Pius Msekwa; Asiyeupenda muungano akajinyonge

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,662
15,015
Spika wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa amesema mtu asiyependa Muungano wa Tanzania akajinyonge.

Msekwa ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 26, 2022 wakati akiwasilisha mada kuhusu hatua mbalimbali ambazo viongozi wa Tanganyika na Zanzibar walipitia kabla ya Muungano.

Msekwa amesema Muungano wa Tanzania utadumu milele kuliko watu walivyodhani na kwamba hana shaka yoyote kuhusu hilo kwani anayaona mema.

"Muungano utadumu milele na milele,lakini asiyeupenda Muungano basi akajinyonge, tumepita kwenye mengi lakini mafanikio ni makubwa," amesema Msekwa.

Ameeleza historia ya waasisi wa Muungano ambao ni Hayati Julius Nyerere na Mzee Abeid Karume akisema kulikuwa na ulazima kuungana kutokana na hofu iliyokuwa imetanda kwa wakati huo kuhusu Zanzibar.

Amesema usalama wa Zanzibar ulikuwa shakani kwa sababu ya hofu ya waliopinduliwa kwambe huenda wangerudi tena katika eneo lao.

Kwa upande wake Balozi, Dk Getrude Mogella amesema wanaoongoza Taifa ni watoto wadogo lakini wanapaswa kuheshimiwa kwa nafasi zao.

Dk Mogella amesema ni utamaduni wa kawaida wazee wakifikia umri fulani kuwapisha vijana kushika usukani wa kiuongozi hivyo lazima kukubaliana na hilo.
 
Kama sababu ilikuwa ni hofu leo hiyo hofu bado iko? Na wasidanganye watu huu muungano Zanzibar ingekuwa na hofu usingekuwa na muundo wake kama hivi ulivyo. Kimsingi Tanganyika imepoteza na inaendelea kupoteza kwenye huu muundo wa muungano kuliko inavyo poteza Zanzibar.

Tulipofika muundo wa muungano hautaepuka kuwa wa serikali 3 au moja au uvunjike. Huu wa serikali mbili unanufaisha baadhi ya wateule wachache tu na wananchi walio wengi hawauridhii na hawa walio wengi iko siku watashinda tu.
 
1.Muungano wa mkataba.

2. Muungano wa serikali 3.

3. Muungano wa serikali 2.

4. Muungano wa serikali 1.

Wote hao wanapenda muungano.
Good summation.

Hawa Wazee wanapotosha sana. Mpaka sasa siyo rahisi kukutana na mtu anayeukataa muungano. Tatizo lililopo ni muungano wa aina gani tunaoutaka. Huo ndiyo mwiba kwa CCM na hawana jibu.
 
Wazee wamekuwa wa hovyo, vijana wao watakuaje sasa..
Lilianza lile liweight kuongea ujinga, amekuja huyu nae ropo anadhani ni nchi ile ya miaka yao. Kama kuna mijukuu yake humu ikamuelimishe aishi sasa.
 
Muungano ni mali ya yule Bibi wa uingereza.
Na wanaogopa muungano ukivunjika Basi OMAN atarudi kwenye koloni lake.
 
We Mzee muda wako na wenzio ushaisha..hii Tanzania si ya kwenu tu nyie wazee.

Tunaishi hapa duniani kwa wakati, huu ni wakati wetu na KATIBA MPYA ni sasa.

Hakuna asiyeutaka muungano ila tunataka Muungano wenye muafaka kati ya sisi watanganyika na wenzetu wa Zanzibar

Kifupi tu mzee wetu hakuna wa kujinyonga ila serikali 3 hazitakwepeka...we need our Tanganyika back.
 
We Mzee muda wako na wenzio ushaisha..hii Tanzania ni ya kwenu tu nyie wazee.

Tunaishi hapa duniani kwa wakati, huu ni wakati wetu na KATIBA MPYA ni sasa.

Hakuna asiyeutaka muungano ila tunataka Muungano wenye muafaka kati ya sisi watanganyika na wenzetu wa Zanzibar

Kifupi tu mzee wetu hakuna wa kujinyonga ila serikali 3 hazitakwepeka...we need our Tanganyika back.
Serikali ni moja tu mkuu, zote hizo tatu ni za nini tena wakati huu.

Tulishapita muda wa majaribio, sasa ni kumaliza kila kitu nchi iende mbele.
 
Muungano wa hovyo unatetewa na wazee wa hovyo..hakuna asiyeukataa ila urekebishwe..tunataka serikali moja au la rudisheni serikali ya Tanganyika..mambo ya kuivika Tanganyika koti la muungano hatutaki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama sababu ilikuwa ni hofu leo hiyo hofu bado iko? Na wasidanganye watu huu muungano Zanzibar ingekuwa na hofu usingekuwa na muundo wake kama hivi ulivyo. Kimsingi Tanganyika imepoteza na inaendelea kupoteza kwenye huu muundo wa muungano kuliko inavyo poteza Zanzibar.

Tulipofika muundo wa muungano hautaepuka kuwa wa serikali 3 au moja au uvunjike. Huu wa serikali mbili unanufaisha baadhi ya wateule wachache tu na wananchi walio wengi hawauridhii na hawa walio wengi iko siku watashinda tu.
2005-6 pale Kuna padri zenji ulimi ulimteleza,lukuvi akayarudia
 
Toka tulivyowapelekea mwinyi kutawawal Zanzibar Happ nikapata mashaka kwamba wanzanzibar watataka nao kupata mtu wao atawale tanganyika

Tuwe makin mbeleni kwa Hali hi wataka tuwe tunabadilishana viongozi wa kutawala Tanzania kwamba akitoka mziibar bas wakufuta awe mtz hatutatki hyo kitu
 
Back
Top Bottom