Platform waliyotengeza CCM ni ngumu kuja kuwatoa madarakani labda wenyewe waamue tu kung'atuka

Hivi unaanzaje kuwasifia CCM, wakati inajulikana wazi kuwa wanatumia nguvu ya chama dola, kuvuruga misingi yote ya kidemokrasia iliyo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa nchi ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Hebu nikuulize swali dogo tu mleta post, hivi ukiutazama uchagizi wa serikali za mitaa namna ulivyoendeshwa, hivi unaupataje ujasiri wa kuisifu CCM kwa ushindi wa kishindo walioupata wa zaidi ya asimia 99.9??

Hivi unaweza kumdanganya hata mtoto mdogo anayesoma chekechea, kuwa nchi hii inaendeshwa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi na akakukubalia??
[Kwan aliyewazima sumaye, zitto, wangwe, cecil mwambe kutogombea uenyekiti ni dola mbona unakuwa msahaulifu sana
 
Ukiangalia muundo wa Chama cha Mapinduzi ulivyo kuanzia chini kwenye shina hadi Taifa utaona kuwa hawa jamaa wapo well organised na wanajua wanachofanya na kukitafuta tofauti na vyama vingine vya siasa.

Ukianzia namna mchakato wa kuwapa viongozi wao wa shina, kata hadi taifa utaona ni wa wazi unatoa mwanya wa kila mtu kuweza kuwa kiongozi kama tu atajipanga vizuri tofauti na wengine wanavyotafuta wagombea wao ni mchakato unaendeshwa kiajabu ajabu na vingen wana viongoz wa kudumu.

Angalia namna ya kuwapata viongozi wao wa jumuiya mbalimbali kama ile ya kina mama, vijana, wazazi na wazee na fananisha vyama vingine vya upinzani vinavyowapata viongozi wao ni kichekesho kitupu, jumuiya zao zina viongozi wa kudumu utasikia tano nyingine tuvushe.

CCM ina wanachama kuanzia chini kabisa huko vijijini ambako vyama vingine havijulikani na vinajiandaa kushika dola sijui dola ipi hiyo kuna baadhi ya vijiji mpaka leo wanajua chama cha TANU na CCM na kiongozi ni Nyerere na CCM yake tu hata vyama vya upinzani vimeshindwa kuweka wagombea huko wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji.

Wa kuitoa CCM madarakani bado hajazaliwa labda baada ya miongo kadhaa kupita.
ccm hawawekwi madarakani na muundo wao unless kama unataka kusema police,TISS na Tume ya uchaguzi nayo ni mashina na matawi ya ccm hapo nitakuelewa
 
Vyama vya upinzani vinasumbuliwa na dola na sio CCM ,CCM imeshakufa muda mrefu kilichopo ni dola ndio imebaki.inawabeba.

Uchaguzi ukiwa huru na haki,Polisi, Jeshi na Usalama wakaamua wakae pembeni wakisubiri mshindi ndiye wafanye nae kazi CCM itashindwa kwabla jua halijazama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uimara wa ccm upo mgongoni mwa vyombo vya dola,gazeti likipromote upinzani linafungiwa,gazeti lilitukana upinzani linapewa ba fedha ili lichapwe kila siku hata kama halina wateja.

Rejea Jamvi la Habari na Vijarida vya Musiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unaanzaje kuwasifia CCM, wakati inajulikana wazi kuwa wanatumia nguvu ya chama dola, kuvuruga misingi yote ya kidemokrasia iliyo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa nchi ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Hebu nikuulize swali dogo tu mleta post, hivi ukiutazama uchagizi wa serikali za mitaa namna ulivyoendeshwa, hivi unaupataje ujasiri wa kuisifu CCM kwa ushindi wa kishindo walioupata wa zaidi ya asimia 99.9??

Hivi unaweza kumdanganya hata mtoto mdogo anayesoma chekechea, kuwa nchi hii inaendeshwa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi na akakukubalia??
Mhh mlijitoa ? Kwa hiyo ulitaka iweje ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia muundo wa Chama cha Mapinduzi ulivyo kuanzia chini kwenye shina hadi Taifa utaona kuwa hawa jamaa wapo well organised na wanajua wanachofanya na kukitafuta tofauti na vyama vingine vya siasa.

Ukianzia namna mchakato wa kuwapa viongozi wao wa shina, kata hadi taifa utaona ni wa wazi unatoa mwanya wa kila mtu kuweza kuwa kiongozi kama tu atajipanga vizuri tofauti na wengine wanavyotafuta wagombea wao ni mchakato unaendeshwa kiajabu ajabu na vingen wana viongoz wa kudumu.

