Pinda: Pamoja na matatizo ya umeme lakini uchumi wetu haujatetereka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Pamoja na matatizo ya umeme lakini uchumi wetu haujatetereka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndibalema, Mar 2, 2011.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nimeshangazwa na kauli ya Waziri mkuu Mizengo Pinda kuwa "pamoja na matatizo ya umeme nchini lakini uchumi wa Tanzania haujatetereka hata kidogo...na ndio maana hata viongozi hawatetemeki kuelezea uimara huo wa uchumi.."

  Mimi simwelewi Waziri mkuu wangu.
  nashindwa kumwelewa jamani, naomba wanaJF mnisaidie huu uchumi ulio imara ni uchumi upi?
  Au miye sijui mambo ya uchumi kwa sababu sio fani yangu?
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona wanashindwa kuwalipa mishahara watumishi wa umma??
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umemsahau yule waziri wa habari wa iliyokuwa serikali ya Iraq WAKATI ULE?......Wakati wamarekani wanamwaga mabomu kama mvua mitaa ya Baghadad, jamaa anaripoti kuwa.."we havent spotted any American Soldier in Baghdad, and any who will approach, his grave will be right here in Baghdad..."..Hizo ni Propaganda za wanasiasa, ambazo kawaida huwa ni kinyume na ukweli....Kiwanda chochote kikisimama abnormally kwa masaa 6 tu, tayari ni hasara kubwa!...Kama viwanda vinaripoti hasara kila siku, uchumi huo wa taifa unaopanda unahesabiwa kutokana na nini?...si ni aggregate ya production za viwanda anuwai?...achana na MWONGO MKUU HUYO!
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha mbali sana.! Kweli watawala wetu wa leo wako kama Mohamed al Sahaf wa Iraq. N-way, dhamiri zao zinawasuta! Hawasemi kama industrial products zetu zimeongezeka au la! Je exports zetu katika kipindi hiki cha mgao wa umeme na ukame zina status ipi? Very sad!
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Kama alidanganya bunge utegemee nini zaidi. Nina mfano halisi: Mwezi wa 12 nilinunua betri ya national Special kwa Tzs.350/= Lakini mwezi huu nimenunua kwa Tzs.700/=. Kama cost of sales ni kubwa namna hiyo how can u compete with other products from other states. Uchumi kuimalika tuna export zaidi ya importation? Jina hili ni baya "PINDA".
   
 6. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  :A S 13::A S 13:Wamelewa madaraka na huduma za bure kila saa.....mwenzetu hajui hata bei ya sukari wala chumvi,gari halipii mafuta wala nini,atajuaje shida zetu??? Dr Slaa akisema wanamuona mchochezi na mwenye nia ya kuharibu usalama.....hawatuelewi jamani....tuchukue hatua....mwenzake Lowassa juzi kasema iundwe tume ya kushughulikia mfumuko wa bei na matatizo ya kiuchumi yeye haoni lolote.......
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Haja ainisha uchumi upi ana zungumzia. Kama ni uchumi wa Tanzania au la. Ingefaa aulizwe. Yawezekana ana ongelea uchumi wa baadhi ya watu maana hata Marekani kuna baadhi ya Wall Street companies zili tajirika kwa kubet against the economy. Kwa hiyo hata hapa nchini kwetu kuna uchumi wa baadhi ya watu una tegemea uchumi wa jumla wa taifa kuwa mbovu.
   
 8. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Siyo lazima kaka uwe MCHUMI kujua uchumi... tena WA NCHI UNAYOISHI , uko imara au magumashi. Pinda naye kesha haribikiwa.
   
 9. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye nyekundu Michelle naona umepotoka na unashindwa kuona alama za ukutani... Kwa kipindi hiki cha 2010-2015 LOWASA NI WA KUPUUZWA KWA KILA KITU AISEE.
   
 10. bona

  bona JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  mwenye shida hajui mwenye njaa! haya ndio ya mfalme yule wa ufaransa enzi izo aliyepinduliwa na kuuawa mitaani na wanachi wenye hasira kali na njaa wakati wanaandamana wako nje ya palace lake juu gorofani yeye yuko juu wanawashangaa alipouliza walinzi na watumishi wake kua wanashida gani akajibiwa eti wanaandamana hawana mikate ya kula mkewe akawatuma watumishi eti kama mikate hamna si wale keki!
   
 11. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Anakuwa mtoto wa mkulima hata kichwani!!! Hii balaaa. Kama kwa hali hii inayokumba sasa wananchi bado uchumi haujatetereka, basi inabidi nirudi darasani kujifunza tena maana ya neno uchumi.
   
 12. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri wanaJF wakamjulisha Mhe. Pinda, Waziri Mkuu wetu kuwa uchumi wetu kwa vyovyote ni lazima unaathirika na kutetereka, kutokana na kutopatikana kwa nishati muhimu kama umeme. Mgao wa umeme unaoendelea sasa matokeo yake ni viwanda kadhaa vinafungwa. Kutozalisha bidhaa wakati huo sio tu mwenye kiwanda hapati pato, bali wafanyakazi wanakosa ajira.

  Kupunguka kwa bidhaa sokoni sio tu kutalazimisha bei kupanda, bali watumiaji na walaji wengine watazikosa na kuathirika. Mfumko wa bei ndiyo matokeo: yaani uchumi utatetereka.

  Kama hospitali imekatiwa umeme kutokana na mgao, huduma ya upasuaji haiwezi kutolewa na wagonjwa wanaathirika. Wagonjwa wakiongezeka uchumi utatetereka.

  Chuoni kusipokuwa na umeme, wanafunzi na wahadhiri wao hawawezi kusoma! Hata kama wazazi wamekwisha lipia ada watoto wao, itakuwa mafunzo hayaendi inavyotakikana.

  Huku nyumbani kwetu tunapokosa umeme, mapishi hayaendi vizuri na inakuwa ni lazima kuni au mkaa utumike. Vitu viaendelea shagala bagala. Matumizi ya mkaa na kuni badala ya umeme yanapunguza uoto asilia kwa miti kukwatwa, na mazingira kuathirika. In the long term, uchumi unatetereka.

  Ofisini kwa wakubwa wenye kukaa maghorofani, kama mawaziri wanaomsaidia Waziri Mkuu na Rais, lifti hazifanyi kazi. Wanaathirika na wanachelewesha kutekeleza majukumu yao. Uchumi unaathirika.

  Nadhani Waziri Mkuu wetu alighafilika kidogo alipotamka eti uchumi haujatetereka. Tumwonee huruma. Kijana wa mkulima, amezidiwa mzigo.
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Jinga kabisa, sasa tumwamini nani sasa, bosi wake juzi anasema uchumi wetu unaathiriwa kiurahisi sana na matatizo madogo madogo wewe unatuambia pamoja na hayo bado uchumi uko bomba, pambaf
   
 14. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Masikini, wameshamchakachua baba wa watu kisiasa..!!! Yaani anaanza kuwa kama kina M....ambao alipokuwa waziri wa fedha aliwahi kuongea hadharani kuwa mgao wa umeme na ukame havijaathiri uchumi..!! Hawa viongozi waache kukurupuka, wawe wanatumia wataalamu ambao hawajachakachuliwa na wanasiasa, ili wawape facts na sio propaganda.

  Kuna vitu mtu unapaswa kuvifikira hata kama huna utaalamu, wewe mgao wa umeme unasema haujateteresha uchumi; wanajua maana ya kutetereka kwa uchumi..?? Muuza kuku au perishables anakula hasara kila siku kwa kutupa bidhaa kisa zimeharibika baada ya kukosa umeme..!!! Anafikiria multiplier effect ya simple problem kama hii ya huyu mfanyabiashara...?? Wafanyabiashara wanatumia nishati mbadala kuzalisha bidhaa zao badala ya umeme wa Tanesco, then anategemea cost of living iwe the same..?? Au anafikiri uchumi kutetereka ni kwa wao kukosa per-diem au sitting allowances..?? Uchumi una aspects au parameters nyingi more than one can think..!!

  Kuna kiongozi mwenzake naye nasikia aliwahi kusema kuwa uchumi wa Tz umekua kwa kuangalia foleni barabarani na kudai kuwa wananchi wengi wana magari siku hz..!! Hajiulizi kuwa uchumi unatetereka kwa kukosa miundo mbinu bora (barabara) ambazo zinarandana na kuongezeka kwa mahitaji ya kijamii ambapo siku hizi gari limegeuka kuwa basic need kutokana na uozo kwenye sekta ya public transport....??? Hajiulizi kati ya hayo ni magari mangapi ni ya makampuni..? Hajiulizi income gap inayoitesa Tz ambapo kuna watu hata nauli ya commuter bus kwa trip moja inawapa shida..!!

  Nafikiri viongozi wetu waanze kupewa shule ya uchumi na public speech..!! Wawe wanajua kuwa wenzetu, viongozi wao huwa wanaongea kitu baada ya vichwa kadhaa katika sekta husika kukaa na kumshauri. Na hivyo vichwa vikigundulika vimem-mislead kiongozi wa serikali hasa Rais, then vinaipata joto ya jiwe. Hapa kwetu; nina mashaka kidogo..!! Si ajabu kuna watu wanawadanganya hawa viongozi kwa kiwango cha juu baada ya kugundua kuwa viongozi wenyewe wanawaamini sana na pia hawana muda wa kuchuja wanayopewa..!!
   
 15. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Nchi hii kila kiongozi anaongea lake
   
 16. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Haijalishi kama ni waziri mkuu au la mwingine yeyote kusema uchumi wetu haujatetereka! Mtu anayetoa kauli hiyo ni mpumbavu kuliko tunavyodhani, ww pinda una uhakika wa mshahara wako na marupurupu umeme ukikatika wanakuwashia jenereta on the spot, mimi ninategemea umeme lets say ni kinyozi au nina machine zangu za kusaga na kukoboa, umeme unapokuwa wa mgao bado sijatetereka? Lets say nilichukua credit kupata machines zangu, at the end napopeleka marejesho nikiwaambia nashindwa kurejesha ipasavyo maana umeme wa mgao watanielewa? Nashindwa kuelewa umekaa madarakani zaidi ya miongo mitatu lakini mpaka leo unatoa kauli za kipumbavu, maskini tz! Ungekuwa nchi za watu makini ungeshafukuzwa kazi mda mrefu mf albino issue, umesema uongo bungeni! Na sasa unatudanganya hadharani! Bora yako umezaliwa tz na si ulaya (au nchi zilizoendelea) kweli tz tuna viongozi useless!
   
 17. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ifike mahali tuanze kutembea na mawe mifukoni... kiongozi akitoa upupu wa hivyo anafurumushwa kwa mawe.. Yaani viwanda 50+ vimesitisha uzalishaji, hatujagusa biashara na shughuli nyingine zinazotegemea umeme, yeye bado hajui kama kuna effects mbaya mno kwenye uchumi???
   
 18. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Maskini Pindaaa naye ameshakuwa contaminated na boss wake jk!!! very sad!
   
 19. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Kwa hapa kwetu, kiongozi akishasiba tu anaweza kuongea kitu chochote kwani ni tumbo ndilo linalomwongoza kusema na si kichwa. Kina Pinda wakishatoka majumbani kwao wmeshiba wanadhani wanajua kila kitu. Uchumi kwangu unakuwa imara pale bidhaa za chakula zinapoweza kufikika kwa unafuu kwa kila mtu na wala si kwa sababu kikundi cha watawala wacache kinakula na kuanza kutuonesha matumbo
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Watanzania tunalishwa uongo kila leo na tunaridhika, hakuna mtu wa kuuliza huo uchumi haukutetereka kwa kiasi gani???????? Kwa data zipi zinazo onyesha kukua au kutokutetereka kwa uchumi!!! Economical indicators zipi maana vyanzo vyote vya mapato viko effected kwa ukosefu wa umeme, sasa wewe waziri mkuu unasema uchumi uko stable haujawa effected unafikiria kweli au kivipi???????? Hao ndio viongozi wetu wa SISIEM.
   
Loading...