Pinda: Umasikini umepungua Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Umasikini umepungua Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mzeewapori, Sep 22, 2010.

 1. m

  mzeewapori Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema Tanzania imefanya vizuri katika elimu, kupunguza umasikini na kukabiliana na magonjwa ya Malaria na Ukimwi.

  Alisema juhudi hizo zinafanyika, ikiwa ni katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) na itajitahidi kukamilisha malengo yaliyobaki katika kipindi kilichobakia cha miaka mitano.

  Alikuwa akitoa taarifa ya Tanzania kwenye mkutano mkuu wa utekelezaji wa malengo hayo mjini New York, Marekani juzi jioni ambako anamwakilisha Rais Kikwete.

  Pinda alisema kwenye malengo ya elimu, uandikishaji wa watoto katika shule za msingi umefikia asilimia 95.4 Tanzania Bara na asilimia 81.5 Zanzibar na uwiano wa wanafunzi wa kiume na wa kike katika shule hizo uko sawa kwa sawa.

  Alisema ukuaji wa uchumi ni wastani wa asilimia saba kwa muongo mmoja uliopita na umasikini kwa wanaoishi chini ya dola moja kwa siku, umepungua kutoka asilimia 38.6 mwaka 1991/92 hadi asilimia 33.6 mwaka 2006/07.

  Kwa mujibu wa Pinda, kwa vile asilimia 80 ya Watanzania milioni 40 wanajishughulisha na kilimo, uwekezaji katika kilimo ndiyo utakaowaondoa katika umasikini na ndiyo maana Serikali imeanzisha azma ya Kilimo Kwanza ili kuendeleza kilimo cha kisasa na cha umwagiliaji.

  Kuhusu Ukimwi, alisema maambukizi mapya yamepungua kutoka asilimia saba 2003 hadi asilimia 5.7 mwaka huu kwa Tanznia Bara na Zanzibar imebaki asilimia 0.6 tu.

  Alisema malaria karibu imekwisha kabisa Zanzibar na kwa Bara mbinu mpya za kukabiliana na ugonjwa huo zinatekelezwa, alisema.

  Hata hivyo, alisema bado hatua kubwa haijapigwa nchini katika kupunguza vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi na vifo vya watoto wachanga.

  Mkutano wa New York unaohudhuriwa na wakuu wa Nchi na wa Serikali, wakiungana na viongozi wa taasisi za kijamii na sekta binafsi, unapima utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia tangu mwaka 2000 mpaka sasa kabla ya mwaka 2015 ambapo utekelezaji unatakiwa ufikie asilimia 100.


  Hiyo niliyo bold siielewi...naomba ufafanuzi
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee bwana
   
 3. u

  urasa JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  labda umepungua mpanda,umasikini utapunguaje wakati tupo chini ya mfumuko uliopindukia wa bei hadi ya mchicha
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sio uongo, umepungua kwake.
   
 5. A

  Andulile Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 5
  Umepungua kwake kwa sababu kodi zetu zinamhudumia yeye na familia yake. Lakini nje ya hapo, sioni kama haya anayosema ni ukweli. Ulimi ni kiungo kidogo lakini matatizo yake makubwa. Kwa maneno ya ulimi viongozi huwa tayari kusema hata yasiyo kweli, lakini ni kwa aslahi ya wenyewe.
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hawa watu sijui wanalewa madaraka?!! Hivi umaskini umepumgua kwa kigezo kipi?
   
Loading...