Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Hawa jamaa nasoma kuwaelewa lakini wapi! Yaani wanapata wapi Mafuta ya ku-propel fast moving engines that far offshore? Engine yenye horse power 75 inakula litre 200 kati ya Zanzibar and Dar kwa mwendo wa kawaida. Sasa hawa jamaa wanakuwa na litre ngapi huko baharini kwa umbali huo? Je wanabebaje? Je, huo uharamia wao wanatutia satellite ku-track ships au wanabahatisha? This is very strange!
Kwa kweli hata sijapata picha yenyewe. tafadhali mwenye kujua atuelezee kwa data.
Mkuu,inaonekana hawa maharamia wanajua vizuri hiyo kazi yao,kumbuka katika historia haya mambo ya uharamia yalianza muda mrefu,haswa sehemu hizo za Pwani zenye Uchumi na serikali dhaifu,watu wengi wanaishi kwa uharifu baharini haswa hapo Ghuba ya Aden.Ambapo panapita luxury Boats na meli nyingi zenye shehena ghali (expensive).
Kwa mujibu wa takwimu kutoka News week magazine (Toleo la Dec'1) kwa mwaka huu wa 2008 kumekuwa na matukio 95 ya uharamia huo ambapo kuna jumla ya crews 300 wameshikiliwa na maharamia katika mji wa Eyl kaskazini mwa Mogadishu,na kwa kipindi hichi cha mwaka mmoja tu hao maharamia wamekwishalipwa jumla ya $30mil ili kuachia mateka na Meli walizoteka.Maharamia hao hawana rekodi ya kuua mateka wao.
Pirates hao wanakimbilia kusini baada ya eneo zima la Ghuba ya Aden kuzidishiwa Patrol baada ya kuteka meli kubwa ya mafuta ya Saudia iliyojulikana kwa jina la Sirius Star katikati ya Novemba,Meli hiyo kubwa kuliko zote kuwahi kutekwa ilikuwa imebeba Mafuta ghafi yenye thamani ya $100mil, Meli hiyo ilipelekwa kwenye mji wa Harardhere ambao nao upo kaskazini mwa Mogadishu.
Baada ya tukio hilo Nchi za Djibouti,Egypt,Sudan,Jordan na Saudia zilikutana na kukubaliana kufanya Patrol ya pamoja katika Gulf hiyo,pia kuna meli za Patrol kutoka Russia na US kusindikiza Meli zao za mizigo,hali hiyo imewafanya Pirates kukimbilia kwenye Pwani za Kenya na Tanzania ambazo bila shaka ulinzi wake ni mdogo.
Imekuwa rahisi kuteka Meli za mizigo kwa sababu kuna sheria ya kutoingia na silaha kwenye Meli za Mizigo na Abiria kama ilivyo kwenye Ndege,nafikiri kwa kuongezeka vitendo vya uharamia,kutarekebishwa baadhi ya sheria za usafiri wa meli ili kuwapa uwezo wa kujihami crews na abiria wa meli hizo.
Ukiacha Somalia, Nigeria na Indonesia ni nchi nyingine zinazoongoza kwa uharamia Baharini.