KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Kweli kabisa.Watu hawajui kwamba hiyo katiba ya 1977 ni huyo huyo Msekwa ndiye mtunzi.
Lakini si ndiye angetoa ufafanuzi kwa nini ilihitajika iwe hivyo kwa wakati huo, na kwamba sasa inahitajika nyingine kufuatana na hali iliyopo?
Watu kama huyu ndio wangesimama mbele bila ya woga wowote kusimamia maslahi ya nchi hii, badala ya maslahi ya kikundi cha walafi waliopo CCM.
CCM hii iliyopo, siyo CCM iliyokuwa inapigania maslahi ya wananchi wa Tanzania kama waliyokuwa wakiiongoza wao. Kukaa kimya kwa uoga ni kusaliti nchi waliyotaka kuijenga wao. Mwalimu Nyerere asingesita kuwaaibisha hawa mafisi waliopo sasa hivi ndani ya chama hicho.
Kwani anaogopa nini, watamnyima mafao yake?