Pinda naye asema HAJUI kwanini watanzania ni maskini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda naye asema HAJUI kwanini watanzania ni maskini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 31, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,413
  Likes Received: 81,452
  Trophy Points: 280
  Eti Waziri Mkuu hajui umaskini wa Watanzania unasababishwa na nini? Halafu anataka ufanywe utafiti ili kugundua chanzo cha umaskini wa Watanzania! Waziri Mkuu wa nchi baada ya miaka 50 ya uhuru hajui umaskini wa Wananchi wake unasabababishwa na nini!

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  Pinda asema hajui kwanini Watanzania ni maskini

  Wednesday, 30 March 2011

  Raymond Kaminyoge

  Mwananchi


  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa), kufanya utafiti ili kufahamu kwa nini wananchi wa kawaida wanalalamikia hali ngumu ya maisha wakati kitaifa, uchumi unakua.

  Pinda alisema hayo Dar es Salaam jana, wakati akifungua mkutano wa 16 wa taasisi hiyo uliowashirikisha watafiti wa masuala ya uchumi.


  Alisema tafiti hizo zikifanyika zitaisadia Serikali kuchukua hatua kuboresha maisha ya wananchi wake…
  "Repoa fanyieni kazi utafiti huu. Watu wanalalamika ugumu wa maisha, hatuwezi kukaa kimya tutafiti inakuwaje uchumi unakua lakini watu wanalalamika maisha ni magumu!" (Toba!) Kwa mujibu wa Pinda Serikali imekuwa ikitumia matokeo ya tafiti za Repoa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo akasisitiza kuwa utafiti kuhusu hali ya umaskini nchini nao ni muhimu.

  "Naomba niwapongeze kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya, Serikali inajivunia tafiti ambazo zinafanywa na taasisi hii," alisema. Aliitaka taasisi hiyo kujikita zaidi kwenye sekta za kilimo na mifungo kwani hayo ni maeneo ambayo wananchi wanayategemea katika kujiajiri.


  "Mkifanya utafiti kwa mfano, katika eneo la ufugaji wa nyuki, matokeo ya utafiti huo yatasaidia wananchi katika kuongeza maarifa na hivyo kujikwamua na umaskini," alisema.


  Aliitaka Repoa kufanya utafiti kufahamu ni kwa nini wasomi nchini hawataki kujiajiri kwenye sekta ya kilimo.


  "Mtueleze Serikali ifanye nini ili wasomi hawa waweze kuvutiwa na kwenda kujiajiri katika kilimo badala ya kutegemea kuajiriwa kwenye ofisi kubwa mijini," alisema.

  Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Repoa, Profesa Samwel Wangwe alisema tangu taasisi hiyo ianzishwe mwaka 1995, imeshafanya tafiti 90 (soma hizi ripoti badala ya kukurupuka!)zinazohusu umaskini na kupendekeza njia ya kuondokana nao.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Inanikumbusha yule malkia aliyekuwa hajui kwa nini wananchi wake wanalalamika hakuna mikate. Naona hapo Wangwe kamjibu kistaarabu kweli kweli.
   
 3. mtaratibuuuuuu

  mtaratibuuuuuu Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni ajabu sana lakini, maana wote ni walewale..................Muungwana asingeweza mteua msimamizi mkuu wa shughuli za serikali yake mwenye kujua zaidi yake. Ilibidi apate wa mfano wake..........ikiwa ni kukwepa pia asizidiwe spidi..................................................................TANZANIA TANZANIA
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu pinda hafai kuwa hata mwenyekiti wa kijiji.
   
 5. m

  magee Senior Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  shame on them....Pinda of all the peopple hajuo umasikini wetu unatoka na nn??yeye ambaye anaaccess kubwa na information mbali mbali,UN reports,WB,IMF,FAO.....mmh mtanzania kweli huyu?alienda shule kweli?wanataka kujitengenezea ulaji mwingine,sasa hv utasikia tumetenga fungu kwaajili ya research!its pity!
   
 6. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante sana!lakini siyo yeye tu,karibu viongozi wote wa serikali hawafai kuwa hapo walipo!wengi wao hawajui wamefikaje hapo,
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Watajuaje umaskini wa watanzania wakati wao kila kitu wanapata tena bure,sioni ajabu kwa waziri mkuu kusema hivyo maana hata raisi aliwahi kuulizwa kwanini nchi yake bado ni maskini,akajibu hata yeye hajui.
   
 8. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nashindwa kujua aina ya viongozi tulionao hapa Tanzania. Kuanzia Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu na wengineo wote wanabakia kulalama na kusema hawajui sababu za matatizo yanayowasibu Watanzania.

  Hivi kweli inahitajika REPOA wafanye utafiti wa kwa nini Watanzania wanalalamika kuhusu hali ngumu ya maisha kama Mhe. Pinda anavyodai? Ama wanaona Watanzania wote kuwe ni limbukeni. Jaribu kufikiri ni kiasi gani cha fedha kinachotumiwa na hizi taasisi za utafiti kwa masuala ambayo yako wazi na pale ripoti zinapotolewa zinaishia kupigwa vumbi kwenye makabati.


  Chanzo Gazeti la Mwananchi:
  Pinda asema hajui kwa nini Watanzania ni maskini
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  huyu mtu ameshajisahau baada ya sasa kuwa na uhakika na afya yake, anaudhi hata kumsoma ama kumsikiliza
   
 10. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Inakera ,inachefua kuongozwa na watu kama hawa ....Lakini inasikitisha zaidi kama sisi wenye akili tunaendelea kuwalea viongozi wajinga! Inawzekana sisi watawaliwa ndio wajinga zaidi!? Ndio maana mm naamini kwa hali ilivyo sasa unaweza kumwekaPunda akawa rais na mbwa akawa waziri mkuu wa Tanzania,na TANZANIA YA AINA HII IKAWEPO .
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wednesday, 30 March 2011 21:22
  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (Repoa), kufanya utafiti ili kufahamu kwa nini wananchi wa kawaida wanalalamikia hali ngumu ya maisha wakati kitaifa, uchumi unakua.

  Pinda alisema hayo Dar es Salaam jana, wakati akifungua mkutano wa 16 wa taasisi hiyo uliowashirikisha watafiti wa masuala ya uchumi.

  Alisema tafiti hizo zikifanyika zitaisadia Serikali kuchukua hatua kuboresha maisha ya wananchi wake… "Repoa fanyieni kazi utafiti huu. Watu wanalalamika ugumu wa maisha, hatuwezi kukaa kimya tutafiti inakuwaje uchumi unakua lakini watu wanalalamika maisha ni magumu!" Kwa mujibu wa Pinda Serikali imekuwa ikitumia matokeo ya tafiti za Repoa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo akasisitiza kuwa utafiti kuhusu hali ya umaskini nchini nao ni muhimu.

  "Naomba niwapongeze kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya, Serikali inajivunia tafiti ambazo zinafanywa na taasisi hii," alisema. Aliitaka taasisi hiyo kujikita zaidi kwenye sekta za kilimo na mifungo kwani hayo ni maeneo ambayo wananchi wanayategemea katika kujiajiri.

  "Mkifanya utafiti kwa mfano, katika eneo la ufugaji wa nyuki, matokeo ya utafiti huo yatasaidia wananchi katika kuongeza maarifa na hivyo kujikwamua na umaskini," alisema.

  Aliitaka Repoa kufanya utafiti kufahamu ni kwa nini wasomi nchini hawataki kujiajiri kwenye sekta ya kilimo.
  "Mtueleze Serikali ifanye nini ili wasomi hawa waweze kuvutiwa na kwenda kujiajiri katika kilimo badala ya kutegemea kuajiriwa kwenye ofisi kubwa mijini," alisema.

  Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Repoa, Profesa Samwel Wangwe alisema tangu taasisi hiyo ianzishwe mwaka 1995, imeshafanya tafiti 90 zinazohusu umaskini na kupendekeza njia ya kuondokana nao.

