Pitia Hii Muhimu:Mtindo hasi wa maisha wa kutozingatia lishe bora na mazoezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pitia Hii Muhimu:Mtindo hasi wa maisha wa kutozingatia lishe bora na mazoezi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by King Kong III, Oct 27, 2012.

 1. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  -Mtindo huu hasi wa maisha,mtindo wa karaha kuwa raha ,tukubaliane lishe za hovyo ni chanzo cha maradhi ya kusendeka(maradi yasiyoambukiza) saratani,kisukari,shindikizo la damu,kiarusi na maradhi ya moyo,Tubadirike wabongo na style zetu ya maisha.

  -Mbongo akiamka asubuhi anaenda mgahawani anahagiza supu chapati tatu chai na soda ya baridi pembeni mwenyewe anasema anajichana ila ktk hali halisi anachanika,ndio anachanika coz chakula hiki ukitumia mara kwa mara sio lishe njema ni lishe mbovu coz mrundikano wa mafuta na sukari lkn kwake mbongo ndio lishe bora maana mbongo kwake nyeusi ni nyeupe

  -Baadae ikifika mchana anaagiza chipsi mayai wenyewe wanaita zege juu mguu wa kuku na mishikaki miwili mitatu kisha yote hio anaishushia kwa soda baridi ukimuuliza kulikoni anakujibu tangu lini mwili ukajengwa kwa matofali? Ni makosa yale yale ni mrundikano wa mafuta sukari na wanga lkn mbongo hasikii maana kwake hasi huwa chanya

  -Inaingia Jioni Lete moja moto moja baridi kata mti panda mti mbongo na bia bia na mbongo pembeni na mishikaki,yale yale sukari wanga na mafuta akitoka hapo utamuonea huruma mbongo anahemea juujuu tumbo limefurika na kwa mujibu wa mbongo kama huyo ambae amejijengea imani potofu milo kama hii inanenepesha na kuwa na kitambi ni kiashirio cha kuwa pesa na hana utamaduni wa kufanya mazoezi kutembea kwa miguu kwake ni sumu yeye na gari tu,kupanda ngazi kwake ni nuksi yeye na lifti tu.

  -Matokeo yake utamkuta mbongo ana kichwa kimeungana na shingo kifua hana badala yake ana bonge la tumbo chini miguu mithiri ya njiti ya kibiriti yupo yupo tu mithiri ya TUFE

  Tubadirike wabongo na style zetu ya maisha

  Kwa Audio Clip ya huu ujumbe Sikiliza Hapa Chini nime-attach

   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hayo mambo labda yanamuhusu babu DC
   
 3. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  asante kwa ushauri mkuu
   
 4. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,357
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...