Pinda: Serikali kuunda jopo kuchunguza madai ya katiba mpya

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,356
Akizungumzia suala hili Mizengo Pinda amesema haja ipo ila bado haijaamua kama mabadiliko yanayoitajika ni makubwa au madogo

My Take
Katiba itawekewa viraka ambavyo havitatatua mahitaji ya wananchi
 
Uani hilo ndo tamko? Makubwa au madogo. ndo tamko la serikali kuhusu katiba??
 
Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.

Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.

Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.

Source-Mimi
 
Ndio kaka Mizengo Pinda akizungumzia issue ya katiba leo amesema kuwa ni kweli kuna umuhimu wa katiba mpya ila serikali itakaa na wadau na kujadili kama madadiliko ya hiyo katiba yanayoitajika ni makubwa au madogo
 
anakaa na wadau lini maana wasije vuta mpaka 2015 ndiyo waanze mchakato....
 
Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.

Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.

Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.

Source-Mimi

Makes sense!
 
Hiyo bado ni longolongo. Labda kwa vile msemaji ni mtu harmless (mtoto wa mkulima). Serikali inachotakiwa kufanya ni kuita wadau wote kukubaliana utaratibu sahihi wa kuandika na kupitisha katiba mpya. Hilo la makubwa na madogo ni letu sisi wananchi, watuachie; sio kazi ya serikali.
 
Akizungumzia suala hili Mizengo Pinda amesema haja ipo ila bado haijaamua kama mabadiliko yanayoitajika ni makubwa au madogo

My Take
Katiba itawekewa viraka ambavyo havitatatua mahitaji ya wananchi

Pinda naye kapunduliwa tu hana lolote huyo. Wananchi tunataka katiba mpya siyo mabadiliko makubwa au madogo. Kama vitakuwepo vitu vinavyofaa katika katiba ya sasa tutavichukua.
 
Mkuu kumbuka hapa:
"Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi."

Hivyo bado kuna tatizo hapa
 
Ningemshauri mtoto wa mkulima chague tume iliyohuru kukusanya data za kama kunaulazima wa Kuwepo kwa marekebisho makubwa ya Katiba na quetionnaire zitokana na watu wenye uelewa wa mahitaji ya katiba mpya siyo waende kijijini kwa bibi zetu wengi wao hawana uelewa juu ya hilo.
Angalizo; watouch vitu muhimu vinavyoleta misigano makini na nyeti ambayo inamizengwe ktk Katiba chakavu ya sasa.
MUNGI IBARIKI TANZANIA.
 
Baada ya kilio cha muda mrefu cha madai ya Katiba, hatimae hii leo serikali ya Tanzania imekiri kuwa ipo haja ya kuifanyia mabadiliko Katiba ya sasa ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya sasa.

Akiongea na wahariri wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali itaunda jopo la wataalam kupitia mapendekezo ya awali na ya sasa yaliyotolewa kuhusiana na mabadiliko ya Katiba.

Hata hivyo Mh. Pinda amesema serikali bado haina jibu iwapo yafanyike mabadiliko makubwa ama mabadiliko madogo kutokana na mapendekezo yaliyokwishatolewa, au suala hilo lipelekwe bungeni ama lirudishwe kwa wananchi kwa maamuzi.

Source-Mimi
Sasa yule aliyekurupuka na kusema serikali kwa sasa fedha za kufanya mabadiliko alisema kwa niaba ya nani? ya kwake au ya serikali? kwa maana maelezo yake yalimaanisha hakuna kitu kama hicho kitaendelea, na kwa maelezo haya ina maana serikali is indecisive, na huyu hajatamka kama ana preempt yale maelezo ya awali.

Hii inaonekana kuwa danganya toto. Mtakumbuka wakati wa Mkapa serikali ilizima wimbi la kudai katiba mpya kwa kuleta "white paper", na hatimaye bunge likapitisha marekebisho ya katiba ambayo badala ya kupunguza madaraka ya rais yaliyokuwa yakinungunikiwa, yaliongezwa; kwa mfano kwa kumpa madaraka ya kuteua wabunge kumi. Hivyo, safari tusidanganyika, kinachotakiwa ni kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya, na wala siyo kuiwekea viraka hii katiba tuliyonayo.
 
Back
Top Bottom