BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Pinda tumechoka na usanii. Fisadi Mkapa kama kiongozi wa CCM alijihusisha na ufisadi, Sumaye naye kama waziri mkuu alikuwamo kwenye ufisadi, Lowassa naye, Karamagi, Msabaha, Chenge, Mramba, Meghji, Rostam Aziz, Mkono, Mzindakaya wote hawa wamehusishwa na ufisadi kwa namna moja au nyingine. Na wote hakuna hata aliyeguswa na mkono wa sheria. Halafu unataka kuwaambia Watanzania wasiihusishe CCM na sirikali na ufisadi uliofanywa na hawa mafisadi wa CCM!
If you have nothing important to say it is better to keep quiet rather that issuing unintelligent statements
Pinda aikingia kifua CCM, Serikali
2008-05-03 09:15:09
Na Mwandishi Maalum
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema CCM na serikali yake visilaumiwe moja kwa moja kwa mapungufu ya mtu mmoja mmoja kwa sababu vyombo vyote hivyo viwili ni safi.
Alikuwa akizungumza eneo la Kihesa mjini Iringa jana wakati wa uzinduzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini na kutoa kadi kwa wanachama wapya 700.
Alisema tuhuma kuhusu rushwa na wizi ni kwa mtu mmoja mmoja ambaye atakuwa na mapungufu yake, lakini siyo kwamba ni sera ya Chama chao na Serikali yake.
``Chonde chonde, nihukumuni mimi Pinda kwa yale ninayokosea muondoeni Pinda kama ni tatizo lakini chama kiendelee na Serikali yake kwa vile ni utaratibu wa kujisafisha tu.
``Chama hiki (CCM) ni kizuri na serikali yake nzuri, kama kuna mapungufu basi yatashughulikiwa na hatua zitachukuliwa.``
Akijibu hoja katika risala ya tawi hilo kuhusu ajira kwa
wahitimu wapya na kupanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, alisema serikali itajitahidi kuhakikisha wahitimu hao wanatumika vizuri.
Alisema pia utaratibu wa mikopo haujapangika vizuri kwa kuwa lazima kwanza kuwajua wote wale wasiokuwa na uwezo wanaohitaji hasa mikopo hiyo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.
Alisema nafasi za vyuo vikuu lazima ziongezeke kwa vile usipofanya hivyo basi utakuwa na vijana wengi waliomaliza sekondari tu na hilo litakuwa tatizo kubwa zaidi.
Waziri Mkuu alizindua tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini katika shughuli iliyopangwa kutekelezwa muda mfupi kabla ya kurejea Dar es Salaam kutoka Iringa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa juzi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.
SOURCE: Nipashe