Please Wana jukwaa, kwenye tasnia ya kutongoza, nashauri turudishe mifumo yetu ya zamani!

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
860
1,382
Nawasalimu Asalam aleykum!

Kwakweli inasikitisha sana tasnia ya kutongoza imeharibiwa vibaya mno!

Vijana wa Sasa utongozaji wao ni wa mwendokasi, yaani ni blah blah tu
Maneno machache, "I love you" na mwingine anajibu " I love you too" kazi imekwisha kesho wanaingia mzigoni kunyanduana
Tena mbaya zaidi maneno hayo yanatumwa tu kwa sms ktk simu

Magwiji wetu wa utongozaji waliweka mfumo imara wa utongozaji

Kwanza kutongoza kulikuwa na muda rasmi, yaani mchana Hadi magharibi, ili kuwapa fursa watoto wa kike kuwepo nyumbani asubuhi yote, jioni yote na usiku wote, si Kama Sasa kutongoza ni muda wowote!

Pili ulikuwa ni utaratibu kutongoza lazima iwe ni Sanaa iliyobeba maneno mengi yenye kuvutia, na ni maneno yenye yakumvuta binti toka mbali

Hii ilisababisha utongozaji kuwa ni Jambo lenye kuvutia Sana na kumfanya binti ashindwe kulala usingizi kwa ajili ya msisimko
Tukashuhudia misemo, nahau na methali mbalimbali zinatungwa ili kuboresha tasnia hii ya utongozaji
Misemo Kama vile, "usiku silali nakuwaza wewe!, au "nimekufa juu yako, au nikinywa maji nakuona wewe! na misemo mingine mingi

Hapa ndipo tulishuhudia binti anauma Uma vidole, kuchorachora chini, na kunesa kichwa na mabega kwa madaha, wakati kidume kinamwaga maneno, mikono mfukoni na huko ndani jogoo kasimama

Pia ilikuwa ni utaratibu kuwa kutongoza si Jambo la siku moja, lazima ukutane na binti Mara tatu au zaidi katika kumweka sawa,
Hapa binti alikuwa anaimarisha tasnia ya utongozaji kwa kutoa majibu ya kukatisha tamaa, Kama "Mimi sitaki" au,"namuogopa baba" au "Mimi mdogo siwezi"

Siku zote bidhaa Bora Ina gharama!

Kwa kweli utaratibu wa utongozaji huu ambao umeachwa na vijana wa Sasa umetuletea ndoa imara sisi vijana wa zamani, si Kama Sasa mahusiano kutongoza kwa "I love you" hayadumu

Harakaharaka Haina baraka

Naomba niwashauri vijana wa Sasa kaeni chini mutafakari!
Oneni umuhimu wa kurudisha Tena mfumo wa kutongoza Kama zamani
Ni mfumo mzuri wenye staha, Ila ohoo moyo unadunda vibaya mnoo
Hapo ndipo ilibidi kijana ukae ndani kufanya mazoezi ya kumwaga neno Kama wasanii wa hip-hop!
Aisee ilikuwa inapendeza

Ya kale ni dhahabu!!
 
With this generations we should accept changes.

Yani vile maisha yanatukeep bize nianze kukufatilia six months??

Nianze kutype essay ndeefu....
 
Kama tulitoka kwenye kanda za kaseti, vhs tukaingia kwenye CD na Memory card mara flash, yaani hapo sijakukumbusha santuri, acha tu tubadilike, labda we bado unavitumia mkuu
 
Nawasalimu Asalam aleykum!

Kwakweli inasikitisha sana tasnia ya kutongoza imeharibiwa vibaya mno!

Vijana wa Sasa utongozaji wao ni wa mwendokasi, yaani ni blah blah tu
Maneno machache, "I love you" na mwingine anajibu " I love you too" kazi imekwisha kesho wanaingia mzigoni kunyanduana
Tena mbaya zaidi maneno hayo yanatumwa tu kwa sms ktk simu

Magwiji wetu wa utongozaji waliweka mfumo imara wa utongozaji

Kwanza kutongoza kulikuwa na muda rasmi, yaani mchana Hadi magharibi, ili kuwapa fursa watoto wa kike kuwepo nyumbani asubuhi yote, jioni yote na usiku wote, si Kama Sasa kutongoza ni muda wowote!

Pili ulikuwa ni utaratibu kutongoza lazima iwe ni Sanaa iliyobeba maneno mengi yenye kuvutia, na ni maneno yenye yakumvuta binti toka mbali

Hii ilisababisha utongozaji kuwa ni Jambo lenye kuvutia Sana na kumfanya binti ashindwe kulala usingizi kwa ajili ya msisimko
Tukashuhudia misemo, nahau na methali mbalimbali zinatungwa ili kuboresha tasnia hii ya utongozaji
Misemo Kama vile, "usiku silali nakuwaza wewe!, au "nimekufa juu yako, au nikinywa maji nakuona wewe! na misemo mingine mingi

Hapa ndipo tulishuhudia binti anauma Uma vidole, kuchorachora chini, na kunesa kichwa na mabega kwa madaha, wakati kidume kinamwaga maneno, mikono mfukoni na huko ndani jogoo kasimama

Pia ilikuwa ni utaratibu kuwa kutongoza si Jambo la siku moja, lazima ukutane na binti Mara tatu au zaidi katika kumweka sawa,
Hapa binti alikuwa anaimarisha tasnia ya utongozaji kwa kutoa majibu ya kukatisha tamaa, Kama "Mimi sitaki" au,"namuogopa baba" au "Mimi mdogo siwezi"

Siku zote bidhaa Bora Ina gharama!

Kwa kweli utaratibu wa utongozaji huu ambao umeachwa na vijana wa Sasa umetuletea ndoa imara sisi vijana wa zamani, si Kama Sasa mahusiano kutongoza kwa "I love you" hayadumu

Harakaharaka Haina baraka

Naomba niwashauri vijana wa Sasa kaeni chini mutafakari!
Oneni umuhimu wa kurudisha Tena mfumo wa kutongoza Kama zamani
Ni mfumo mzuri wenye staha, Ila ohoo moyo unadunda vibaya mnoo
Hapo ndipo ilibidi kijana ukae ndani kufanya mazoezi ya kumwaga neno Kama wasanii wa hip-hop!
Aisee ilikuwa inapendeza

Ya kale ni dhahabu!!
Siku hizi ni Tigopesa Na Mpesa
 
Sahivi tunatongozana kwa mifumo ya TEHAMA kwahiyo lazima Mambo yawe mafupii hakuna kufikiriana tena
 
Back
Top Bottom