Pinda na Makinda wamefanikiwa kuposha mjadala wa posho za wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda na Makinda wamefanikiwa kuposha mjadala wa posho za wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mechard Rwizile, Feb 9, 2012.

 1. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 80
  Nina uhakika wa kutosha posho za wabunge hazikuwa zimepandishwa. Ndio maana katibu wa Bunge anashikilia msimamo kuwa posho hazikuwahi kupandishwa. Mgogoro ulianza baada ya gazeti la mwanahalisi kuonyesha hati ya malipo aliyoitumia Jairo, katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Nishati kuwalipa posho Pinda na Makinda ya shilingi 280,000 kwa siku wakati wa semina ya wabunge. Baada ya kuonekana malipo hayo, watu walianza kuhoji inakuwaje waziri mkuu na spika wa bunge wakubali posho ya shs. 280,000 kwa siku? Wametumia viwango gani? Na viwango hivyo viliidhinishwa na nani?

  Ili kujiepusha na aibu hiyo, hoja ya kupandishwa posho za wabunge ikaanzishwa na Makinda mwenyewe! Dhambi hii imezua mambo makubwa na ya hatari kwa taifa hili. Nina uhakika hata suala la madaktari kutaka kupandisha posho na mishahara yao katika wakati huu zimechochewa na upandishaji wa posho usiozingatia taratibu na hali halisi ya maisha ya watanzania. Matokeo ya mgomo wa madaktari ni makubwa, watu wamekufa, wengine watapata ulemavu ambao usingetokea kama sio mgomo huu.

  Ni adhabu gani watu hawa wanastahili? Tuache ipite tu?
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wabunge wapo kwa maslahi yao sio kwa maslahi ya wananchi huo ndiyo ukweli.
   
Loading...