please watanzania, tumusaidie huyu ndugu yetu

Prof

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,578
2,410
ndugu wana jamii, kwa masikitiko makubwa naomba nifikishe dira ya mnyonge mbele zenu ili kwa yule ambaye angependa kumusaidia ndugu yetu huyu amusaidie. ni dira ya mnyonge kipindi kinachorushwa hewani na star TV. ambapo kijana ambaye amejitambulisha kwa jina la Romana Charles alipoteza miguu yake yote miwili katika ajali ya Treni akitokea Dodoma kuelekea Dar es salaam mwaka ambao aliutaja lakini sikuweza kusikia vizuri.

Nikinukuu simulizi yake kama alivyokuwa anahojiwa na mtangazaji wa TV, anasema " hakubahatika kupata elimu ya secondary, hivyo basi aliishia darasa la saba kwani familia yake ilikuwa masikini sana. Mungu alimujalia kipaji cha kucheza mpira kwani kabla ya kumaliza hata dar asa la saba aliweza kuchezea timu za ngazi ya mkoa, alizitaja timu kama Mirambo na timu ya idara ya Maji ya Dodoma ambazo aliwahi kuchezea enzi hizo akiwa na miguu yake yote miwili. kwa kuwa familia ilikuwa masikini aliwekeza nguvu katika soccer ili aje kucheza timu kubwa na arudi kuwasaidia wazazi wake ambao ni masikini sana. bahati mbaya akiwa safarini kuelekea DSM alipata ajali ya Treni na kukatwa miguu yake miwili na behewa la Treni. Ndoto ya kucheza mpira ikapotea na kujikuta ikiwa helpless. ndugu yetu huyu anafamilia ya watoto wawili na wanasoma mwalimu nyerere Magomeni. hana kazi/ajira hivyo basi anashinda kuomba watu msaada barabarani karibu na Movenpick ili apate chochote''.


RAI KWA WANA JAMII WENZANGU: tumusaidie huyu ndugu yetu.


KWA HISANI YA STAR TV, naomba niweke namba zake humu kwani hata yeye alizitaja Hewani. endapo nita infringe any right or cause damage to anyone, it remain not my intention. am trying to pass the pain of our brother to all Tanzanians wherever they are. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

ANAITWA ROMANA CHARLES(0717968954)

ANAJITAFUTIA RIZIKI(kuomba) MITAA YA MOVENPICK OPPOSITE YA BACKLAYS.

Wana jamii kwa maelezo zaidi munaweza kum-contact mtangazaji wa kipindi cha dira ya mnyonge cha star TV anaitwa kama sikosei MAGRETH TENGULE.


Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom