Niliandika hapa kwamba moto kuhusu katiba mpya uliowashwa na CHADEMA hakuna wa kuuzima. Sasa ni kuendelea kuishinikiza Serikali kwamba hatutaki kuongeza viraka kwenye katiba mpya ambavyo vinavyoulizana mwenzangu umekuja lini, bali tunataka katiba mpya ambayo itaendana na hali halisi ya siasa za vyama vingi nchini na pia kuhakikisha katiba hiyo inapatikana kabla ya uchaguzi ujao 2015. Hongera sana CHADEMA juhudi zenu taratibu zinazaa matunda.
Mkuu,
Samahani sana mkuu kama kwa kauli yangu nitakuudhi lakini usifanye issue ya katiba mpya kama issue ya kichama, ni issue ya kila mlalahoi, ya kila mwananchi na kila chama isipokuwa CCM. CHADEMA kama Chadema pekee hawatofika mbali na issue hii.
Wala usiuchukulie ujumbe huu kuamini kuwa nina beef na chadema,, no,no..
Katiba mpya ni kwa manufaa ya umma, si kwa manufaa ya chama kama ilivyo sasa.Na kila anayeipendelea mema nchi hii awe-on board.