Pingamizi la Dr Slaa dhidi ya Rose Kamili lakataliwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pingamizi la Dr Slaa dhidi ya Rose Kamili lakataliwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Oct 19, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na ‘mkewe’ Rose Kamili Slaa nee Sukum, akiomba mahakama hiyo imzuie ‘mumewe’ Dkt. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.

  Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Laurnce Kaduri ambaye alisema amepitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dkt. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo na amefikia uamuzi wa kuona hoja zilizowasilishwa mbele yake na Dkt. Slaa zikiomba mahakama hiyo iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose, ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.

  Jaji Kaduri alisema Dkt. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake Josephine kwa taratibu za kisheria kwa sababu Slaa na Rose hawakuwai kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.

  “Mahakama hii inaitupilia mbali, tena kwa gharama, pingamizi hilo la Dkt. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawai kufunga ndoa, kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, sheria inawahesabu kama ni wanandoa, hivyo Mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na mahakama inatupilia mbali pingamizi la Slaa,” alisema Jaji Kaduri.

  Kesi ya msingi itatajwa mahakamani hapo Novemba 6 mwaka huu.


  1. Kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dkt. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwa ajili ya kupatanishwa.
  2. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dkt. Slaa bado ni wanandoa.
  3. Dai la tatu, anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dkt. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
  4. Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe (Dkt. Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.

  “Pia, nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili”

  Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dkt. Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.

  Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya Shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake.

  Akaongeza kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

  Source: wavuti.com - wavuti
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  mkuu unawazaga vitu viwili tu.........Dr.Slaa na Ukiristo
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndoa kati ya Dr Slaa na Rose Kamili ilifungwa wapi, na lini?
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  He, kazi imeanza.
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Dr slaa kwa vimwana ni balaa, ile picha aliyopiga wakati anampa Esther Wassira kadi inaelezea yote, jamaa ni balaa
   
 6. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Sheria inahesabu kuwa mwanaume akiishi na mwanamke kwa miaka miwili au zaidi hao ni wanandoa regardless wana watoto au laa.... Mbaya zaidi Dr. Slaa kazaa ma Rose watoto 2, kaazi kweli.... yaani patamu hapo..
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mungu yupo pamoja na Mama yetu Rose Kamili.
   
 8. Myocardial Stunning

  Myocardial Stunning Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahaha ... huyu jamaa alafu anataka kuja kuongoza nchi!.. while ku control hao wanawake wawili wakakaa wakayamaliza hawezi...

  slaa ni more than mchekeshaji ..
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Shehe wa mkoa wa DSM Sheikh Alladi Mussa amesema waislam wanaoandamana ni wahuni na vibaka
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Here we go again, tuko busy na fujo za ndugu zako wanazoendelea kuzifanya katika taifa letu hili la amani na hasa waloyafanya leo Dar na Zanzibar we uko busy na ndoa za watu? "Harusi siyo yako we waishonea suti?". Well miafrica ndivyo tulivyo Ritz
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Dah!!! Nimeshangaa kuona JF Leo iko silent. juu ya tukio hili. Haya yetu macho ngoma inogile.
   
 12. T

  Top Cat Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rose Kamili anatumiwa. Hana shida kwa sasa; ni mbunge na ameshajijenga. Angemwacha kibabu atengeneze first lady wake bila matatizo. Ina maana Rose....kama Willy akikuomba nanhii utampa? unaona! achana nae bhana
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu haya ni masuala ya kisheria hayataki kulazimisha sheria ni taaluma Jaji Laurnce Kaduri ni msomi aliyebobea hawezi kukurupuka kutoa hukumu.
   
 14. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kumbe Mheshimiwa alikuwa akizini miaka yote hiyo. kwani dhehEbu la Mh Dr Slaa linahalalisha uzinzi? hatari hii.
   
 15. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,667
  Likes Received: 17,712
  Trophy Points: 280
  Ndio kipaumbele cha Chama Chako, yaani unrest inayoletwa na waislam we haikuusu, ni nani ya kumleta ku-disscus huu ujinga
   
 16. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mmeona mmerikoroga la udini mnataka mponee kwa dk, malizen kwanza hilo mlilolianzisha la udini la sivo hakuna mtu atakae waelewa
   
 17. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Kasome The Law of Marriage utajua ndoa ilifungwa lini
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani hii habari ni ya uongo? usitake kuziba watu midomo kwa mapenzi yako mkuu.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Shehe wa mkoa wa DSM Sheikh Alladi Mussa amesema waislam wanaoandamana ni wahuni na vibaka
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu mbona hakuna uhusiano wowote na hii hukumu ya leo.
   
Loading...