Pinda: Nikila rushwa Mungu aniue!

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Alisema anataka kufanana na kiongozi wa kimila wa Kimasai aitwaye 'Laigwanan' ambaye kwenye kiapo chake wakati wa kupewa wadhifa huo huapa kuwa "Nikikiuka niliyoapa kuyatenda Mungu nilaani, niadhibu na ikibidi nichukue mapema," Bw. Pinda alisema.

Bw. Pinda alisema atakuwa kiongozi wa aina ya Laigwanan na kuwataka wasaidizi wake nao kuiga mfano wa 'Laigwanan.'
 
Pengine Yale Maombi Ya Watanzania Yameanza Kusikilizwa Na Mungu Maana Kama Kweli Hatokula Akiwa Kama Kinara Wa Viongozi Wa Serikali, Basi Tutegemee Tanzania Kuwa Nyuu Yoku Ndani Ya Mwaka Huu. Maana Masikini Wa Mungu Pesa Za Watanzania Huishia Mifukoni Mwa Walafi Fisadi Sasa Kama Huyu Akisema No Basi Watu Wote Wataogopa Na Mambo Yatakuwa Dangachee Na Hapo Labda Ninaweza Kufikiri Kurudi Home, Maana Nilishapasusa. Kuja Kuwapa Wajasiri Ya Mali Wenzangu Mawazo Mapya Ya Ni Jinsi Gani Ya Kutoka.
 
asipokula Yeye Kuna Malowassa Wengi Tu Wamebaki Serikalinikwa Hiyo Atabaki Na Maisha Yake Uku Watu Wanakula Pesa Swala Wajisafishe Toka Chini,,ufisadi Uko Kuanzia Kata
gday
 
Lakini Mimi Nina Imani Inaweza Kusaidia Maana Alipokuwepo Mamvi Ilikuwa Mtu Ukitoa Rushwa Kidogo Unaambiwa Hii Haitoshi Maana Mzee Mwenyewe Yumo Ndani Kwa Hiyo Itabidi Uongeze Dau
 
Kwa Hiyo Hao Viongozi Wa Serikalini Wakawaambukiza Mpaka Polisi Yaani Ukifika Polisi Kama Una Matatizo Wenyewe Wanakuambia Kabisa Waziwazi Kuwa Kiwango Unachotoa Inabidi Uongeze Maana Ni Lazima Wampatie Na Mkubwa Yaani Bosi Wao. Mpaka Ikawa Ni Halali. Lakini Kama Bosi Angekuwa Anaogopewa Kwa Kutokuchukuwa Rushwa, Na Hawa Wadogo Wangekuwa Na Uoga Na Nidhamu Ingekuwepo Jamani Si Mnakumbuka Enzi Za Akina Zombe Na Mahita Na Akina Chico Yaani Ni Aibu
 
Nimeona picha ya MP akipokea sakrament, hakika alisali sala ya toba ndo maana akapata nguvu mpya yakutamka haya. EL niliona akiwekewa mikono tu sina imani kama yule askofu alimbariki au alimlaani! kwani baada ya hapo nyota yake ilianza kufubaa na badae kuzimika.

MP yuko ziara ya kikazi siku 9 rukwa! msafara huu utatumia posho, disel, chakula kiasi gani? sidhani kama kunashughuli rukwa za kukagua siku 9! labda yuko likizo!

safari za mawaziri kumkimbiza zitto ziligharimu posho 149,000,000/= tunahitaji sasa viongozi walio na "cost sensitive workplan".
 
Jamani Si Ni Lazima Akapate Kisusio Na Tambiko Kidogo Si Nasikia Ndo Kwao,"jamani Wadhifa Huu Ni Mkubwa" Lakini Hata Hivyo Kuna Jamaa Alinidokeza Tu Kwamba Siyo Mtu Wa Kupenda Mapene Sana, Yaani Yeye Na Rais Wetu Ni Ngoma Droo. Jamani Si Mnajua Kabisa Kuwa Rais Wetu Si Mpenda Mapene? Yeye Ni Demu Na Kusafiri Tu Kwa Hiyo Nina Imani Mambo Yatakwenda Biyee
 
Du! mimi nadhani hicho kiapo chake akirefushe kidogo isomeke au ieleweke akijihusisha na ufisadi Mungu amuue, Rushwa kwa nafasi aliyo nayo hapelekewi kama polisi wa trafiki wanavyopewa na makonda wa daladala!!!!!!!!!
 
hii itakuwa bomba sana.Mie naomba ikiwezekana amshauri Rais AMng;oe huyu mjamaa Gray Mgonja amabye anadhani Serikali ni mali yake
 
Hope tumepata mtu "sampuli" sample ya SOKOINE!!!!
THE ONE FOR TANZANIANS!!!!!
 
mh! teh teh teh, wanamaneno hawa jamaa,utahadhani kweli vile, nilivyokwisha wazoea lazima awe na sifa hizi kuwa kiongozi wa ccm, kulindana, kuficha ukweli,kuogopa ukweli,na unafiki.......kama ni mkweli atujibu yeye maana mh jk kashindwa kumrudisha balali,yeye asituletee balali ila amtaje anayezuia ballali asirudishwe na hatua za sheria zichukuliwe, pili aseme tu kwanini wezi wa BOT WANARUDISHA PESA LAKINI HAWAKAMATWI,AMTAJE NANI ANAZUIA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE. MH PINDA ,USIJE UKATUPA GHARAMA ZA MAZISHI KAMA UKISHINDWA KUJIZUIA VISHAWISHI ,MAANA SERIKALI YAKO BADO MAFISADI WAPO, MFANO HAI NI HUU,EL KAPOKELEWA KAMA SHUJAA, MWAKYEMBE ANAAMBIWA NI FITNA, NA MAPOKEZI YAKE KUMEJAA MIZENGWE. Rais keshatamka el ni shujaa, hajampa sifa hiyo dr makyembe.
by Utajiju

seff mpitanjia
 
Alisema anataka kufanana na kiongozi wa kimila wa Kimasai aitwaye 'Laigwanan' ambaye kwenye kiapo chake wakati wa kupewa wadhifa huo huapa kuwa "Nikikiuka niliyoapa kuyatenda Mungu nilaani, niadhibu na ikibidi nichukue mapema," Bw. Pinda alisema.

Bw. Pinda alisema atakuwa kiongozi wa aina ya Laigwanan na kuwataka wasaidizi wake nao kuiga mfano wa 'Laigwanan.'

haya bwana, ngoja tusubiri vitu vya Laigwanan
 
Hii Kazi Ya Kumaliza Rushwa Ni Ngumu Sana Lakini Naona Pia Inaweza Kuwa Rahisi Kabisa Iwapo Tu Hawa Wahusika Watakuwa Siyo Wanafiki Kwa Kuwapa Adhabu Za Ukweli Hawa Wahusika Kama Vile Kuwafunga Jela Na Kadhalika. Kwa Mfano Mwanya Mzuri Ambao Wangeanza Kuutumia Ni Kwa Hawa Wanaorudisha Hizi Pesa Za Bot. Kwa Kuwa Kitendo Tu Cha Kurudisha Pesa Tayari Ni Ushahidi Wa Kuwa Waliiba, Sasa Hapa Sijui Pinda Anataka Kutuambia Nini? Au Labda Hajajua Maana Ya Kuwa Waziri Mkuu Ni Nini? "tusubiri Tuone"
 
Alisema anataka kufanana na kiongozi wa kimila wa Kimasai aitwaye 'Laigwanan' ambaye kwenye kiapo chake wakati wa kupewa wadhifa huo huapa kuwa "Nikikiuka niliyoapa kuyatenda Mungu nilaani, niadhibu na ikibidi nichukue mapema," Bw. Pinda alisema.

Bw. Pinda alisema atakuwa kiongozi wa aina ya Laigwanan na kuwataka wasaidizi wake nao kuiga mfano wa 'Laigwanan.'

Rushwa ni nini???

Ni kweli anaweza asile Rushwa hata kidogo na pengine kuiepa kwa nguzvu zake zote na kweli akanusurika katika mauti aliyoyaomba mwenyewe.
Lakini Pinda huyu huyu anaweza kuwa Mtazamaji, msindikizaji wa macho na mla jiwe mkubwa akiona viongozi wanakula rushwa na kfanya ufisadi wa kila aina.
Pinda huyu huyu anaweza kuwa ni mwepesi kupokea zawadi nuyingi na mialiko ya kukata kwa mundu kutoka kwa mafisadi.
Pinda huyu huyu anaweza asile mlungula lakini akawa akicheka na kima hawa wa kifiasdi mpaka jino la mwisho wakati mtama wetu unateketea shambani.
Nina imani Pinda utafuata uliyosema.
 
Nimependezwa na iyo kauli.Inatia moyo atleast watu wataiba lakini kwa woga unlike in the past where ukiiba unaambiwa mbona kidogo ebu kazia zaidi.

Nitafurai zaidi kama akianza deal na hawa ambao wako kwa system right now awatie Jamba jamba.

Pinda play your part it can be done,nasikia kwao wanamwita mzee wa kujinyima so I hope atalizungusha vyema gurudumu letu la maendeleo.

Mungu ibariki Tz,na viongozi wake na uwalinde na kuwaongoza ktk hii vita ya ufisadi nasi tupate angalau kufaidi rasilimali za Tifa letu.
 
hii itakuwa bomba sana.Mie naomba ikiwezekana amshauri Rais AMng;oe huyu mjamaa Gray Mgonja amabye anadhani Serikali ni mali yake





Aachane na hiyo kitu,kwani ni uongo na yeye anajua kua ni uongo kkwani Sir God kwa nyakati hizi hawezi kufanya hayo,hata akiongopa na kuapa hivyo atamwacha ila huko juu ndio watakapoa onana na nina uhakika atamwua kwa mara ya pili.
Mfano kuna Sheikh mmoja hapa Bongo DASLAM mjini maarufu sana kwa kutabiri na kusoma quraan,yy anasema "mgoja ajipe raha hapa hapa duniani kwani huko kwa bwana Mungu adhabu yake anaijua ni kichapo tu au kugeuzwa kuni za kuunguzia wengine" ila pepo yake ni hapa hapa duniani na hata ruhusu mtu kumwingila na ataipata kwa cost yoyote.na huyu bwana anasikia yupo kwenye system siku nyingi sasa yy na bwana Pinda si ndo wale wale\?
 
hayo ni ya Pinda, nami naamini ana dhamira njema, ila wale makatibu wakuu ktk mawizara atawafanye kwani hawa hawaelewi cha pinda au yoyote yule sasa atafanyeje? na kule TRA atambana nao vipi, usisau yeye ndiye msimamizi wa serikali?
 
Back
Top Bottom