Pingamizi la Dr Slaa dhidi ya Rose Kamili lakataliwa mahakamani

Kuna kipindi si kirefu watu walitunduka humu picha ya mwanamke mwenye mtoto mdogo ambaye alitelezwa baada ya kuzaa na Kikwete. Habari hiyo mmeifinyangafinyanya hadi kuipotezea mbali. Ingekuwa ni ya kiongozi wa chadema magazeti na vyombo vingine vya habari kurasa zisingetosha. Mama mwenyewe alionekana kuchoka sababu ya kutelekezwa, maana viongozi wengi wa nchi hii wanavutiwa na vimwana wanapowakawaka, wakishaishiwa pouger huwatelekeza na kutowapatia child support.

JF kuna wenye kumbukumbu hizo ipo situ watatundika vitu hivyo tuakisi ukweli

Mkuu kama una ushahidi wa kutosha wasiliana na huyo mama mmepelekeni JK mahakamani kama alivyopelekwa Omar Mahita.
 
Katibu wa CCM Nape Mnauye ililetwa mada hapa kukanwa na familia ya Mnauye kwamba si mwanafamilia, ni wa kuzaliwa toka mwanamke asiyetambuliwa kama mke rasmi vinginevyo wanafamilia wa kweli wa Moses Mnauye wasingemweka kando. Hapa angekuwa kiongozi wa Chadema mngetoa povu jingi mno isivyo kawaida.

Mkuu sijakuelewa unavyoleta mfano wa Nape kwenye sakata ili, kwa hiyo hao watoto wawili wa Rose Kamili, Dr Slaa kawakana.
 
Wewe ndio unajiita msomi? Kabla sijaanza mjadala na wewe msomi Lukurunguru jifunze kwanza matumizi ya herufi kubwa na ndogo JF kuna Greant Thinkers usiandike kama mtoto wa Kindergarten.
.

Hahahaha...jitu puuzi always lipo kuangalia vitu ambavyo havina substance yoyote. Look, hapa tunajadili issue ya uandishi na ustadi wa sentensi? crazy guy......Halafu seems huna kazi nyingine ya kufanya ndiyo maana watu tukipiga mzigo tukirudi kuchungulia JF wewe upo online.....au JINI?
 
mungu yupo pamoja na mama yetu rose kamili.

kwa kweli hata mimi nasema mungu atakuwa pamoja na mama huyu ambaye dr. Slaa mumewe alimkimbia na anataka kufunga ndoa na huyo josephine aliyeacha ndoa yake na kuingilia ya mwenzie
mimi niliachwa kama huyu mama rose lakini mungu hakuniacha mpaka sasa ninashuhudia mkono wa mungu ukiwa pamoja nami
mungu anachukia kuachana kwenu dr. Slaa mrudie mke wako mna watoto wawili na mlitoka mbali na mama huyu
kuwa na hofu na mungu
asante
 
Sheria inahesabu kuwa mwanaume akiishi na mwanamke kwa miaka miwili au zaidi hao ni wanandoa regardless wana watoto au laa.... Mbaya zaidi Dr. Slaa kazaa ma Rose watoto 2, kaazi kweli.... yaani patamu hapo..
Kwa maana hiyo na Josephine naye ni mke wa Dr. Slaa kwa maana wana mtoto na wameshakaa zaidi ya miaka miwili
 
Kwa hiyo kesi ndiyo imeanza eeeeeee!! hebu tusikie matokeo yake!! Ila ninachojua huwezi kulazimisha ndoa ambao mapenzi yalisha kwisha!!! Cha msingi Dr. mpe talaka Rose!! Kiukweli kuishi na mwanamke kwa miaka miwili hata kama hujafunga ndoa kidini/kiserikali/kimila jua ni mke!! Na mkitengana kwa miaka miwili bila tendo la ndoa basi ndoa ni batili na inastahili kuvunjwa!!! Both applies, so Dr. na Rose fikieni maamuzi ya busara muachane na comedian za SSM!! Hivi ni kwa nini Rose yuko CDM tena ni mbunge wakati ni kiranja wa SSM?
 
Mkuu kama una ushahidi wa kutosha wasiliana na huyo mama mmepelekeni JK mahakamani kama alivyopelekwa Omar Mahita.

Ritz!! Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!! uliza taratibu maji yakimwagika hutayazoa!! Yatazidi yale ya tsunami!!
 
Wanabodi,



Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na ‘mkewe’ Rose Kamili Slaa nee Sukum, akiomba mahakama hiyo imzuie ‘mumewe’ Dkt. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Laurnce Kaduri ambaye alisema amepitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dkt. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo na amefikia uamuzi wa kuona hoja zilizowasilishwa mbele yake na Dkt. Slaa zikiomba mahakama hiyo iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose, ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.

Jaji Kaduri alisema Dkt. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake Josephine kwa taratibu za kisheria kwa sababu Slaa na Rose hawakuwai kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.

“Mahakama hii inaitupilia mbali, tena kwa gharama, pingamizi hilo la Dkt. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawai kufunga ndoa, kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, sheria inawahesabu kama ni wanandoa, hivyo Mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na mahakama inatupilia mbali pingamizi la Slaa,” alisema Jaji Kaduri.

Kesi ya msingi itatajwa mahakamani hapo Novemba 6 mwaka huu.


  1. Kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dkt. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwa ajili ya kupatanishwa.
  2. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dkt. Slaa bado ni wanandoa.
  3. Dai la tatu, anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dkt. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
  4. Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe (Dkt. Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.

“Pia, nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili”

Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dkt. Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.

Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya Shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake.

Akaongeza kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

Source: wavuti.com - wavuti


Matatizo ya ndani kila mmoja anayo. Tusipoteze muda hapa
 
Back
Top Bottom