kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,815
Habarini wana jamvi,namshukuru Mungu TCRA wamenikosa, na pia siwazi sana maana simu feki zimeletwa na mchina na bahati mzuri hata huo mtambo wa kuzimia simu umeletwa na mchina, kwahiyo naamini hakitaaribika kitu!!
Wakuu kuna mwanamke hapa tupo kwenye mahusiano,kabla yangu alikuwa na mwanaume wake mwingine kutokana na ulevi wake na tabia zake (kwa jinsi alivyonisimulia huyu mwanamke) aliamua kujitoa ndipo alipokutana nami na kufungua ukurasa wa mapenzi.
Nimeishi naye kwa muda kidogo mara yule ex wake akanipigia simu tuonane tuongee kiume,nikaonana naye bila kumpa taarifa huyu mwanamke, jamaa alitiririka mengi hadi akawa analia akiniomba nimuache huyu mwanamke labda akiwa hana mtu anaweza kumsamehe maana alimuacha kwa bahati mbaya na bado anampenda, tukaongea mengi sana kama unavyojua wanaume hatunaga kinyongo tunapokutana, nikamwambia asubiri nitampa mrejesho..
Sasa wakuu ndo nipo nawaza nifanyeje na mwanamke ametulia na of course ananipenda na namfurahia,. naombeni uzoefu nifanyeje katika hili........ (Mwanamke sijamwambia chochote na hawana mawasiliano kwasasa maana namba amebadilisha kwasababu alikuwa anamsumbua sana kumuomba msamaha na jamaa aliomba nimpatie namba sikumpa)