Kwa mfumo wa uundwaji serikali ulivyo sasa, ambapo Rais anateua Waziri mkuu na "kuthibitishwa" na bunge lkn pia anateua mawaziri wengine wote, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi, makatibu wakuu wa wizara, wakuu wa mashirika, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, n.k ni vigumu waziri kumuwajibisha mtendaji aliye chini yake. Mfano bungeni Hawa Ghasia katajawa na kamanda Sugu kuwa ana majibu ya jeuri kwa kuwa tu anaelewana na mama Salma. Hii ina tafsiri nyingi sana. Moja ni kwamba Ghasia anajua kwa kuwa karibu na mke wa rais kibarua chake kiko salama zaidi. Hawezi kuwajibishwa hata na Waziri mkuu. Mifano kama hii iko mingi kwa ngazi zote. Ndiyo maana Pinda akasema uwaziri mkuu ni msalaba. Kwa sababu anaongoza mawaziri ambao yy hana mamlaka ya kuwafuta kazi. Waziri naye chini kuna tatizo kama hilo. Kwahiyo tatizo lipo kwenye mfumo.
Kinachofanywa na CC ya CCM ni kucheza karata ya uchaguzi mkuu ujao. Kwa kuwachafua mawaziri na hatimaye kuwavua madaraka ionekane ati CCM nayo inawajibisha. Ni mpango mkakati wa CCM KUJISAFISHA KWA DAMU YA AKINA PINDA. Kwa kusema hivi c kwamba nawaunga mkono mawaziri. Laa! Hasha. Ninachokisema tatizo ni serikali nzima tukianza na rais kwa kuteua mtu eti kisa ni rafiki wa mwanaye, mkwewe, mkewe, n.k