Pinda & Shein becoming CCM Spinning Machine?

mwanatanu

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
854
127
Baada ya kusoma hili gazeti nina wasiwasi ya kuwa Mzee Pinda na Mkulu Shein (the only clean people in Chama Cha Makulaji)wanatumiwa ku spin ile scandal ya chenge wanatuletea EPA....ama kweli wajinga waliwao

WAKATI wananchi wakidhani kuwa serikali inaelekea kukata tamaa kuwashughulikia mafisadi wa EPA na Richmond, serikali imeamka na katika muda wa siku mbili, viongozi wake wakuu wametoa kauli zinazoonyesha kuwa sasa wameanza kuonyesha mwelekeo tofauti na wa awali.

Akizungumza na Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Fogh Rasmussen, Jumatano wiki hii, Dk. Shein alisema kuwa watu wote watakaoonekana kuwa walihusika katika ufisadi kwenye maeneo hayo mawili, watafikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Pili, Pinda alisema kuwa, fedha zinazorudishwa zitatumika kama ushahidi mahakamani, iwapo serikali itafungua kesi dhidi ya watu waliozikwapua kutoka katika akaunti hiyo.

“Ndiyo, hata akikataa tutamwambia lakini bwana we si ulikubali ukarudisha hizi?” alisema Pinda ambaye siku chache tu zilizopita baadhi ya magazeti (si Tanzania Daima) yalimkariri akisema kwamba wezi wa EPA ni watu wenye fedha nyingi, ambao wanaweza kuisumbua sana serikali iwapo watafikishwa mahakamani.

Kabla ya kutoa ufafanuzi huo, Pinda alisema kuwa watu wasifikiri kufungua kesi dhidi ya wezi wa EPA na kuiendesha kwa mafanikio ni suala rahisi.
 
jamani ebu google CORRUPTION INVOLVED JERSEY ISLAND ENGLAND halafu muone jinsi hiki kisiwa kilivyokubuu kwa kuweka pesa za wizi, please weka thread.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom