Pinda: Tuhukumuni sisi, kiacheni chama, Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Tuhukumuni sisi, kiacheni chama, Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 3, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280
  Pinda tumechoka na usanii. Fisadi Mkapa kama kiongozi wa CCM alijihusisha na ufisadi, Sumaye naye kama waziri mkuu alikuwamo kwenye ufisadi, Lowassa naye, Karamagi, Msabaha, Chenge, Mramba, Meghji, Rostam Aziz, Mkono, Mzindakaya wote hawa wamehusishwa na ufisadi kwa namna moja au nyingine. Na wote hakuna hata aliyeguswa na mkono wa sheria. Halafu unataka kuwaambia Watanzania wasiihusishe CCM na sirikali na ufisadi uliofanywa na hawa mafisadi wa CCM! :confused:
  If you have nothing important to say it is better to keep quiet rather that issuing unintelligent statements


  Pinda aikingia kifua CCM, Serikali

  2008-05-03 09:15:09
  Na Mwandishi Maalum

  Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema CCM na serikali yake visilaumiwe moja kwa moja kwa mapungufu ya mtu mmoja mmoja kwa sababu vyombo vyote hivyo viwili ni safi.

  Alikuwa akizungumza eneo la Kihesa mjini Iringa jana wakati wa uzinduzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini na kutoa kadi kwa wanachama wapya 700.

  Alisema tuhuma kuhusu rushwa na wizi ni kwa mtu mmoja mmoja ambaye atakuwa na mapungufu yake, lakini siyo kwamba ni sera ya Chama chao na Serikali yake.

  ``Chonde chonde, nihukumuni mimi Pinda kwa yale ninayokosea muondoeni Pinda kama ni tatizo lakini chama kiendelee na Serikali yake kwa vile ni utaratibu wa kujisafisha tu.

  ``Chama hiki (CCM) ni kizuri na serikali yake nzuri, kama kuna mapungufu basi yatashughulikiwa na hatua zitachukuliwa.``

  Akijibu hoja katika risala ya tawi hilo kuhusu ajira kwa
  wahitimu wapya na kupanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, alisema serikali itajitahidi kuhakikisha wahitimu hao wanatumika vizuri.

  Alisema pia utaratibu wa mikopo haujapangika vizuri kwa kuwa lazima kwanza kuwajua wote wale wasiokuwa na uwezo wanaohitaji hasa mikopo hiyo.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.

  Alisema nafasi za vyuo vikuu lazima ziongezeke kwa vile usipofanya hivyo basi utakuwa na vijana wengi waliomaliza sekondari tu na hilo litakuwa tatizo kubwa zaidi.

  Waziri Mkuu alizindua tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini katika shughuli iliyopangwa kutekelezwa muda mfupi kabla ya kurejea Dar es Salaam kutoka Iringa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa juzi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wasomi wetu bwana .Haya wacha wachukue na wiki ijayo waingie mitaani tena na kuja kuomba msaada JF .
   
 3. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Pinda is always talking too much even if there is nothing important to talk about, when you talk too much you dont have tym to think.. Pinda tumekuchoka Funga bakuli sisi si wajinga
   
 4. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pinda anajaribu kurudisha imani kwa watanzania, ila bado wanashindwa kutekeleza hata moja kati hayo wanayoyasema, sisi tutaendelea kutega masikio, Pinda just do any thing watanzania waamini usemacho.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Isayamwita Pinda na ukoo wake wa CCM hawako serious na hawana jpya wamegota soon wataanza mambi ki Mugabe then itakuwa issue sana .
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  PINDA naye mwoga tu bla bla tu hana lolote mbona anawaogopa MAFISADI wakubwa mbona wametajwa mm nilitegemea atasema watakamatwa na kuwekwa cello huku uchunguzi wa miezi 6 ukiendelea zaidi zaidi tunapigwa michango ya macho. KILICHO BAKIA KUIKOMBOA NCHI HII NI MM NA WEWE KUELIMISHA NDUGU ZETU KIPINDI CHA UCHAGUZI SI KUCHAGUA CHAMA CHA MAFISADI CCM KILA MTU NI FISADI TU HAKUNA MSAFI HUMO WACHAGUE UPINZANI WALETE MAENDELEO TUMECHOKA NA BLA BLA ZAO HIZI ZA KINA PINDA.
   
 7. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mie nshasema kabisa huyu ndio hafiki popote,, Waziri mkuu mwenye personality alikua sumaye bwana sijui waliomtangulia maana sikuwa experience sana,,,ila kwenye maswala ya vijisent sumaye nae kiboko
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Matumaini yote niliyokuwa nayo kuhusu Pinda sasa yametoweka, inaonekana kama Premiership sasa ina vacuum, anytime this PM of ours opens his mouth it is some kind of gibberish, sijui kama anajua kauli zake ni muhimu, au haoni uzito wa kiti na ofisi yake.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  watanzania bwana .yaani hata nyie hapa JF malikuwa na matumaini a Pinda ? Penda kawekwa na JK naJK si mfanyaji kweli Pinda mnategemea afanye nini ?
   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Pinda: Tuhukumuni sisi, kiacheni chama, Serikali
  na mwandishi maalumu, iringa

  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda,(pichani) amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali zake visilaumiwe moja kwa moja kutokana na upungufu wa mtu mmoja mmoja.

  Amesema chama hicho, na Serikali zake, ni visafi, hivyo makosa au tuhuma za mtu mmoja mmoja, zisichukuliwe kuwa ni tuhuma au makosa kwa vyombo hivyo.

  Pinda alikuwa akizungumza katika eneo la Kihesa mjini Iringa jana, wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini. Alikabidhi kadi kwa wanachama wapya 700.

  Alisema tuhuma kuhusu rushwa na wizi ni kwa mtu mmoja mmoja ambaye atakuwa na upungufu wake, lakini siyo kwamba ni sera ya chama na Serikali zake.

  "Chonde chonde, nihukumuni mimi Pinda kwa yale ninayokoseaÂ…Muondoeni Pinda kama ni tatizo, lakini chama kiendelee na Serikali zake kwa vile ni utaratibu wa kujisafisha tu.

  “Chama hiki (CCM) ni kizuri na serikali zake ni nzuri, kama kuna upungufu, basi utashughulikiwa na hatua zitachukuliwa," alisema.

  Akijibu hoja katika risala ya tawi hilo kuhusu ajira kwa wahitimu wapya na kupanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, Pinda alisema Serikali itajitahidi kuhakikisha wahitimu hao wanatumika vizuri.

  Alisema pia kwamba utaratibu wa mikopo haujapangika vizuri kwa kuwa lazima kwanza kuwajua wote wasiokuwa na uwezo wanaohitaji hasa mikopo hiyo.

  Hata hivyo, alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.

  Alisema nafasi za vyuo vikuu lazima ziongezeke kwa vile isipofanyika hivyo, kutakuwa na vijana wengi waliohitimu sekondari tu na hivyo hilo litakuwa tatizo kubwa zaidi.

  Waziri Mkuu alizindua tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini katika shughuli iliyopangwa kutekelezwa muda mfupi tu kabla ya kurejea Dar es Salaam.

  Alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa, juzi.


  source: http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=4746&section=kitaifa
   
 11. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tunakiukum chama kwa kushindwa kufanya maauzi kule butiama maamuzi ambayo watu waliyataraja na vilevile walitka yafanyike,,ila kwa kua ni wabinafs wakasindwa kuanya hivyo, so tunawahukum wao na hilo chama lao
   
 12. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ..i have to question this PM's state of mind!! kama hana vitu vya kuongea basi akae kimya!!...wahenga walisema samaki mmoja akioza.... well, it is then a fact kuwa CCM na serikali yake ni one entity. Rotten party!!Mugabe chaliii huko, next stop magogoni!!Suckers!!
   
 13. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ufisadi sio sera ya CCM sasa kama viongozi wachache ni mafisadi wahukumiwe hao na sio chama na serikali
   
 14. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hapana mkulu sie tunakihukum chama kwa kushindwa kutoa uamuzi kwa manufaa yetu na badala yake wanakua wanatafuta mbinu za kulindana kila siku sasa sie tumhukum Lowasa wakati CCM walishindwa kumfuta uanachama kule butiama,,serikali na taasisi zake kama polisi, PCCb na TISS wanashindwa kuwashugulikia kina chenge hadi watu wa nje ndio wanashughulikia udhalim kama ule,,hapana mzee mie nadhani wanastahili lawama, matusi na hukum
   
 15. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2008
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  This guy is a joke, du hata miezi mitatu haijakamilika!!They say if u cant beat them, join them!!Nothing is new yeah, new bottle with the same old wine!!
   
 16. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwi kwi kwi kwi kwi,,,,,najua baadae jioni atapitia JF so atajionea watu wanavyomtuhum
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Waambie hao Wadanganyika na Wazanzivinjari.

  Tumekuwa watoto wa chekechea, ukitupa mwanasesere mpya siku hiyo hatunywi uji wala hatusikii tukifinywa, japo hatujui na hatujamuuliza Mama kama huyu mwanasesere ana features mpya tofauti na mwanasesere wa zamani.

  Huyu Pinda, ni nini kingekufanya uwe na matumaini nae? Pinda kaibuliwa wapi huyu? Nani anamjua huyu mtu mpaka uwe na matumaini ?

  Tuanze kupima qualification za mtu kwa kuangalia background pia. Sio mapendekezo tu. Hata mwajiri anasoma barua za mapendekezo akisha maliza kupitia Resume. Nyakati za kuimbishwa nyimbo za 'Ali Mwinyi Ali Mwinyi NDIO NDIO NDIO' zimepita zamani. Unamjua mpaka useme NDIO NDIO NDIO?

  Siku nyingine wakituimbia 'Pita Pinda Pita Pinda' tujibu NANI NANI NANI, na sio NDIO NDIO NDIO!

  Tafadhali!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Inabidi sasa mheshimiwa asiwe anaongea bila kuwa na notes, kwa mtu aliye na akili hawezi kuelewa kauli yake. Ni sawa na mwizi akisema msinihukumu mimi, muuhukumu mkono wangu ndio ulioiba. Chama kinaundwa na watu, na serikali inaundwa na watu, how can he say serikali ni safi, serikali ambayo imetuibia mabilioni ya pesa? How can he say CCM ni safi wakati hizo hela zilizoibiwa waliewa wabunge kufanyia kampeni za uchaguzi?
  Labda watu wa Iringa siku hizi wamekuwa na matatizo, kama walielewa alichokuwa anasema itakuwa ajabu sana.
   
 19. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nimependa uchambuzi wako mkuu,,,salute!
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  He is turning comedian himself without knowing kwamba anajivua nguo kwa maneno yake .Wacha tumnyame mnyama
   
Loading...