Pinda: Zanzibar sio NCHI... Werema: Zanzibar ni NCHI (Serikali yao ni MOJA, RAIS wao ni MMOJA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Zanzibar sio NCHI... Werema: Zanzibar ni NCHI (Serikali yao ni MOJA, RAIS wao ni MMOJA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jul 5, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huku akiwasilisha kwa mbwembwe zilizoonekana kuwa ni za kishabiki akipinga hoja zilizowalishwa na kambi ya upinzani bungeni, Werema alishindwa kuunga mkono hoja ya Upinzani kuhusu mstakabari wa TZ baada ya Zanzibar kuutangazia UMMA na dunia kuwa ni NCHI.

  Werema alisema zanzibar ni nchi ndo maana ukaungana na Tanganyika ambayo pia ni nchi ili kutengeneza JMT. Werema alitumia maneno ya kejeli eti kiswahili sio lugha mama ya upinzani, hawajui kiswahili vizuri ambapo yeye pia alijifunza na kwa vile ni msomi mzuri alielewa kiswahili barabara.

  Werema anashindwa kutofautisha wakati uliopita na uliopo ktk lugha ya kiswahili. Kwa wakati uliopita Zanzibar ilikuwa nchi, na kwa wakati uliopo zanzibar sio nchi, hivyo kunauwezekano mkubwa kuwa katiba ya JMT imevunjwa na rais wa JMT anastahili kujibu mashitaka ya kuvunjwa kwa katiba aliyoapa kuilinda.

  Kama Zanzibar na Tanganyika bado ni nchi ktk sheria za leo, basi JMT sio nchi ni umoja wa nchi mbili znz na tgk.

  HUKU akijua kuwa kauli yake hiyo inamburuza PINDA waziri wake mkuu, ambaye aliwahi kusema kwa ujasiri kuwa Znz sio nchi as we speak. Werema alitaka kuthibitisha kuwa wakati PINDA anasema vile hakuwa amepata ushauri wa AG kitu ambacho kinamfanya PINDA awe kituko ktk suala zima la uongozi wa nchi hii.

  Hadi hapo tutakapopata ufafanuzi wa wanasheria wengine suala hili linabaki kuwa Werema, AG amemsihaki Pinda, PM kuhusu zanzibar kuwa nchi au la.

  Wanasheria waliobobea kwenye masuala ya sheria na katiba please tutegulieni kitendawili hiki.

  Nawasilisha.
   
 2. H

  Hebron Caleb JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is the confusion among our leaders, nilikuwa najaribu kutafakari haya mambo baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari ambavyo bunge limekataa kuviamini na nikashangaa kusikia Mwanasheria Mkuu wa serikali anapingana na waziri mkubwa hatari mambo haya ndugu zangu. Where are we going??? Wasomi wa sheria tusaidieni tafadhali!!
   
 3. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Muungano ambao wao wenyewe kuueleza hawawezi bado hawataki ujadiliwe! Irresponsible leaders indeed.
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama pinda alisema zanzibar sio nchi na upinzani wamesema hivyo hivyo basi huyo AG amwambie na pinda kua kiswahili sio lugha mama kwake mbona kaisema upinzani tu...na ye ni mnafiki aishie zake
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wote wanasheria
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,931
  Trophy Points: 280
  Kama Mwanasheria mkuu wa Serikali (ambaye ndiye mshauri mkuu wa serikali katika mambo ya kisheria) anatoka kauli ya kupingana na Waziri mkuu (ambaye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za serikali) na mambo yanaachwa yaende as usual, basi tengeneza picha ya hiyo serikali na utapata picha ya lidude la ajabu hapana mfano.

  Kwangu napata picha kama ya likiumbe fulani hivi; Uso uko kwenye goti,makalio yako kisogoni na mikono imeota sehemu za siri. Halina mfano dude hilo, kweli nimeamini nchi yetu ni LIWALO NA LIWE.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Zanzibar sio nchi ila ni sehemu/mko ndani ya JMT
   
 8. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hii yote imeletwa na Mkapa alipo ruhusu ZNZ kuwa na bendera yao ya Taifa, Wimbo wa taifa hilo ndilo kosa kubwa sana alilifanya Mkapa alilifumbia macho sasa madhara yake ndio haya, ZNZ pia inakatiba yake.

  nifahamuvyo mie kwa uwelewa wangu mdogo nchi ikiwa na bendera yake ya utaifa na wimbo wake pia basi jua hiyo nchi ni jamuhuri kwa maana inajitegemea yenyewe kwa kila kitu bila kutegemea nchi nyenzake (Tanzania)

  serikali ya JMTZ ina jumla ya marais 5: Kitwete, Shein,Dr. Balali, Maalim Sefu, Balozi Seif Ally hao wate wana hadhi ya rais wanapewa ulinzi na watalindwa kama marais.
  kwa nchi kama yetu ambayo "ni maskini" kuwa na mzigo wote huu wa marais 5 ni garama kubwa sana na mzigo wote huu anabebeshwa mlalahoi kwa kukatwa kodi kubwa kila mwezi.
   
 9. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni nchi ndani ila si nchi nje- JK
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  futikafutikafuti na futikafutikafuti=tui na nazi
   
 11. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 648
  Trophy Points: 280
  Hahaha....hiyo kali!
  JK ni kiboko kwa kuepusha upepo upite.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Huu sio MUUNGANO ni MJUMLISHO yaani 1+1=2 au Zanzibar+Tanganyika=Zanzibar+Tanzania
   
 13. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zanzibar kila kukicha wajitoa kidogo kidogo, Tanganyika walitumiwa tu enzi hizo na sasa hawahitajiki.Zanzibar sio nchi kabla ya katiba ya 2009
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Liwalo na liwe zanzibar ni nchi
   
 15. d

  dkn Senior Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Zanzibar na Tanganyika si nchi. Tanzania ni nchi yenye kuwa na Muungano wa Tanganyika na visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja). Tatizo wengi wa Wazanzibari wanachukulia Tanzania ni Tanganyika kwa sababu ambazo zinakubalika kama mgawanyo wa rasimali ukiegemea upande mmoja wa Tanganyika (Tanzania Bara), tatizo kubwa ni structure ya Muungano na hayo wanayosema kero za Muungano. Kama ni Muungano basi hakukuwa na sababu ya kuwa na Marais wawili (wa Muungano na Zanzibar). Kama Zanzibar walitaka (tokea mwanzoni) wawe na Rais then ilikuwa na weakness ya viongozi kwani Tanganyika ingekuwa na Rais pia na Rais wa Muungano awe mmoja au kungekuwa na position kama Makamu wa Rais - Tanganyika na Makamu wa Rais - Zanzibar wawe chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 16. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Zanzibar si nchi bali ni koloni la Tanganyika.
   
 17. k

  kula kwa tindo JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Shalom wana JF...
  Hili jamvi huwa naliheshim mnoo.
  Kwanini:
  1: JF ni zaidi ya Chuo.
  2: JF ni mahala pekee uwezapo kulisha Ubongo na Ukashiba..
  Kwa mbumbumbu ataingia humu akichukulia kama FB.Twiter.n vjiblog vya udaku ...
  Wakuu tusishangae sana na yanayotokea sasa hasa kwa hawa jamaa..
  Hawa jamaa walisha potea kutambo tu.. Toka aondoke RA hali imekua mbaya ktk kundi(CCM) hili ambalo sasa limejikita kufunga midomo ya wenye chao kwa kuua..
  Werema alishasema kua KATIBA iliyopo ni mzuri na hakuna haja ya kutengeneza mpya..
  Lisu huyuhuyu aliichambua KATIBA hii na kuweka peupee kila lile lililo pungufu pale mjengoni, Gamba wakazomea lkn mwishowe wakasalim.. Nani Mwanafunzi hapo kati ya WEREMA & LISU?
  Issue ya Madaktari Mjengoni "LIWALO NA LIWE" alisema kukikua na maazimio 10 na 5 wamekubaliana na 5 uamekwama. "DHAIFU" kasema maazimio yalikua 12, sasa hapo tumuamini nani? Kwa akili ndogo tu, huyu anayejiita AG hatambui kua mtu kuleta maneno (ripoti inayo kinzana) tofauti nu dalili ya uwongo?
  Kwa nini tusiamini kua hii Serikali yooote imeoza??
  LIWALO NA LIWE aliona Mwezi ,pale alipocta kutoa tamko la Serikali kwakua issue iko Mahakamani, ajabu "DHAIFU " Katoa maamuzi jambo ambalo bado liko Mahakamani, Tusemeje hapo!!!
  HAJUI SHERIA?
  MWANASHERIA WA SERIKALI NDIYE HAJUI?
  HAJUI MIPAKA YAKE KIKATIBA?
  KI BURI NA JEURI YA UDHAIFU ALIONAO?
   
 18. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hesabu halisi ya Muungano wetu ni kile Nyerere alichomwambia Jumbe kuwa ni mjinga kwa kuhesabu 1+1=3:
  Serikali ya Zanzibar+{Serikali ya Tanganyika+Serikali ya Muungano}= Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Ingawa Serikali ya Tanganyika haionekani kwa machouchi, lakini ndiyo ile inayofanya shughuli zisizokuwa za Muungano.
   
 19. d

  dkn Senior Member

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna ukweli ndani yake haswa kwenye issue ya rasimali...

   
 20. Imam Yussuf Shamsi

  Imam Yussuf Shamsi Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Twende kidogokidopo ipo siku tutaelewana
   
Loading...