PINDA: Singida NO 1. kwa UMASIKINIi Tanzania

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
900
Akiwa anajibu maswali Bungeni W/Mkuu amepinga kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara si masikini kama wengi wajuavyo bali kwa Takwimu zilizopo mikoa masikini kabisa ni
1.Singda
2.Dodoma
3.Kagera

  • Kilichonishangaza hizi takwimu ni harari?
  • za mwaka gani?
  • Je hata Mikoa ya Zenji ni tajiri kuzidi dodoma?
  • na kwa mkoa kama Dodoma ambao ni makao makuu ya serikari na ccm inamaanisha nini?
  • Kwenye uchaguzi kwa nini wanachagua ccm?
Mwenye majibu japo kidogo hapo juu anijuze
 
Si kawaida ya leaders wetu kuwa na takwimu sahihi kwa baadhi ya mambo nyeti ya kijamii, lakini kwenye PESA zipo takwimu sahihi japo huvurugwa.
 
Hivi kuna takwimu kweli? Na vigezo gani vinatumika ku-rank huu umasikini kati ya mikoa..
 
Mh,
Singida na lindi mh makubwa !
AU wachumi wanaangalia vitu gani
Ni Singida ipi aliizungumzia .Hebu linganisha wilaya ya Iramba na Bagamoyoa AU Morogoro vijijni! hali za watu makazi nk,afu tafakari wilaya zingine.
Afu SINGIDA VIJIJINI NA WMKOA KAMA WA LINDI,
SINGIDA IKO MBELE KWA MAENDELEO YA WATU.
 
Sina uhakika na credibility ya hizo statistics, lakini inawezekana kuna kaukweli manake ukiacha Kagera, Singida na Dodoma ndio nguzo kuu ya CCM, hii inamaanisha CCM=Umasikini, mark my words .
 
Wangefanya na tathmini walipata ushindi wa kishindo kwa kiasi gani.kweli sisiemu na umasikini ni sawa na pua na makamasi.huko wamelemewa kwa umasikini wa fikira mpaka kiuchumi.
 
Sina uhakika na credibility ya hizo statistics, lakini inawezekana kuna kaukweli manake ukiacha Kagera, Singida na Dodoma ndio nguzo kuu ya CCM, hii inamaanisha CCM=Umasikini, mark my words .

we tininti, Nahisi utajiri mwingi wa kagera unajulikana UGANDA. Maana kahawa, Ndizi na kwa sasa sukari ya Kagera yote upelekwa uganda kisha sukari ufungwa tena na pinda alijulishwa akasinyaa.
 
Mkuu TUNDU LISU Katokea wapi?

Sina uhakika na credibility ya hizo statistics, lakini inawezekana kuna kaukweli manake ukiacha Kagera, Singida na Dodoma ndio nguzo kuu ya CCM, hii inamaanisha CCM=Umasikini, mark my words .
 
Mnaosema maskini hawana akili inawezekana nyie ndiye hamnazo! Kuchagua chama zaidi ya CCM haimaanishi kuwa hawana akili. Ni chaguo lao. Ni tastes zao kama vile mtu anapoamua kuoa au kuolewa na mwenza mlemavu; mfano kipofu au kiziwi ili hali walijaariwa kila kitu wako kibao. Mafano unaweza kuwa si mzuri sana ila maana yake ni nzuri. Achana na fikra za kulazimisha mawazo yako yawe ndiyo ya wengine wote.
 
I will be the last to agree and believe that Kagera is amongst the poorest regions in Tanzania.
 
Naamini Singida si masikini kama ilivyo mikoa ya Kusini na Zanzibar .WiLAYA za mkoa wa pwani zina waakazi wengi masikini.
Hii ni kwa sababu nimeishi Singida kwa 20 yrs na Pwani na Dar ,kwa hiyo maendeleo hayahitaji darubini yanaonekana ndio maana hii maada ikawa hapa jf kwa sababu watu wameshangaa hii orodha.
 
Vigezo vinavyotumika kupima umasikini katika mikoa ni pamoja na; pato linalotokana na shughuli mbalimbali katika mkoa husika,mfano,mazao ya biashara,viwanda vidogovidogo na vikubwa,kiwango cha elimu kwa wakazi wa mkoa husika,wingi na ubora wa huduma mbali mbali za kijamii,ubora wa makazi ya wananchi,uhifadhi wa mazingira,uwepo wa vivutio mbalimbali vya utalii kuweza kuingiza mapato katika mkoa,uwepo wa rasilimali zinazoongeza kipato kwa mkoa husika,nk.

Hivyo inawezekana kabisa Ndugu Pinda akawa sahihi au la,maana wataalamu wetu siku hizi hawaaminiki tena.
 
Back
Top Bottom