The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 14,924
- 12,218
Mafisadi sasa kiama
2008-07-18 10:02:58
Na Mashaka Mgeta, Dodoma
Serikali inaandaa muswada wa marekebisho ya sheria, ili kuongeza nguvu ya kudhibiti ufisadi unaoshamiri nchini.
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alisema hayo jana bungeni mjini hapa, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kishapu (CCM), Bw. Fred Mpendazoe, wakati wa maswali ya papo kwa hapo, kutoka kwa wabunge.
Bw. Mpendazoe, alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kuchukua hatua za dharura, kuipitia Katiba na sheria ili kuukabili ufisadi, kwa vile unaathiri ustawi wa jamii.
Mbunge huyo, aliuliza swali hilo, huku akirejea katika ibara ya 8(i)(b) inayoelezea lengo la serikali katika ustawi wa wananchi.
Bw. Pinda, alisema suala hilo linafanyiwa kazi, ambapo sheria husika zitapitiwa upya, ili kufikia maamuzi yatakayojenga na kuimarisha misingi ya utawala bora nchini.
Hata hivyo, Bw. Pinda, alisema kuwa na sheria nzuri haitoshi, bali kunahitajika ushiriki wa watu binafsi, hasa viongozi wa umma, kuwa waadilifu.
Alisema ufisadi siyo dhana inayowahusisha matajiri pekee, na kutoa mfano wa kuwepo taarifa za vitendo hivyo katika ngazi ya halmashauri za wilaya nchini.
Awali, Bw. Mpendazoe, alielezea kuwepo wimbi la wafanyabiashara, wanaotumia fedha kuingia katika siasa na baadaye katika uongozi wa serikali.
Bw. Mpendazoe, alikariri sehemu ya hotuba iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete, alipolihutubia Bunge Desemba 30, 2005 na kuzungumzia athari za uongozi unaopatikana kwa njia ya `kununuliwa`.
Pia, Bw. Mpendazoe, alitaka kujua ikiwa serikali ipo tayari kuleta mswada wa sheria ili kuliwezesha Bunge kuteua watendaji wakuu serikalini, ambao hivi sasa wanateuliwa na Rais.
Alisema ushiriki wa Bunge katika uteuzi huo, utakidhi ibara ya 4(2) ya Katiba na kazi ya Serikali ya Muungano na ya Zanzibar itakuwa utekelezaji, wakati Bunge na Baraza la Wawakilishi vitasimamia utekelezaji huo.
Aidha, Bw. Mpendazoe, alisema kwa kuwa Bunge linawajumuisha wawakilishi wa wananchi, kushiriki kwake katika uteuzi huo, kutakidhi ibara ya 8(i)(c) inayozungumzia serikali kuwajibika kwa wananchi.
Bw. Mpendazoe, alitaja baadhi ya watendaji wakuu wanaostahili kuteuliwa na Bunge kuwa ni Wakurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Usalama wa Taifa, Tume ya Haki za Binadamu, Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na mabalozi.
Akijibu swali hilo, Bw. Pinda, alisema mageuzi hayo yatafanyika ikiwa kutakuwa na mfumo wa kikatiba uliopo sasa.
Hata hivyo, Bw. Pinda alisema kuwa kwa mujibu wa Katiba, Rais ni sehemu ya Bunge, aliyepewa mamlaka ya kusimamia shughuli za Serikali ikiwemo uteuzi wa watendaji hao.
Alisema Bunge linajumuisha wabunge kwa upande mmoja na Rais kwa upande mwingine, hivyo fursa na wajibu wa chombo hicho (Bunge) ni kusimamia utekelezaji wa watendaji wanaoteuliwa na Rais.
Naye Mbunge wa Musoma Mjini (CCM), Vedastus Manyinyi, alitaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu madai ya fedha zilizotolewa, maarufu kama `mabilioni ya Kikwete`, kutowafikia walengwa.
Kwa mujibu wa Bw. Manyinyi, fedha hizo zilitolewa katika mpango wa Serikali, kupitia benki za CRDB na NMB, ziliwafikia matajiri na watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi badala ya wajasiriamali wadogo waliokuwa walengwa wake.
Akijibu swali hilo, Bw. Pinda, alisema serikali imewaagiza viongozi wa mikoa yote nchini, kuwasilisha taarifa yenye majina ya watu na kiasi walichokopa, ili yachapishwe kwenye kitabu maalum.
Bw. Pinda, alisema kitabu hicho kitasambazwa kwa wabunge ili kuwarahisishia kazi ya kubaini kasoro zilizojitokeza.
Aidha, Bw. Pinda, alisema kiasi cha fedha zilizotengwa katika mpango huo, kilikuwa kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi, hali inayoweza kuwa miongoni mwa sababu za kuibuka kwa malalamiko.
Pia, Bw. Pinda, alisema kuna changamoto inayoikabili Serikali, kuwawezesha wananchi wa Kihadzabe, kuishi kwa kufuata mabadiliko yanayotokea duniani.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Bw. Mgana Msindai, ambaye pamoja na mambo mengine, alitaka kujua mpango wa serikali kuwapelekea Wahadzabe mahitaji muhimu kama wataalamu wa masuala ya maendeleo.
SOURCE: Nipashe