  Source:Mwananchi

  My take:
  Prezidaa anashangaa, PM nae anashangaa, kila mtu anashangaa kwa nini sisi ni masikini!! Mbombo ngafu!
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Another shame on 'SIJUI'
   
 13. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mramba akiwa waziri wa Fedha nae alisemaga hajui kwa nini Tanzania ni maskini, msanii JK nae hivyo hivyo, kiranja mkuu a.k.a shock absorber nae anasema hajui.......... nikiwa mdogo kuna siku mjomba wangu nilikua nimeenda mtembelea alinikuta nimekaa kwenye katika maongezi akaniambia KAMA UMEKAA KWENYE HIKO KITI NA HUJUI KWANINI UMEKAA HAPO, UTAKUA NI MJINGA - very philosophical.... na mwenye akili atajua maana ake...... Pinda anachosema hata hao REPOA wakimpa hiyo tafiti bado atauliza kwa nini hizo sababu za umaskini zipo?

  Hivi anaendaga na ndege Bungeni? Driving from Dar Es Salaam to Dom could tell someone the miserable life our brothers and sisters are living. Badala ya REPOA wamfanyie tafiti kwa nini Pinda asijiulize on a way to Dom what has changed kutoka Pwani hadi Dodoma? Zaidi ya desertification, nyumba za nyasi zile zile etc........ kweli akutukanae hakuchagulii tusi............. Kuna malkia wa ufaransa nafikiri.... kuna wakati wanachi waliandamana mikate haipatikani - akiwa kwenye balcony akauliza kama mikate ni shida kwanini wasile keki? Ndio haya ya Pinda........
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280


  Hivi kwa nini yeye au watoto wake wasituonyeshe mfano wa kwenda kujiajili kwenye kilimo badala ya kukaa maofisini. Yeye kakaa ikulu miaka kibao. Alipoona anakaribia kustaafu akakimbilia kwenye siasa, sasa leo anataka sisi watoto wa walala hoi ndiyo tukajiajili wakati watoto wao wanaajiriwa BOT na kwenye commercial banks.
   
 15. N

  Newvision JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hajui ndiyo maana hana mikakati madhubuti ya kuiokoa nchi yetu katika lindi la umaskini. Je ni kweli hajui kwanini kule kijijini kwake watu ni maskini au ni kwa sababu tu natembea kwenye VX na kiyoyozi siku zote????????????? Ananitapisha
   
 16. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii inashangaza kama viongozi wakuu wa nchi wanakuwa hawajui kwa vipi watanzania bado wanazama katika lindi la umasikini kila kukicha!!!!!!!!! Utaongozaje sera za nchi kuwaondoa watu katika umasikini unaokithiri??? bofya,
  Pinda asema hajui kwa nini Watanzania ni maskini.

  Kama alivyo mhe. rais jk ndivyo alivyo waziri mkuu wake. uongozi wa ukasuku-kukariri kila alichosema mkuu wa nchi bila kujua mstakabari wake..."like a father, like a son"!!! Labda ni vema wana jf tusaidiane kuainisha sababu za umasikini unaozidi kukithiri kwa watanzania waliowengi badala ya kusubiri taarifa (report) za tafiti za "repoa"-which mostly do not reflect realities any way!!
   
 17. m

  mtimbwafs Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni unafiki wa kisiasa hivi ni kweli kuwa viongozi wetu wakuu hawajui ni kwa nini sisi maskini?. Hapana narudia tena hapana tuna wachumi wakutosha na Tafiti zimefanyika nyingi za kutosha na sababu lukuki zimetolewa lakini zimewekwa makabatini tu basi. Hii haiwezekani lazima viongozi hawa watuambie sababu na si kujifanya hawazijui sababu.
   
 18. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kama mkuu wake wa kazi nae hakujua recession/credit crunch ina affect vipi nchi yake, tusitegemee miujiza kutoka kwa huyu mtoto wa mkulima.wanachefuaaaaaa :yuck:..kazi kuchekacheka tuuu..mxiii
   
 19. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hii tabia ya viongozi wa juu kusema hawajui tatizo la umaskini wa nchi yetu ni sawa na kufanya research without a problem statement..!

  NUTCASES ........!
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  wakati pinda anaapishwa kuwa Waziri Mkuu, nilijua sasa Tanzania tumepata kiongozi shupavu, mwajibikaji na ambaye yupo makini.
  Lakini kadri muda unavyozidi kwenda Lo!!
  Mara alilie lie bungeni, siasa zimekuwa nyiingi kuliko vitendo.
   
Loading...