Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda na Makinda wameshindwa kutimiza wajibu wa waziri mkuu na Spika bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Feb 11, 2011.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa waliomwona na kumsikiliza Pinda akielezea kuhusu mauaji ya Arusha watahitimisha bila shaka yoyote kuwa ni mnafiki na ana tabia inayofanana na Paka. Anaoongea mambo yasiyothibitishwa huku amepindisha mwili na shingo upande mmoja na kuonyesha sura ya kutaka kuonewa huruma kama njia ya kuwahadaa watu wakubali anachoeleza. Chadema walimtega Pinda, kwa unafiki wake akalieleza bunge eti wenye makosa ni Chadema huku akijua kuwa kesi ya mauaji ya Arusha iko mahakamani. Kama Pinda asingekuwa mnafiki basi angeacha kujibu maswali kuhusu mauaji ya watu Arusha yaliyofanywa na Polisi kwa kuwa suala hilo liko mahakamani. Pinda alitakiwa akatae kama Makinda alivyokataa hoja ya Dowans kwa kisingizio cha eti kesi iko mahakamani. Ndiyo, ni visingizio tu vya kulinda mafisadi kwa sababu kamati ya wabunge wa CCM hivi karibuni ilijadili suala la Dowans na kuiambia serikali ya CCM isiilipe Dowans ya Rostam huku suala hilo likiwa mahakamani tayari. Kwa nini Makinda anakataa Dowans isijadiliwe bungeni wakati wao CCM wamelijadili katika kamati ya wabunge?

  [FONT=&quot]Kwa upande wake Pinda anataka watanzania waamini kuwa Polisi wa CCM hawakuua raia wasiokuwa na makosa Arusha huku akijua kesi iko mahakani. Ni mara ngapi polisi wanaua raia na kushiriki katika ujambazi?. Je hajui kuwa hivi karibuni kwa mfano kuna askari Polisi aliyempiga risasi dereva wa teksi na kumnyanganya gari kisha kwenda kupora pesa kituo cha Mafuta huko Arusha?. Hajui kuwa Polisi wa CCM wanashiriki uhalifu kama walivyo majambazi? Kwa hiyo Pinda anaishawishi mahakama ihukumu kuwa Polisi hawakuua bali wenye makosa ni Chadema, je huku si kuingilia uhuru wa mahakama? Makinda naye anafoka na kuonyesha chuki kwa Chadema huku amekalia kiti cha uspika. Anahamaki kama mama anayemfokea mtumishi wa ndani kumbe anamtetea Pinda. Kwa hiyo Makinda anaungana na Pinda kuishawishi mahakama kuwa Chadema ndiyo wenye makosa. Hivi ni tabia gani ya spika kuhemkwa, kufura na kuwafokea Wabunge hasa wa Chadema kana kwamba anashughulika na mambo ya nyumbani kwake?. Kwa hakika tabia ya Makinda haiendani na cheo cha uspika na Watanzania tumshauri ajiuzuru uspika kabla hajaendelea kuliharibu zaidi bunge. Bunge la Sitta ndiyo lilikuwa bunge la maana kwa Watanzania, hili la Makinda naona ni la kutetea Mafisadi tu. Tabia mbaya ya Pinda na Makinda kutetea mafisadi na uovu wa serikali inatisha na inazidi kuota mizizi. Clip ya video yaweza kuthibitisha kuwa Pinda kweli ni mnafiki na anatabia ya paka, na kwamba Makinda ana chuki kwa Chadema na Watanzania, chuki iliyopitiliza na wanalinda mafisadi hata kushindwa kutimiza wajibu wao wa uwaziri mkuu na uspika.[/FONT]
   
 2. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods naomba msaidie kuhariri aya ya pili ili herufi zifanane na za aya ya kwanza.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  :coffee:
   
 4. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hebu tupe kesi iliyoko mahakamani ni ipi? Je ni ile ya viongozi wa Chadema kushitakiwa kwa kukaidi amri ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano au ni kuhusiana na mauaji? au ni zote?
   
 5. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ikiwa chama chao kimeshindwa kuleta maendeleo ya nchi unategemea hao 2 wataweza tena wajeuri kama Fisadi Kikwete[/B]
   
Loading...