Chachandu ya pilipili, yaani pilipili ya kusaga

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,775
6,553
Jinsi ya kutayarisha (CHACHANDU YA PILIPILI) yaani pilipili ya kusaga..

Mahitaji:
1.Pilipili
2.Tangawizi
3.Kitunguu saumu
4.Ndimu natural au mchina
5.Chumvi
6.Nyanya
7.Kitunguu maji na
8.Mafuta ya kupikia
9.Maji kwa ajili ya kusaidia kusagia kwenye blenda

Jinsi ya kupika
Changanya kuanzia 1 hadi 6 kwa kuvisaga kwenye blenda ukishamaliza, weka mafuta yako jikoni kisha tia kitunguu maji kikiiva weka ule mchanganyiko wako kwenye hayo mafuta pika mpaka maji yapungue uone mafuta. Hii husaidia chachandu yako ikae muda mrefu bila ya kuharibuka..

Cheers!
 
Alternatively, unaweza kutumia carrots badala ya nyanya halafu unablend mahitaji yote pamoja na vitunguu maji pia. Unabandika jikoni, unaweka mafuta ya kupikia kiasi vinachemka pamoja. hii inakuwa na utamu kwa mbaaaali kutokana na carrots ulizotumia.

oooh thanx kwa hiyo mupya..
 
Na nyingine wasaga kwa pamoja
nyanya 1
kitunguu maji 1
swaumu kisi
tangawizi kiasi
karoti 1
tango 1
na pilipili jinsi upendavyo, ukimaliza waweka ndimu na chumvi, ni tam sana.
 
kuna mchanganyiko mmoja tulikuwa tunaenda nao shule-boarding wakati huo miaka ya 98 hivi ila nimesahau ilikuwa inachanganywa vipi, tulikuwa tunaweka na vipande vya nyama nao ulikuwa mchachandu mzuriii sana
 
yakatuni.jpg
 
Wakuu naomba munisaidie ..nataka kujua namna ya kitengeneza au kupika pilipili ya kutoelea mishikaki..kwani napenda sana kuchoma mishikaki but testi ya pilipili sijui kuifanya..msaada please
 
Unasema pilipili ipi ile ya mbichi unayoblendi pamoja na karoti na swaumu nk au???
 
Kumbe unaweza kutia na karoti pia!? Mie hutengeneza kwa kuweka pilipili, kitunguu swaumu, limau, chumvi na wakati mwingine giligilani, ni nzuri sana.
kuwa na mwanaume kama wewe unayeijua girigilani unatakiwa uwe mtaalamu wa mapishi maana mkurya wangu mmoja alipoona kwa mchuzi giligilani akaniambia nimemuwekea majani ya uchawi bado kidogo nichezee mabao
 
Hahahahah lol! hakawii kususia chakula, "Mke wangu anaanza kuniroga, nimekuta katika mboga ametia vimajani majani kwenye mboga, machale yakanicheza nikaamua kususa kula." kwi kwi kwi....


kuwa na mwanaume kama wewe unayeijua 4ligilani unatakiwa uwe mtaalamu wa mapishi maana mkurya wangu mmoja alipoona kwa mchuzi giligilani akaniambia nimemuwekea majani ya uchawi bado kidogo nichezee mabao
 
si kula ni kura best dah kuna watu noma alinuna alikasirika hapa nimekumbuka nimecheka sana loo
Hahahahah lol! hakawii kususia chakula, "Mke wangu anaanza kuniroga sasa nimekuta katika vimnajani majani kwenye mboga, machale yakanicheza nikaamua kususa kula." kwi kwi kwi....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nilipitiwa badala ya kutumia R nikatumia L lol!!!!....kwi kwi kwi kwi

si kula ni kura best dah kuna watu noma alinuna alikasirika hapa nimekumbuka nimecheka sana loo
 
Nilipitiwa badala ya kutumia R nikatumia L lol!!!!....kwi kwi kwi kwi

sambusa hali,akiona ile chatne anasikia kutapika hawa ndo jirani zake watu8 wao chakula maugali tu tena magumu yanayokaba kwa koo hata ukisokomeza na mlenda.
BAK nimeweka thread ya apetizer itakufaa kaipitie
 
Last edited by a moderator:
Shukrani amu....unajua kutengeneza tomato soup au onion soup kama appetizer? Hizi huwa nazipenda mnoo. Kuna hotel Dar (siku hizi haipo) walikuwa wakitengeneza appetizer ya prawns nadhani walikuwa wanachemshwa sijui na nini tena kiliwekwa kwa wale prawns...yaani walikuwa ni watamu balaaa!!! Mara nyingi tulikuwa tukienda lunch basi na dinner inaunganishwa hapo hapo lol!!!!

sambusa hali,akiona ile chatne anasikia kutapika hawa ndo jirani zake watu8 wao chakula maugali tu tena magumu yanayokaba kwa koo hata ukisokomeza na mlenda.
BAK nimeweka thread ya apetizer itakufaa kaipitie
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom