Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,762
- 40,987
Serikali yakwama mahakama kuu uchaguzi wa madiwani
Na Nora Damian
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi la serikali la kuomba mahakama hiyo isisikilize ombi lililowasilishwa na vyama vinne vya upinzani nchini vinavyotaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa madiwani katika kata 16, uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Njengafibili Mwaikugile wa mahakama hiyo na aliongeza kuwa mahakama hiyo leo itasikiliza maombi yaliyowasilishwa na vyama vinne vya upinzani ili kuamua uchaguzi huo usitishwe au la.
�Hoja zilizowasilishwa na serikali kupinga mahakama isisikilize maombi ya upinzani kwamba isimamishe uchaguzi, hayakupaswa kuletwa sasa kwa sababu hoja zinazungumzia maombi yenyewe, walipaswa kuleta wakati wa kusikiliza maombi yenyewe,� alisema Jaji Mwaikugile.
Jaji Mwaikugile pia alipinga madai yaliyowasilishwa na serikali kwamba maombi ya wapinzani yameletwa chini ya kifungu ambacho sio sahihi na kusema kwamba kifungu hicho ni sahihi.
�Kifungu hicho cha nne cha Sheria ya Haki za Msingi na Wajibu wa watu ni sahihi kwa kuwa mtu akiona haki zake za kikatiba zinavunjwa hakuna, kifungu kingine kinachoweza kutumika zaidi ya hiki,� alisema.
Juzi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha pingamizi katika mahakama hiyo akitaka kutupiliwa mbali kwa ombi la vyama vinne vya upinzani vinavyotaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi wa madiwani katika kata 16, uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo.
Wakiwasilisha hoja zao kwa zamu, mawakili watatu wa serikali, Joseph Ndunguru, Paul Ngwembe na Abraham Senguji walidai kuwa maombi ya upinzani yamepitwa na wakati na kwamba yanapingana na ibara ya 74 (6) (d) ya katiba ya nchi.
Katika ombi lao la msingi, vyama vya Chadema, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF pia vinaitaka mahakama kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha Uchaguzi wa Madiwani.