Pinda; Safisha Maswa, rushwa hadi ofisi za chama - Shibuda

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
MBUNGE wa Maswa, John Shibuda, amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kufanya ziara wilayani humo, ili kuisafisha kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa kama alivyofanya katika Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.

Shibuda aliitoa kauli hiyo jana katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo wakati akibainisha kero zinazowasumbua wananchi wa wilaya hiyo.

Alisema wananchi wamekuwa wakidhulumiwa kupata haki zao kutokana na kuombwa rushwa na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo pindi wanapotaka kupata huduma mbalimbali katika ofisi za serikali.

“Wananchi katika Wilaya ya Maswa wamekuwa wakilalamika kila mara kupata huduma katika ofisi za serikali mpaka watoe rushwa, jambo hili ndilo linalowafanya wananchi waichukie serikali ya CCM jambo ambalo linawafanya kukata tamaa hata kuchangia shughuli za maendeleo,” alisema.

Mbunge huyo alisema kama Waziri Mkuu aliweza kuisafisha Wilaya ya Bagamoyo ni vizuri akafika wilayani humo kwa ajili ya kuondoa uozo huo ambao umekuwa ukikithiri licha ya kuwepo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nitumie fursa hii hasa kupitia vyombo vya habari kumuomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuja wilayani Maswa kujionea utalii wa dhuluma unaofanywa na viongozi wa serikali katika kuwahudumia wananchi wanaofika kupatiwa huduma,” alisema.

Alisema viongozi wa wilaya hiyo wanashindwa kupiga vita vitendo hivyo kutokana na wao kujihusisha kupitia madalali wao kwa lengo la kujipatia utajiri wa haraka.
 
Kumradhi ni maswa badala ya mara
radhi iwaendee wanamara wote
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom