Pinda: Ngeleja ni kiongozi jasiri na mwadilifu

nyangasese

Senior Member
Aug 21, 2011
129
22
Ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Sengerema.

Source: Gazeti la Uhuru



ALHAMISI, SEPTEMBA 13, 2012 05:18 NA JOHN MADUHU, MWANZA

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amemmwagia sifa Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, kuwa ni mmojawapo wa vijana wachapa kazi na jasiri na kumfananisha na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, aliyewahi kujiuzulu uwaziri.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Sengerema katika Viwanja vya Shule ya Msingi Sengerema, wakati akiwa katika ziara ya kuitembelea wilaya hiyo.

Aliwataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanamtumia Ngeleja kuwaletea maendeleo na kueleza kuwa Taifa bado linamuhitaji kutokana na mchango wake.

Alisema katika jambo la nadra kutokea hapa nchini, baada ya Ngeleja kuondoka katika Baraza la Mawaziri kutokana na mabadiliko yaliyofanywa alimuandikia barua Rais Jakaya Kikwete na kumshukuru kutokana na kumuamini na kumsaidia kama Waziri wa Nishati na Madini kwa muda wa miaka mitano.

"Kwa kufanya hilo, Ngeleja alionyesha ujasiri wa hali ya juu, hivyo namfananisha na mzee wetu, Rais Mwinyi ambaye aliamua kujiuzulu nyadhifa alizokuwa nazo, ingawaje hakuhusika na jambo lolote lililokuwa limetokea na baadaye alikuja kuwa rais.

"Chama na Serikali baada ya kuona kelele zimezidi viliamua kuchukua hatua kwa wale waliokuwa wakilalamikiwa ingawaje hawakuhusika na lolote, lengo lilikuwa ni kuondoa malumbano, mimi nimekuwa mshauri mkuu wa Ngeleja pia namuamini ni mchapa kazi mzuri," alisema Pinda.

Alisema katika kuhakikisha Serikali inaondoa kero za wananchi wa Sengerema, tayari Serikali imetoa kiasi cha Sh milioni 350 kwa ajili ya kumlipa mkandarasi aliyekuwa akijenga kilomita tano za barabara za Sengerema na kueleza itaongeza kilomita nyingine nne za lami.

Alisema Serikali inatarajia kuweka lami nyepesi kwa barabara ya Kamanga- Sengerema yenye urefu wa kilomita 35 kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Sengerema.

Kuhusu maji, alisema Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanatarajia kuupatia Mji wa Sengerema majisafi na salama katika mradi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo utawanufaisha wakazi wa Nyatukala, Mwabaruhi, Tabaruka na Nyampulukano.

Awali, Ngeleja alimueleza Pinda kuwa wananchi wa Sengerema wanakabiliwa na tatizo sugu la majisafi na salama na kuiomba Serikali kuhakikisha inatatua tatizo hilo.

 
Ulitarajia tofauti!??, hata mkulu alimnadi Mramba kuwa ni mchapakazi na mwadilifu afu keshokutwa yake kampeleka mahakamani!, they are kinda possessed!
 
nyie mlitaka aseme nini? Hata wakiamua kumfanyia karamu ikulu. Who care? Ilimuradi keshaondoka na mgawo wake unaoumiza wananchi. Hata wakitaka wamtunuku udaktari wa uadilifu ni wao tu . Ccm oyeee
 
nyie mlitaka aseme nini? Hata wakiamua kumfanyia karamu ikulu. Who care? Ilimuradi keshaondoka na mgawo wake unaoumiza wananchi. Hata wakitaka wamtunuku udaktari wa uadilifu ni wao tu . Ccm oyeee

hoyeeeee!
 
Amemlinganisha na Mijangili mingine ndani ya Magamba. Maana jirani yake ambaye pia ni mdogo wake kiumri Maige ameondoka na jumba la bilioni Saba!
 
Kutengeneza mgao wa umeme, na kuacha watanzania kibao wakifariki mahospitalini wengine wakihangaika na mfumuko wa bei kunahitaji Ujasiri jamani, ndio Pinda anachomaanisha
 
Nchi hii ukiwa mwizi ndio unasifiwa kwa hiyo Pinda naye lazima asifie mwizi mwenzie
 
jk alimsafisha chenge ufisadi wa rada ambayo dunia nzima inajua chenge na majambazi wenzake walipiga hela...kuna kampuni fulani kubwa pale mikocheni ambapo ridhiwani na mke wa pinda wanagongana mara kwa mara kukutana na yule bilionea mwenye hiyo kampuni,..am doing my homework kupitia informers wangu mle ndani na nikipata ushahidi nitaanika ufisadi mzito wa pinda...eti huyu bilionea biashara yake ni kuchimba visima vya maji na kuuza,..kuna tetesi jamaa anauza powder,silaha za kivita jeshini etc
 
Ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Sengerema.

Source: Gazeti la Uhuru

Duh huyu mtoto wa mkulima naye naona sasa anazeeka vibaya na nadhani hili jina halimfai tena ni bora akaitwa mtoto wa kifisadi.Alianza vizuri but naona upepo wa kifisadi umemuelemea na harufu ya pesa imeshamlevya
 
Huo ndo uzuri wa viongozi wa serikali yetu,wanajiandaa kuachia madaraka kwa kuexpose weaknes zao ili iwe rahisi kwa wananchi kuwahukumu kirahisi. Pinda! Mtoto wa mkulima! Shame on you....
 
siasa zinaendeshwa na watu confused? Pinda anajua ukubwa wa statement aliyoisema au alinukuliwa vibaya?
 
Ngeleja mwadilifu? Hii nchi ifanywe kama mradi wa KIGAMBONI tukaishi uhamishoni labda wajukuu wetu watapata uraia halali wa huko.
 
walivyomwua-wangosi.JPG

liwalo na liwe
 
Haya ndo mambo yanayoiponza Serikali ya CCM, katika nchi serious, hukuti mambo kama haya ya kuwasafisha viongozi walioharibu.
 
Sasa na wewe mzeee unataka kujishushia hadhi, huyo ngeleja ana usafi gani?????????????? Hebu achana na mafisadi watakusababishia ustaafu bila heshima
 
ziara yake hata haina maana ukimsikiliza utaona ni hadithi tu zilezile hawana lolote wanalofanya labda kutembea tu kuijua tanzania...
kwa mfano anasema wnanchi wajiunge vikundi wapewe mikopo je nani kamuachia jukumu hilo? akiondoka tu hakuna lolote...ukijaribu kuunda kikundi utakavyo pata shida ya kusajili na kupata mkopo mwenyewe utarudi home kulala
 
Back
Top Bottom