Pizza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pizza

Discussion in 'JF Chef' started by Bweri, Mar 3, 2012.

 1. B

  Bweri Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  X PASTER mwisho wa wiki nataka kula pizza ya kuku au nyama ya ng،ombe ila sijui hata nianzia wapi mwenye ujuzi plz nisaidie
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Pizza

  Vipimo:
  • Unga............................4 Vikombe
  • Maziwa ya unga.............2 vijiko vya supu
  • Mafuta ya zaituni...........½ kikombe
  • Hamira.........................1 kijiko cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Sukari..........................1 kijiko cha chai
  • Maji vugu vugu..............2 kikombe

  Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Unga
  • Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
  • Ufunike na uache uumuke.

  Sosi Ya Pizza
  1. Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo .. 1
  2. Thomu iliyokatwa ndogo ndogo ....... 3 chembe
  3. Sosi ya HP .................................. 3 vijiko vya supu
  4. Sosi ya tomato ............................. 3 vijiko vya supu
  5. Pilipili manga ................................. 1 kijiko cha chai
  6. Oregano ...................................... ½ kijiko cha chai
  7. Parsley (ukipenda) ......................... ½ ukipenda

  1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
  2. Epua kwenye moto.


  Upendavyo Katika Hivi Au Vyovyote Vinginevyo
  1. Tuna
  2. Nyama ya kusaga iliyopikwa
  3. Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande
  4. Sauage zilizokatwa
  5. Salami
  6. Vipande vya nanasi

  Vitu Vya Kujaza Juu Ya Pizza
  • Nyanya zilizokatwa vipande vipande
  • Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo
  • Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
  • Cheese ya Mazorella

  Jinsi Ya Kutayarisha

  1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size kama kwenye picha.
  2. Paka sosi juu ya unga
  3. Tia kiteo upendacho
  4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
  5. Mwagia cheese
  6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 au zaidi hadi ziwive pizza.
   
 3. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waaaaooh, nilitafuta hii kitu 4 a long tym! Thanx mkuu
   
 4. D

  Dine Member

  #4
  Nov 15, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kitambo nilitaka kujua jinsi inavyoandaliwa leo nimeinyaka asante sana
   
Loading...