Pius Ngeze: Mfupa uliomshinda fisi waonyesha dalili za kupata mlaji...

Waziri wa Kilimo unaombwa kutuma tume ya kuchunguza yale yanayoendelea kwenye bodi hii huku malalamiko yanazidi kuendelea.Ingawa katibu Mkuu ndie anaepajua vizuri maana alishafika na kuongea na wafanyakazi kipindi cha nyuma.

Ripoti za Bw Kumburu alizomwandikia Waziri wa Kilimo akishirikiana na Mh Zambi ambae ni Mbunge wa Mbozi waziri na timu yako mnaombwa kuunda timu ya kwenda kuhakiki kama kweli ni za kweli au la.

Kwa hili la fedha za wakulima wanaouuza kahawa zao mnadani ,na tofauti ya fedha baada ya kuadilishiwa kwenye exchange rate nzuri hiyo tofauti ndio fedha zinazoliwa na bodi hii na ni zaidi ya mabilioni ya Sh na sio bilioni moja au mbili ni zaidi ya bilioni tano na zaidi na ndio fedha anazozitumia Mkurugenzi huyu kusafiri nje ya nchi kila mara na kusambaza fedha kwa watu wachache ili wamsaidie kumlinda kwa kuwa fedha hizi hazina hesabu na wala hazitoki serikalini,Je huyu Mkulima anasaidiwaje na Bodi hii? Hili ndilo ambalo alihojiwa na wakurugenzi na kuambiwa kuleta maelezo ya kina na inasemakana mpaka sasa hajatimiza na ndicho kinachomsababisha kuipiga vita bodi hiyo iondolewe

Kutokana na Bodi ya wakurugenzi iliyochaguliwa hivi karibuni ambayo Bw Kumburu anaipiga vita ifutwe akishirikiana pia na Mbunge Zambi ambaye ni mdau kwenye ulaji huo wa fedha hizo ni kutokana na Bodi hiyo ya wakurugenzi kugundua haya yote pamoja na unyanyasaji mkubwa wa wafanya kazi unaofanywa na Bw Kumburu na yeye Kumburu anaona ulaji unataka kukatika ndio maana anawapiga vita.

Waziri Chiza unaombwa kuwaokoa wafanyakazi wa bodi hii na pia kuwaokoa wakulima wa kahawa kwa kufanya uchunguzi wa kina na pia unaombwa kuzifanyia kazi kwa undani ripoti zote alizokuandikia Mkurugenzi Mkuu huyo maana kutokana na uongo wa Mkurugenzi huyo akakuingiza pabaya ni mtu ambae hajali kama utaingia pabaya au la ni mtu ambae hanaga urafiki wa ukweli.Utakumbuka Alivyotaka kumwingiza pabaya waziri kwenye mkutano pale Morogoro mwaka juzi.
kwa kuleta sheria zake ambazo hazipo akishirikiana na Mwenyekiti wa wakati huo Bw Pius Ngeze.

Haya yote sio fitina wala majungu bali ni uhalisia wa mambo yanayoendelea kwenye bodi hii.
Huku akilalamika shirika halina fedha.Hivi sasa Mkurugenzi huyu anaelekea zake Italy kutalii kama kawaida yake huku ikiwa inasemakana hata Mwenyekiti wake akiwa hana habari ya safari hiyo akiongozana na maafsa wawili, je safari hizo zina manufaa yoyote kwa mkulima wa kahawa?

Naomba kurudia tena Kwako Waziri wa Kilimo unaombwa kuingilia ndani swala hili la bodi ya kahawa na usikilize pande zote mbili au tatu yaani Bodi ya wakurugenzi,Menejimenti na wafanyakazi bila kusita.
 
Ukisoma kwa undani sana hii thread, utajua moja kwa mjona imetoka kwa wafanyakazi wa TCB au watu wenye haabri za kina kabisa kutoka TCB. This is a shame, hasa ukizingatia kwamba macho na masikio ya wakuliam wote wa kahawa yapo TCB, kama organisation ambayo inasaidia kukuza vipato vyao.

Kuna mengi sana yamefanyika ili kukuza private buyers na kuua vyama vya wakulima na wakulima wenyewe. hebu jiuliuze, kulikuwa na haja gani ya kumpa DAE ltd na wengine leseni za kununua parchment wakati at least vyama vya msingi ndio vilikuwa vinahemea hapo? Ndio maana hadi sasa PCB wanatawala zadi ya 85% za zao la kahawa.

Ukiangalia yote haya, unaona kwamba lazima kuna shida fulani kwenye bodi ya kahawa. Ni mategemeo yangu Waziri mhusika atalifanyia kazi.
 
Back
Top Bottom