
Utapata ushauri mzuri kama ungeeleza ulipo na unapofanyia kazi.

Sehemu zingine huna haja ya kuwa na usafiri binafsi na zingine utahitaji hardtop badala ya hivyo vingulinyunguli ulivyoviorodhesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom