Pinda: Ngeleja ni kiongozi jasiri na mwadilifu



[h=2][/h]ALHAMISI, SEPTEMBA 13, 2012 05:18 NA JOHN MADUHU, MWANZA

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amemmwagia sifa Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, kuwa ni mmojawapo wa vijana wachapa kazi na jasiri na kumfananisha na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, aliyewahi kujiuzulu uwaziri.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Sengerema katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sengerema, wakati akiwa katika ziara ya kuitembelea wilaya hiyo.

Aliwataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanamtumia Ngeleja kuwaletea maendeleo na kueleza kuwa Taifa bado linamuhitaji kutokana na mchango wake.

Alisema katika jambo la nadra kutokea hapa nchini, baada ya Ngeleja kuondoka katika Baraza la Mawaziri kutokana na mabadiliko yaliyofanywa alimuandikia barua Rais Jakaya Kikwete na kumshukuru kutokana na kumuamini na kumsaidia kama Waziri wa Nishati na Madini kwa muda wa miaka mitano.

“Kwa kufanya hilo, Ngeleja alionyesha ujasiri wa hali ya juu, hivyo namfananisha na mzee wetu, Rais Mwinyi ambaye aliamua kujiuzulu nyadhifa alizokuwa nazo, ingawaje hakuhusika na jambo lolote lililokuwa limetokea na baadaye alikuja kuwa rais.

“Chama na Serikali baada ya kuona kelele zimezidi viliamua kuchukua hatua kwa wale waliokuwa wakilalamikiwa ingawaje hawakuhusika na lolote, lengo lilikuwa ni kuondoa malumbano, mimi nimekuwa mshauri mkuu wa Ngeleja pia namuamini ni mchapa kazi mzuri,” alisema Pinda.

Alisema katika kuhakikisha Serikali inaondoa kero za wananchi wa Sengerema, tayari Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 350 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi aliyekuwa akijenga kilomita tano za barabara za Sengerema na kueleza itaongeza kilomita nyingine nne za lami.

Alisema Serikali inatarajia kuweka lami nyepesi kwa barabara ya Kamanga- Sengerema yenye urefu wa kilomita 35 kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Sengerema.

Kuhusu maji, alisema Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanatarajia kuupatia Mji wa Sengerema majisafi na salama katika mradi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo utawanufaisha wakazi wa Nyatukala, Mwabaruhi, Tabaruka na Nyampulukano.

Awali, Ngeleja alimueleza Pinda kuwa wananchi wa Sengerema wanakabiliwa na tatizo sugu la majisafi na salama na kuiomba Serikali kuhakikisha inatatua tatizo hilo.

 

Fair and Square for CCM to protect the EMPIRE; they cannot dare to disown him to resemble CHADEMA's courage...
 
kuelekea 2015 watamwagiana sifa hata kuitana mitume au nabii.Mmesahau AESH HILALY alisema JK ni mungu baba na yeye ni yesu na diwani wa CCM ni Roho mtakatifu.MAJI YAMESHAZIDI UNGA
 
CHAMA CHA WAJINGA sikutegemea aseme tofauti kwakua wanaungwa mkono na wajinga hayo ndio matokeo yake, AMKENI
 
Pinda asingesema hivyo ningemshangaa. Huo ndio utamaduni na "maadili" ya ki-CCM. Kikwete alisema hajaona kama Lowassa na pia Mramba ni kibeberu! Hahahaaa na Rostam ni mzalendo halisi! Kamusi ya CCM sio kama ya Watanzania wengine.

Mijizi na mihalifu inaheshimiwa sana CCM. Ila raia wema ni adui zao wakubwa.

Lakini patakucha tu na lazima sote tuone nuru ya ukombozi ktk Tanzania. GOD is faithful!
 
yani pinda huwa na mfananina na .................................... yani ningeweza kuandika hicho kitu najua mod hataniacha ila yanii ni mze................, mpu........................ kazub...................... yuko kama lafa. yani anadhalilisha lile kundi la watu wa enzi za mwal nyerere.
 
Ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Sengerema.

Source: Gazeti la Uhuru

Pinda anazeeka vibaya huo mfano wa Mwinyi na Ngeleja hakuna hata ukaribu.mwinyi aliwajibika kwa kujiuzulu,Je ngeleja alishawahi kujiuzulu?Hilo la kuandika barua halina uhusiano wowote na ujasiri au uchapakazi bali ni ustarabu wa kawaida kumshuru aliyekupa nafasi.
Lakini sishangai coz hata JK kwenye kampeni aliwamwagia sifa lowasa,rostam,chenge na mramba
Poor Pinda...Poor uhuru
 
Tumeshawazoea hao magamba kwa kuwaogopa waovu hivyo hayo maneno ni ya mdomoni tu ila moyoni anamaanisha mengine kabisa, ni kama kumsifia mwanaume aliefumaniwa kuwa ni dume la mbegu. SHAME ON THEM!.
 
pinda ar u out of ur mind?dats why ulikuja jion xana uculizwe hata maswali?kiongoz gan mwadilifu asiye ka hata ofcn wanasengerema ni kaz kumpata na kutatua kero zao.a leader z born a leader not by influence of money lik him.pinda open ur eyez coz the end justifiez the meanz unamaliza vibaya.
 
Kuna haja ya kumfanyia Pinda psychiriatic evaluation maana tunaweza kuwa na waziri mkuu ambaye ni mental unstable.
 
vipi alikua akilia wakati anayasema haya, anashangaa au kanuna??? maana jamaa haeleweki

back to topic, yawezekana kwa "pindameter" Ngeleja ni muadilifu kuliko pinda (anayeuza kule kwao kama njugu) na jasiri kuliko pinda anayelia-lia
 
Back
Top Bottom