Angalia namna ya kuwapata viongozi wao wa jumuiya mbalimbali kama ile ya kina mama, vijana, wazazi na wazee na fananisha vyama vingine vya upinzani vinavyowapata viongozi wao ni kichekesho kitupu, jumuiya zao zina viongozi wa kudumu utasikia tano nyingine tuvushe.

CCM ina wanachama kuanzia chini kabisa huko vijijini ambako vyama vingine havijulikani na vinajiandaa kushika dola sijui dola ipi hiyo kuna baadhi ya vijiji mpaka leo wanajua chama cha TANU na CCM na kiongozi ni Nyerere na CCM yake tu hata vyama vya upinzani vimeshindwa kuweka wagombea huko wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji.

Wa kuitoa CCM madarakani bado hajazaliwa labda baada ya miongo kadhaa kupita.

Halafu umeanzisha uzi kabisa kisha unasifia ccm ni chama imara, huku ukionyesha kuwa bado kuna watu wanajua TANU na Nyerere bado ni kiongozi! Sasa hapo unajisifia uimara au unajosifia kuwa madarakani kwakuwa unaoongoza wajinga?
 
Ccm Zanzibar ilishindwa ikadai imeibiwa kura ikafuta uchaguzi,ikaitisha tena ikajitangaza,halafu umekula fedha za rushwa unakuja hapa kubwabwaja kwamba wamejipanga.

Umesahau kama juzi wameogopa uchaguzi wa serikali za mitaa? Hivi wangekuwa wapo Organise na wanauhakika watashinda wangeogopa kushindana na vyama unavyoviita dhaifu?

Uimara wa CCM upo kwenye uvunjaji wa taratibu na kutumia state aparatus kuwatisha wapinzani,ndio.maana leo kila kona kuna mikutano ya CCM huku wapinzani wakidhibitiwa na polisi wasifanye mikutano,halafu bila aibu unakuja hapa jukwaani kujimwambafai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia muundo wa Chama cha Mapinduzi ulivyo kuanzia chini kwenye shina hadi Taifa utaona kuwa hawa jamaa wapo well organised na wanajua wanachofanya na kukitafuta tofauti na vyama vingine vya siasa.
Sijui kama huko chini ya mada yako uliongelea 'kura za polisi, wasimamizi wa chaguzi, tume isiyo huru ya chaguzi, n.k.) katika andiko lako.
Kama umeandika chochote kuhusu hao niliowataja, basi hiyo 'platform' unayoizungumzia hujui maana yake ni nini.

Wangekuwa na hilo li'platform' unaloandika juu yake, wasingehangaika kabisa kulazimisha washinde wao.

Kama una akili za kuelewa, utakuwa umeelewa ninachokwambia hapa.
 
Kama unazungumzia Tanzania Bara sawa lakini kwa Zanzibar CCM ina hali mbaya sana. Kinachoiweka madakarakani ni mtutu wa bunduki tu. Kule wananchi wameamka hawaitaki kabisa CCM sema nguvu za kupambana nao kwa silaha hawana ndo maana inaendelea kutawala ila kama ni kwa kutumia kura 2015 ingekuwa ndio mwisho wa CCM. Pemba ukieka mgombea wa CCM na wa upinzani ukaeka nazi basi nazi itashinda kwa kishindo.
 
CHADEMA MSINGI TUPO KILA KIJIJI.
Kama huamini kwa nini mlikata majina ya wagombea serikali za mtaa??
Kwa maana hiyo CDM ipo kona zote, uliza Manyara tulipata madiwani wangapi kabla ya kuwanunua??
Wananchi watatoa adhabu kwa udhalimu wenu na rushwa zenu.
Nyie jipeni moyo tuu labda mtumie watendaji na Mapolisisiemu maana watu wana usongo wamechoka na dhuluma zenu watawaadhibu tuu tulia uone!!
 
Boss DAT BOY SU Uwezo wako wa kufikiri ni Mdogo mno na sana, 2015 kwa Dar, Upinzani ulichukua Viti vingi, je unata kusema Muundo wa CCM kwa Dar ulikuwa mbovu???
Jibu ni Moja, CCM wanajua kucheza na Akili za Wananchi na WaTanzania.
Siku Wananchi na WaTanzania wakija kuichoka, CCM inafutika kwa sekunde.
Uzuri ni Uvumilivu na Amani kati yetu bado ipo, Pamoja na Changamoto zilizopo bado tuna Uvumilivu na Amani.
Na mimi nazidi kuliombea, Uvumilivu na Amani kwa Wananchi na Viongozi wetu wote.
Kumbuka Vyama siku vyote vitakuja na kupita ila Nchi na Taifa litakuwepo Vizazi na Vizazi mpaka mwisho wa Dunia.
Mifano ni mingi Africa na Dunia wa Vyama Vikongwe, vilikuwepo na vikafa kwenye ramani ya Dunia, Mfano mdogo hapo Kenya tu.

Back
Top Bottom