Platform ya kuuza na kununua muziki wasafidotcom tayari kwa matumizi

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,941
2,042
Kupitia ukurasa wake wa instagram,Diamond platnumz ameweka wazi kua plaform yake ya kuuza na kununulia kazi za wasanii iitwayo,wasafidotcom ipo tayari kwa matumizi pande zote yaani wasanii (wauzaji) na mashabiki (wanunuzi).

Aliongeza kua plaform hio si kwaajili ya wasanii wa WCB tu bali ni kwaajili ya wasanii wote ndani na nje ya Tanzania!.
Pia aliandika,wazo la kuanzisha platform hio (wasafidotcom) ni baada ya kuona wasanii wanaekeza kwa kiasi kikubwa na wanapata kidogo kwa 7b alioleza kua wanadhulumiwa!.

Alihitimisha kwa kuandika wimbo wa harmonize mpya unaotarajia kutoka kesho kwa mara ya kwanza utapatikana kwenye platform io tu,Nimepita nimekuta gharama ni shilingi 300 tu kwa nyimbo moja!..Pia aliomba ushirikiano kutoka kwa wadau yaani mashabiki.

Pita hapa www.wasafi.com kuitazama.
Tuache ushabiki,Huyu jamaa anajua sana.
[HASHTAG]#BongoFlevaToTheWorld[/HASHTAG]
 
Huyu jamaa atadumu sana kwenye game, anafikiri positive na international zaidi. Hapo kila msanii anaetaka maendeleo ataingiza ngoma zake na pengine itakuja kua trending site ya music kwa Africa... kuna wakati nafikiri wanaomchukia wanajitafutia maradhi ya bure.. Bora uwe upande wake tu kuepusha balaa. Hongera sana Diamond.
 
Huyu si alisema alilipwa Bilioni 2.2 na Universal Music alafu akalipa Kodi Milioni 35 ili nyimbo zao za Wcb waziuze wao?!

Imekuaje tena mbona wanauza wenyewe tena?!
Diamond akili nyingi kusaini universal music hakumbani yeye kutumia platform yake kutengeneza pesa hasa huku East Africa
Na aje ya kibakuli inapatikana kwa 30000 maana ni mziki watofauti a.k.a mziki mzuri
 
Kwa habari kamili tembelea hapa
[/https://mushkhani.wordpress.com] [URL]
Diamond katangaza njia mpya ya kupata nyimbo za WCB kama inavyoonesha picha hapo chini

Screenshot_20170309-152328.png
 
Huyu si alisema alilipwa Bilioni 2.2 na Universal Music alafu akalipa Kodi Milioni 35 ili nyimbo zao za Wcb waziuze wao?!

Imekuaje tena mbona wanauza wenyewe tena?!
Mzaramo acha kuwa mvivu wa kufikilia!.Hii inaitwa self-investment haihusiani hata kidogo na universal.Mfano mdogo ni kibakuli mbona yupo sonz na bado anatumia mkito ku-push kazi yake.Labda hujaelewa,io platform(wasafidotcom) haisambazi kazi za WCB tu bali wasanii wote Tanzania na nje ya mipaka ya tanzania kwaivo jamaa anaeza akaitumia kusambaza kazi za wengine sio lazima zake tu.Kumbuka he is worldwide known huoni fursa kwa wasanii wengine kua international kupitia hii wasafidotcom.
 
Wimbo mmoja wa kibakuli ni album nne za domo kwa hiyo lazima bei iwe juu mara dufu.usishangae kijana
Huu ushabiki muwe mnauweka pembeni kwenye vitu vya msingi kama hivi!.Anyways,ukitaka kujua nani ana mauzo mengi mtandaoni,Kama unafuatilia utakua unafahamu kwamba [HASHTAG]#MarryYou[/HASHTAG] ilikua kwenye list ya vevo ya nyimbo 20 zilizotazamwa sana marekani kati ya wiki juzi na wiki jana!.swali,Kama kiba ni bora mbona hajatokea kwenyee hii list ilhali na yeye yupo vevo.
Anyways,mimi sio team member wa popote!.Uo ulikua mtazamo wangu tu.
 
Back
Top Bottom