Pinda: Nitazungumza baada ya sikukuu

Salam JF...
Hivi wanaoshabikia Pinda ajiuzulu ni kwa ajili ya nini hasa, utendaji mbovu au kutokuwajibika ipasavyo au ni kufuata mkumbo na maslahi binafsi?
Lowasa alijiuzulu, kipi hasa kilichobadilika. Je mikataba dhalimu ilifutwa?
Je gharama za kujiuzulu Pinda ni ndogo kuliko kuendelea na wadhifa wake...kumhudumia PM aliyeng'atuka.
Je atakuja PM yupi ambaye hana au hatakuwa na mawaa?
Tuache ushabiki na tutafakari kwa kina, huenda tukalikomboa Taifa letu Tanzania.
 
Ni kweli wengi wetu tunashauri Pinda ajiuzulu,lkn pia tunashindwa kutafakari gharama za yeye kuachia hayo madaraka.....kama alivyosema mchangiaji mmoja kuwa tayari Serikali hii ina waziri Mkuu mstaafu sada ikitokea na Pinda naye anaachia hiyo nafasi basi ni aibu kwa hii Serikali,binafsi nadhani Pinda anataka kweli kuachia hayo madaraka kutokana na vigingi anavyokutana navyo anapotaka kufanya kazi yake,lkn kuachia madaraka ya uwaziri Mkuu si jambo dogo na rahisi hasa kama Mh Rais hayupo tayari kukubali hilo jambo.
Pinda amekuwa akiongea kiutu uzima akionyesha kutoridhishwa na wateule wa Rais,lkn afanye nini? tukumbukeni ishu ya Jairo,Pinda alitamani sana kumuondoa yule jamaa madarakani lkn akaishia kulalama tu maana anajua ni mteule wa Rais,sasa hata hili la operation tokomeza majangili naamini angetanani kuwatoa kina Said Mwema na wenzake waliokuwa wanasimamia hiyo zoezi,lkn angeanzia wapi......ni mpk Rais apende......Pamoja na udhaifu wa Pinda lkn udhaifu na uswahiba wa aliye juu na wateule wake unatesa sana,Pinda hataondoka kuficha aibu ya JK,udhaifu Pinda ndio umaarufu wa JK.

Umenena kama ambavyo amepata kunisimulia mwanataaluma mmoja. Tusikurupuke, tusome na kuuelewa mfumo wa ufanyaji kazi katika serikali ili tujue wajibu na haki zetu pamoja na za viongozi wetu...nani anawajibika kwa nani na kwa jambo lipi.
 
Kwa nini usijiuzulu tu tujue moja??viongozi wa kiafrika mbona mnapenda sana kun'gang'ania madaraka??kwanini usitoke hapo madarakani ukabaki kuheshimiwa??huoni kuwa wewe pinda ndio chanzo cha mambo yote yaliyotokea bungeni?????????Nenda mwalimu

Unakataa utumwa na ukoloni mamboleo lakini unakumbatia ukoloni....kila jamii inayonamna ya kuishi, ndio maana najivuna kuwa Mwafrika kama ambavyo mzungu anajivuna kuwa Mzungu na zaidi anajitahidi watu wote ulimwenguni wawe Kama Wazungu.
Mfumo wetu wa kiafrika hauna msamiati wa kujiuzulu ila kufa kishujaa ukiwa madarakani...
Unataka ajiuzulu ili nani aweze kutekeleza Majukumu ya PM kwa ufanisi?
 
Pinda alituambia amechoka; aondoke haraka kwa sababu hamsaidii Rais. Ameacha hadi Rais Anapata shinikizo la kufukuza mawaziri wake!
Kwa kauli yake wapigwe tu amesababisha maafa kwa wananchi kwenye tokomeza
Hata sisi wananchi tumemchoka
 
Hivi alisema atatoa tamko rasmi ni baada ya sikukuu ya christmas au na mwaka mpya au tumsubirie tu mpaka atoke nyumbani kwa wazazi wake hata kama ni mwezi?
Kweli zogo lote la mawaziri wote hao kuondolewa limetokana na usimamizi wake mbovu,maana yeye ndio msimamizi wa mawaziri wote,angetakiwa kuona ubovu uko wapi na kuwaajibisha,sio mpaka bunge iunde kamati.na kufanya kazi yake,
Hivyo hakuna sababu ya kuwa na waziri mkuu kama bunge inaweza kufanya hiyo kazi,ni aibu kama mpaka raisi afanye kazi yake au bubge,kwa maono yangu, mimi naona asisubiri mpaka mwaka mpya,atoe tamko la kujiuzulu mapema iwezekanavyo bila kutoa hata chozi,bcozi yeye ndio mzigo mzito zaidi kuliko hao wengine,mimi nasema,haraka ondoka usisubiri kuondolewa
HERI YA CHRITMAS wana JAMVI
 
sijawahi kuona waziri mkuu dhaifu kama pinda,sijui anasubiri nini kutoka madarakani,waziri muu mzigo huyu,au wadau mnasemaje??
 
Back
Top Bottom