PK Kibaoni Dispensary ya Tegeta iangaliwe kwa Umakini wa hali ya juu na Mamlaka husika

Blacklist18

Member
Jul 4, 2018
28
148
Wasalaam wakuu.
Pk kibaoni Dispensary imekuwa ikitoa huduma kwa watu waishio maeneo ya Tegeta hadi madale. Pamoja na kutoa huduma (ambalo ni jambo jema) lakini kuna mambo yanafanyika ambayo si haki kwa serikali (kodi), wateja (huduma) na wafanyakazi (masilahi).

1. SERIKALI: Baada ya uongozi wa awamu ya tano kuingia madarakani na kutoa amri kwa wafanyabiashara kuwa na EFD machine, PK dispensary pia walinunua mashine hiyo, lakini pamoja na kuwa nayo kumekuwa na udanganyifu sana kwenye swala la mauzo. Lisiti za EFD hutolewa kwa wagonjwa ambao huomba list tena kwa kulazimisha, tofauti na hivyo wagonjwa wanaandikiwa lisiti za kitabuni. Kinachofanyika baadae, zinatolewa kwenye mashine lisiti za transaction tofauti tofauti za thamani ya mauzo ya 200,000 hadi 250,000 kwa siku wakati ukweli ni kwamba mauzo kwa siku huwa ni kati ya 1,800,000 hadi 3,000,000. Hivy nashauri wahusika wa mapato wafanye uchunguzi pale nina imani watagundua udanganyifu wa hali ya juu.

2. WATEJA (wagonjwa): Pamoja na kuwa wagonjwa wanapata huduma mahali hapo lakini kumekuwa na ukakasi kwenye huduma yenyewe na gharama za huduma. Lakini pia kuna baadhi ya tiba ambazo Dispensary hiyo hupewa bure na manispaa ili ziwafikie walengwa bure kupitia dispensary hiyo, lakini zikifika pale mambo yanakuwa kinyume kabisa. Mafano ni VITENDANISHI na SINDANO YA TETENASI ambapo vyote hutolewa hospitalini hapo kwa gharama ya shilingi elfu tano (5,000) kwa kila kimoja. Huduma hii ilipaswa kuwafikia walengwa bure lakini wanatozwa pesa kwa ukiritimba wa uongozi wa Dispensary hiyo. Hivyo nawasihi wahusika kufatilia pia swala hili ili haki iweze kutendeka.

3. WAFANYAKAZI: Hawa wanafanya kazi kwa uonevu kutoka kwenye uongozi wa Dispensary hiyo, mbaya zaidi amekua akiwadhalilisha wafanyakazi wake hasa wakike pale wanapotaka kujua kuhusu mafao yao au jambo lolote lenye masilahi ya wafanyakazi anakutafutia sababu ya kukufukuza kazi..mfano juzi amewafukuza wadada 3 kwa makosa ya makusudi ili tu asidaiwe na huwa anawafungia ndani anawapiga na kuwatishia bastora,na kuwaandikisha barua za maaelezo kwa nguvu mwisho anakufukuza kama mbwa usiye na thamani,na amekua akijinadi sanaa kama yeye ana pesa kwa hyo sheria ipo kwenye mikono yake,na hata mkuu wa mkoa hawezi mfanya kitu kwa kuwa wote wa wametoka sehemu moja. kingine nikuwa na wafanyakazi wasiokuwa elimu ya fani husika mfano katika vitengo vya pharmac(duka la dawa) yupo dada ambae atoa dawa yeye ni medical record lakini kamgeuza kuwa mtoa dawa tena na koti la kidaktari anavaaa

Lakini pia wafanyakazi wamekuwa wanakatwa pesa kwenye mishahara yao kwa ajiri ya NSSF tangu mwezi March 2016, cha kushangaza ni kwamba wameenda kuangalia mafao yao NSSF wamekuta hakuna pesa yoyote iliyopelekwa tangu wafungue akauti hizo. Hapa naomba wataalam wa sheria msaidie ni njia gani wafanyakazi hawa wafuate ili wapate mafao yao.
Hivyo naomba Wahusika serikalini wafuatilie Dispensary hii ina mambo yanayofanyika pale ambayo si mazuri kwa serikaria na jamii kwa ujumla.

Nawasilisha
IMG-20180705-WA0001.jpg
 
nina mpng wa kufungua hospital halaf nje nauza majeneza na sanda, mnaonaje nitapata wateja?
 
Asilimia kubwa ya Wamiliki wa dispensary huwa wanajitoa akili na wana roho mbaya kwa wafanyakazi wao
 
NawasilishaView attachment 803110
Wewe una roho ya kichawi kabisaaaaaaaà..
 
Pamulikwe kabisa. Pasi bezwee. Sema utawala huu na wao ni ukanda mmoja. Hakuna jipya
 
Back
Top Bottom