Pinda naye kwa ahadi za kushughulikia mafisadi!

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuenzi ushauri aliopewa na waumini wenzake wa kutoogopa kufanya maamuzi wakati akitekeleza majukumu katika nafasi yake mpya ya Uwaziri Mkuu.

Alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na waumini waliohudhuria ibada yake ya shukrani iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Anna, Parokia ya Hananasif, Kinondoni, Dar es Salaam.

“Nimeambiwa na Mwenyekiti wa Parokia kwamba kwenye Biblia neno usiogope limeandikwa mara 365, nami nina hakika nikisema kila siku ‘Pinda usiogope’ watu watapata walichokitarajia… katika utumishi wangu nitaenzi ushauri ambao wanaparokia wenzangu mmenipatia.”

Katika ibada hiyo iliyoongozwa na mapadri saba, Waziri Mkuu Pinda aliwaeleza waumini wenzake kwamba yote yaliyotokea ameyachukulia kama changamoto na kwamba cha msingi ni kwa wote kujiuliza ni kwa nini yametokea.

“Kitu kimoja ni dhahiri, Watanzania hawakufurahia jinsi Serikali ilivyokuwa ikisimamia shughuli zake ndiyo maana tukafika hapo… changamoto kubwa tuliyonayo viongozi ni kurejesha imani iliyopotea miongoni mwa Watanzania,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema: “Leo ni siku ya 16 tangu nilipoapishwa na siku ya 17 tangu Mheshimiwa Rais ateue jina langu ili lithibitishwe na wabunge, ni kipindi kifupi sana … mengi yamesemwa, mengi yamefanyika na maandamano juu kana kwamba yaliyofanyika hayakutosha… Yaliyotokea ni funzo, tunapaswa kuhakikisha hayarudii tena…,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Alisema Serikali itahakikisha waliohusika kuifikisha hali ilipo sasa, wanachukuliwa hatua za kisheria kwani sivyo walivyotumwa kufanya.

Haya wana JF, tusubiri tuone au kutakuwa na janjajanja ya kuendelea kumsafuisha Lowassa ambaye Pinda amekuwa akisema ni kaka yae, ni bosi wake, ni mtu aliyemfundisha kazi na kwamba atafuata kila alichokuwa akikifanya Lowassa (sijui ni pamoja na mambo yetu yale au?). Tusubiri!
 
Back
Top Bottom